Sijaona baya ambalo mtoa mada kaongea, kwakuwa yeye hajawazuia wanawake kuwa selective. Nashangaa mpaka wengine wanashuka na logical structure ya kumcriticise
. Kuna vitu vingi ulimwenguni mpaka sasaivi bado walimwengu wanavishangaa kuhusu jinsia ya kike ukihusisha logic bila kuweka bias, ila bado watu wanamkandia. Mind you hivi vitu vinatokea kweli na madhara yake yamezidi kuongezeka ila watu watashupaza shingo
. Ni kama vile mwanaume akishauriwa kuwa don't go for those ladies si wakiwango chako na akashupaza shingo ila in 3 months atarudi kafilisika kila kitu kwakuhudumia asivyoviweza na akirudi atachekwa hasa
, sasa shida wadada wakitaka kuambiwa wanaona wanasimangwa na jamii inawaficha. Matokeo yake watoto wasio na baba kibao na wadada kulizwa kila siku huku wakichukia wanaume. Ila jamii bado inashindwa kuwaambia ukweli
. Mtu kashangaa tu ila watu kuja kumsimanga hao. Ila angekuwa mwanaume yangeshushwa makavu humu balaa. Tuwape dada zetu na watoto wetu wakike ukweli maana uhuru wa kuchagua umepewa ila usipochagua kwa akili, hakika hamna mtu atakayelia na wewe kamwe.
Kushangaa si tatizo, ila wanaume wengine tumezidi mansplaining.
Yani tunataka kuwapangia wanawake cha kufanya, tunataka kuwaeleza, kuwafundisha, hata pale ambapo hawataki kuambiwa wala kufundishwa.
Kama ulivyofanya wewe hapo.
Kwenye haya mambo kila mtu ana haki ya kufanya anachotaka, hata kama wewe unaona ni kibaya kwake.
Kwa sababu uchaguzi ni wake.
Wakati Tanganyika tunagombea uhuru, Mwalimu Nyerere alikwenda kwenye kipindi kimoja cha TV New York, "Prospects of Mankind" cha Eleanor Roosevelt, aliyekuwa First Lady wa US.
Katika kipindi kile, Nyerere aliulizwa swali.
Tanganyika mnataka uhuru, je, mko tayari kujitawala?
Nyerere alijibu kwa falsafa kubwa, akasema nchi ni yetu, mmetukuta na uhuru wetu, mkauchukua, kama tunaweza au hatuwezi kujitawala ni swali lisilo na maana hapa. Hili swali ni sawa na kumkuta mtu kavaa koti lake, inawezekana halimtoshi vizuri, labda linambana, lakini koti ni lake. Hutakiwi kusema "Wewe, nipe hilo koti liwe langu kwa sababu linakubana". Mwache mwenyewe aamue afanye nini na koti lake.
Sasa, wanawake nao ni kama huyo mtu mwenye koti. Maadam uamuzi ni wao, tusiwazonge kwa hoja nyiingi za kimepanda kimeshuka, jamii bora itakuwa hivi na vile, hoja ambazo ukiziangalia sana ni za mfumodume tu, wanaume wanataka kuwapangia maisha wanawake.
Waacheni wanawake waamue wanavyotaka bila unyanyapaa wala mansplaining.
Na kama kuna kuelekezana na ufafanuzi, tuwasikie wanawake wenyewe wakieleza mambo na kufafanua.
Kwa sababu, ni hatari kwa mwanamme kutoa majibu ambayo anatakiwa kutoa mwanamke.
Wewe jitu dume, utajuaje mchakato wa mwanamke kuchagua mwanamme unaendaje ndani kabisa ya akili ya mwanamke?