Ili Tanzania ifike mbali kiuchumi

mtingi1

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
945
923
Wasalaam!

Kama mada inajieleza , ili nchi yetu ifike mbali zaidi KIUCHUMI na technology, hatuna budi kuwaiga wachina;

1. Namna wanavyopiga kazi kwa bidii. Tusiige imani zao tu.

2. Namna wameweka kando ustaarabuwa magharibi yaani mfumo wa democracy binafsi naona unazingua waafrika tu, sisi tulizoea mfumo wa kifalme au ki chifu, bora mfumo wetu wa ki chifu kuliko u democracy. Tusiige utaratibu wao wa kuzaliana, sisi tuendelee kuzaliana sana.

4. Tuwakuze wanasayansi wetu, kwa kuwekeza fedha zaidi katika tafiti za kisayansi ili ikiwezekana baada ya muda flani na sisituwauzie wazungu madawa, na bidhaa zingine.

5. Tufanye tafiti juu ya bidhaa za kisayansi mfano silaha na vinginevyo ili na sisi tujitenezee vyetu.

Naomba ongeza na wewe pia za kwako....

Tuendelee kujikinga na korona.

Mungu ibariki Tanzania

3.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna chama fulani cha Siasa Tanzania kinaamini bila Mabeberu Nchi haiwezi kuendelea
 
Vyuo vya ufundi viwe kila kila kata ili anaehitimu kidato cha 4 aende veta moja kwa moja fani ziongezwe zakila namna after 15 yrs kutakuwa na watalaamu wengi sana itakuza uchumi wetu
 
Tupunguze riba kwenye taasisi za fedha ili watu waliomaliza elimu ya juu au elimu ya veta waweze kuchukua mikopo na kufanya biashara. Kuwe na mazingira mazuri zaidi ya walio maliza shule waweze kujiajiri
 
Back
Top Bottom