Ili tuendelee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili tuendelee

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mshiiri, Dec 7, 2008.

 1. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Maendeleo
  "ili tuendeleee tunahitaji vitu vinne watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
  Tanzania tunakosa nini hapa? Watu, hapana. Siasa safi, hapana na UONGOZI BORA sidhani. Wana JF hebu tuichambue hii policy statement kisha tujue nini kinakosekana nchi yenye rasilimali nyingi kuwa maskini kunuka mkiani. Si ajabu hata Zimbabwe na matatizo yote kimsingi hatuipiti kwa utajiri. It is a deadly funny!

  Mfano
  Nchi kama Norway ina population 5mil people na haina ardhi, wala rasilimali zozote ni barafu karibu mwaka mzima, hamna kilimo wala madini, wala utalii kama Tanzania, wala misitu wala mito. There is completely NOTHING but is among the richest countries in the world na hata inasaidia Tanzania pesa. Norway shule na afya ni bure hadi PhD na ingawa hawana utajiri wa rasilimali kama Tanzania. Sasa tena huu mtindo wa kukataa kuwapatia fedha za mikopo wanafunzi wetu na afya wakidai ni shinikizo la mataifa hisani je Norway iko Mars?

  Kosa kubwa
  Viongozi wetu pia wameifanya serikali yetu iwe na uvivu kama akili zao kuwa eti serikali haifanyi biashara na wengine kufanya biasara hizo on behalf. Viongozi wetu ni chanzo cha kufa kwa viwanda vyote nchini hat bora shoes, tanganyika packers, general tyre, baby food, nmc, kiltex, mt meru hotel, bwawani hotel etc kwa uchache sana; hata kuvitaja nafikiri kama kuna kiongozi atakayesoma hii thread atakubali na kukiri kuwa akili zao zina hitilafu.
  Ajira za kudumu zaidi ya uhitaji wa watanzania zingeweza kutoka katika hivi viwanda vyetu walivyovi-ground na kisha kupeana kishemeji, kishkaji, na kiwizi-wizi. Again I fail to see whether we have UONGOZI BORA (good governance)

  Wizi mtupu
  Wizi mtupu!! NASEMA wizi mtupu! Na naongeza na uvivu wa kufikiri; anasa na wanawake, ufisadi, rushwa, kusema uongo yaani udanganyifu, ukaidi, usaliti, ukosefu wa uzalendo, uonevu, udhulumishi, kwa baadhi ya wengi wa viongozi wetu. Kufikia hapa nashindwa kuikubalia nafsi yangu kuwa TANZANIA tumekosa UONGOZI BORA. Michango zaidi jamvini.
   
 2. A

  Adili JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,017
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Mshiiri,

  Norway wana samaki (ufugaji wa salmon) kuliko yeyote ulaya, wana misitu, na cha zaidi tangu 1971 wanapump petroleum. Kwa sasa hivi Norway ni nchi pekee ulaya isiyokuwa na deni. Tofauti na nchi nyingi,mapato kutokana na mafuta wanayatunza kwa ajiri ya vizazi vijavyo. Hata kwa wazungu wenzao, Norwegian wako tofauti kwenye maswali ya utunzaji wa rasilimali zao.
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Any ideas?
   
Loading...