Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nchi za Libya na Misri ziliingia kwenye machafuko kutokana na tamaa za watu wachache na kwa sababu za kijinga jinga. Tanzania tumeanza kunyemelewa na hali hiyo pale tuliporuhusu watu wachache tena wengi wao hawapo nchini wakatawala bongo zetu.
Wakati wa sakata la ESCROW, baadhi ya mawaziri akiwemo Profesa Muhongo walijiuzulu kwa sababu tu ya msukumo kutoka kwa wabunge waliokuwa na maslahi binafsi na hoja hiyo. Nakumbuka mjadala mzito uliotawala kushinikiza Prof Muhongo ajiuzulu. Na alifanya hivyo baada ya kelele kuzidi. Hata hivyo, Rais Magufuli alipoingia madarakani akalazimika kumtejesha tena Muhongo kwenye wizara ile ile. Watu wakavimba mpaka wakapasuka. Sasa mambo ya epoa na umeme unasambaa vijijini.
Lilipokuja sakata la Operesheni TOKOMEZA baadhi ya Mawaziri walitolewa mbuzi kafara. Ni kutokana na kelele za akina Kangi Lugola ambao walienda na rundo la vielelezo bandia ili kuwaangamiza wenzao.
Limekuja suala la madawa ya kulevya. Makonda kaasisi mapambano hayo na sasa Tume ya Kamishna Sianga inafanya kazi kwa wepesi zaidi. Hata hivyo, kama ilivyotokea kwa matukio ya nyuma, lazima isombe watu. Hata hivyo, kwa mara nyingine napongeza msimamo wa Serikali. Jamii yetu imelelewa kimayai mayai sana. I ekuwa legelege aka mdebwedo. Lazima apatikane mtu wa kutunyoosha! Magufuli kiboko ya wazembe. Watatukana sana. Wataandika sana na watapiga kelele sana. Ila hapo wamefika mwisho.
Rais wetu ana kazi kubwa ya kujenga Ma flyovers, reli, mabomba ya mavuta, mabarabara na kuimarisha uchumi wa nchi. Hawezi kupoteza muda kujibizana na masuala ya kipuuzi. Hapa Kazi Tu.