Ile Movie Hii hapa ishaisha

dansmith

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
2,305
2,094
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.

Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.

“Hadi kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.

Mawaziri waliotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye alitakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye alitakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira), Mhe. Luhaga Mpina aliyetakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, FEBRUARI 26, 2016
MICHUZI BLOG at Friday, February 26, 201M
 
Nijuavyo ili MOVIE ipendeze na steringi aonekane yuko vizuri kumkabili mtu yoyote lazima Actors wengine waonekane katika Scene ya mwisho pindi ambacho steringi anonekana kuchoshwa na mikimiki, au pengine haaminiki kwa mtizamaji kama atamaliza MOVIE ,ghafla tu utaona.....majambazi wameweka bunduki chini ...kumbe nyuma ya pazia kulipangwa iwe hivyo....

Ni mtizamo tu...!
 
Nyumbu mnahangaika sana kukosoa mambo ambayo Watanzania tunayataka yatekelezwe. Endeleeni huku mambo yakiendelea kuivaaaaa
 
Nijuavyo ili MOVIE ipendeze na steringi aonekane yuko vizuri kumkabili mtu yoyote lazima Actors wengine waonekane katika Scene ya mwisho pindi ambacho steringi anonekana kuchoshwa na mikimiki, au pengine haaminiki kwa mtizamaji kama atamaliza MOVIE ,ghafla tu utaona.....majambazi wameweka bunduki chini ...kumbe nyuma ya pazia kulipangwa iwe hivyo....

Ni mtizamo tu...!
Mtazamo wako mbovu, umekaa kinafiki, unaleta sarcasm ambayo sio mahali pake. Mahiga alikuwa busy safarini, wengine walikuwa mikoani, wengine kuna data kama za mshahara wao na marupurupu walikuwa hawazifahamu siku walipopewa hizo fomu. Sio kil akitu ukitazame katika mtazamo wa kejeli, sometimes wewe mwenyewe unaweza kuonekana kituko kwa watu ambao wanao uwezo wa kusoma katikati ya mistari, kile unachokiandika.
 
End of part one...
Part two will be more interesting. .
ila wabongo wastahimilivu licha ya sarakasi na kutufanya wajinga tumeeamua tuyaache yatawale. Badala ya kutuonea huruma na kutuheshimu kwa kuficha haya maigizo wao bado wanaendelea tu tena hadharan
 
Back
Top Bottom