Ilani ya CCM ya mwaka 2005 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya CCM ya mwaka 2005

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Mar 19, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nitaanza na mimi mwenyewe kwa kuangalia sera za uchumi CCM iliyo jiwekea kwenye ilani ya 2005. Nanukuu baadhi ya vipengele:

  SURA YA KWANZA
  MAFANIKIO YA KIUCHUMI NA KIJAMII YA MIAKA 10
  YA SERIKALI YA AWAMU YA TATU

  10. Hali ya uchumi na huduma za jamii haikuwa ya kuridhisha wakati Rais Benjamin W. Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995. Ukuaji wa uchumi ulikuwa 3.6%, mfumuko wa bei ulikuwa juu kwa kiwango cha asilimia 27; mapato ya Serikali yalikuwa ya wastani wa shilingi 25 bilioni kwa mwezi;

  12. Katika kipindi hiki cha Awamu ya Tatu ukuaji wa uchumi umefikia asilimia 6.7; mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 27 mwaka 1995 hadi asilimia 4.5 mwaka 2005 mwanzoni; mapato ya Serikali yameongezeka kutoka wastani wa shilingi 25 bilioni kwa mwezi mwaka 1995 hadi shilingi 160 bilioni kwa mwezi katika nusu ya kwanza 2005;

  Hapo juu wameorodhesha hali ya uchumi ilivyo kuwa wakati muheshimiwa Mkapa anaingia madarakani na mafanikio ya awamu yake linapo kuja swala la uchumi. Swali ni je hali ya uchumi wa sasa ikoje ikilinganishwa na hizo figures za wakati wa Mkapa? Awamu ya nne imeboresha hali ya uchumi au uchumi umezidi kushuka? Hapa nahitaji msaada wa wadau mbali mbali ambao wanaweza kutoa statistics za sasa.

  22. Mchakato wa kuitoa nchi yenye uchumi ulio nyuma na tegemezi kama ilivyo Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa kisasa lazima uzingatie vipaumbele vikuu vitatu. Kwanza lazima kuwaandaa kwa elimu, maarifa na mwelekeo watu wenyewe. Rasilimali watu ndiyo nyenzo kuu katika ujenzi wa uchumi wa kisasa.

  Je serikali imefanya nini "kuwaandaa kwa elimu, maarifa na mwelekeo" wananchi? Program zipi zime tumika kutekeleza hili?

  Jambo la pili la kipaumbele katika mchakato wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Kilimo ndicho msingi wa uchumi, kwa hivyo, mapinduzi ya kilimo (pamoja na ufugaji na uvuvi) yanategemea hali halisi ya kila nchi.

  Jambo la pili la kipaumbele katika mchakato wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Kilimo ndicho msingi wa uchumi, kwa hivyo, mapinduzi ya kilimo (pamoja na ufugaji na uvuvi) yanategemea hali halisi ya kila nchi.

  Sijaona kilimo kikipewa kipaumbele ambacho kina sisitizwa hapa. SIjaona mapinduzi yoyote katika kilimo yaliyo fanyika kati ya mwaka 2005 hadi sasa na wala sijaona maendeleo yoyte ya maana. Kilimo umekua mwimbo tokea uhuru lakini bado sekta hii haija imarishwa. Binafsi mimi nafikiri kama kweli tunataka maendeleo kupitia kilimo tusi kazanie kwa walimaji wadogo wadogo bali tuwekeze nguvu kwa kilimo cha hali ya juu ambayo mashamba yatakua ni ya wawekezaji wakubwa wenye teknologia ya kisasa wanaolima bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutoa ajira kwa wananchi. Kukazania wakulima wadogo wadogo kwangu mimi haisaidii uchumi kiujumla. It's time to change strategies.

  Jambo la tatu la kipaumbele katika mchakato wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni mapinduzi ya viwanda na miundombinu ya kisasa. Viwanda ndivyo kiongozi wa uchumi wa kisasa.

  Kama kilimo ndiyo msingi wa uchumi kama walivyo sema hapo juu na viwanda ndiyo kiongozi wa uchumi wa kisasa basi ina leta maana kusema kiwanda vinavyo wekeza katika kilimo ndiyo njia kuu ya kuji komboa kiuchumi. Kuwa na viwanda vingi vya vilimo ina maanisha kuwa na mashamba makubwa ya uwekezaji ambayo yanaweza kusupply material kwa viwanda hivyo.

  Naendelea kusisitiza ulimaji wa kisasa na hali ya juu kwa sababu naona huu mwimbo wa kumuwezesha mkulima mdogo mdogo ni political correctness tu. Siyo kwamba mkulima mdogo asiwezeshwe....lahasha! Bali kama una taka kilimo ambacho kitakua ni industry na gurudumu la maendeleo unahitaji uwekezaji wa hali ya juu ambayo mkulima mdogo mdogo hataweza kumudu.
   
 3. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kwa ujumla ukisoma Ilani yao kwa umakini sana utagundua kuwa;

  a). CCM wanaimba kama malaika- Lakini wanacheza kama Mashetani;
  Hii ilani ni nzuri lakini hakuna aliyeitekeleza, ndiyo maana nikasema kuwa wanaimba kama Malaika ili tuwaone wao ni mabingwa sana na wanaweza kila jambo lakini mwisho wa siku na miaka mitano imetimia hakuna ambacho wametekeleza katika ilani yao wamegeuka mashetani hawa.
  b). Watakwambia kuwa: Vipaumbele katika mchakato wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni kufanya mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Kilimo ndicho msingi wa uchumi, kwa hivyo, mapinduzi ya kilimo (pamoja na ufugaji na uvuvi) yanategemea hali halisi ya kila nchi.
  Lakini ukiangalia wameanzisha KILIMO Kwanza ili kuigeuza EPA nyingine baada ya ile ya BoT kushtukiwa hawana lengo la kukipa kipaumbele kilimo. Bado wanacheza kama mashetani lakini nyimbo zao za mageuzi ya kilimo ni tamu kama zile za Malaika.
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  [FONT=AHIFDO+Tahoma]ILANI YA CCM YA 2005-2010 INASEMA:[/FONT]
  [FONT=AHIFDO+Tahoma]Barabara [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]44. Kipindi cha Awamu ya Tatu kimeshuhudia ujenzi na uboreshaji mkubwa wa barabara nchini. Katika kipindi cha miaka mitano cha 2005-2010, Serikali chini ya uongozi wa CCM zitatekeleza yafuatayo:- [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](a) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Barabara (Tanzania Road Fund). [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](b) Kukamilisha ukarabati wa barabara zote ambao unaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami ambao umekwishaanza katika barabara kuu. [/FONT]

  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Barabara hizo ni Dodoma-Manyoni, Manyoni-Singida, Singida-Shelui, Shelui-Igunga, Igunga-Nzega-Ilula; Muhutwe-Kagoma; Nangurukuru-Mbwemkulu-Mingoyo; Mkuranga-Kibiti; Pugu-Kisarawe; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Chalinze-Morogoro-Melela; Tunduma-Songwe; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Kiabakari-Butiama; Dodoma-Morogoro; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Kagoma-Biharamulo-Lusahunga; Tabora-Kaliua-Malagarasi- iUvinza- Kigoma; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Usagara-Chato-Biharamulo na Ndundu-Somanga. [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](c) Kuendelea kuimarisha barabara nchini zitakazounganisha nchi yetu na nchi jirani kwa barabara za lami; zitakazounganisha Makao Makuu ya Mikoa yote pia kwa barabara za lami na kuunganisha Makao Makuu ya Wilaya zote kwa barabara zinazopitika wakati wote; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](d) Kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara zifuatazo:- [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Tunduma-Sumbawanga;Marangu-Tarakea-Rongai; Minjingu-Babati-Singida; Rujewa-Madibira-Mafinga; Mbeya-Chunya-Makongolosi; Msimba-Ikokoto-Mafinga; Arusha-Namanga; Tanga-Horohoro; na ukarabati wa Barabara ya Kilwa (DSM), Barabara ya Mandela (DSM) na Barabara ya Sam Nujoma (DSM). [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](e) Kuzifanyia upembuzi yakinifu na usanifu barabara zifuatazo kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami: Maganzo-Maswa-Bariadi-Mkula-Lamadi; Babati-Dodoma-Iringa; Sumbawanga-Kigoma-Nyakanazi; Musoma-Fort-Ikoma; Korogwe-Handeni-Kilosa-Mikumi; Nzega-Tabora-Sikonge-Chunya; Mtwara-Masasi-Songea-Mbamba Bay; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Manyoni-Itigi-Tabora; Ipole-Mpanda-Kigoma na Bagamoyo-Saadani. [/FONT]

  [FONT=AHIFFO+Tahoma](f) Kuhimiza maandalizi na ujenzi wa Daraja la Kigamboni chini ya uongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuunganisha Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](g) Kuhakikisha upatikanaji wa kivuko kipya cha Kigongo-Busisi (Mwanza); [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](h) Kukamilisha ujenzi wa daraja jipya la Mpiji ambalo litawezesha njia mbadala ya Dar es Salaam-Tanga. [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](i) Kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na ujenzi wa daraja la Mto Kilombero na kukamilisha ujenzi wa daraja la Mto Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro. [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](j) Kufanya usanifu wa daraja jipya la Ruvu; [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](k) Kuendelea kuandaa mazingira mazuri ya kuishirikisha sekta binafsi katika ujenzi na matengenezo ya barabara kwa kutumia mfumo wa Jenga, Endesha na Kabidhi (BOT). [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](l) Kuanza ujenzi wa Daraja la Umoja (Tanzania na Msumbiji). [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](m) Kuanzishwa Programu ya Taifa ya Usafiri Vijijini[/FONT]

  [FONT=AHIFFO+Tahoma]JE NI YAPI YAMEFANYIKA KWA MAFANIKIO? MLIOKO KATIKA MAENEO HUSIKA MTUJUZE.[/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Ninayoyafahamu kuwa bado, ni haya yafuatayo[/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Kagoma-Biharamulo-Lusahunga, [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]Dodoma-Manyoni, Manyoni-Singida,[/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](c) Kuendelea kuimarisha barabara nchini zitakazounganisha nchi yetu na nchi jirani kwa barabara za lami; zitakazounganisha Makao Makuu ya Mikoa yote pia kwa barabara za lami [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma](m) Kuanzishwa Programu ya Taifa ya Usafiri Vijijini [/FONT]
  [FONT=AHIFFO+Tahoma]nk..[/FONT]
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tukiendelea kuwa na watanzania wenye akili kama zako hakika hatutapiga hatua kamwe.
  Mungu tuepushie watu kama huyu! Wanaodhani watanzania wote leo ni wajinga.
  Please ukikuta watu wanazungumza mambo ya maana tafadhali kaa kimya kwani hatuhitaji nyimbo zile zile.
  Nimemfurahia mwana jf mmoja aliyesema kuwa mnaimba nyimbo kama malaika lakini mnaozichezakumbe ni mashetani! Bwahahahahahahahahahaha!!!!!!:D
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ilani ya CCM ni LAANA kwa Watanzania

  Alishasema Mkapa kwamba hazitekelezeki, sijui mnasubiri nani aje kuwaambia tena kwamba msiichague cm maana kinara wao alisharudisha manyanga kwamba ngoma ni ngumu lakini nyie bado mnacheza MAHEPE!

  Ujinga umefungamana na akili za MTOTO naamini mtu mzima yeyote hana akili za kitoto
   
Loading...