Ila Wanawake hili huwa linawaumizaga sana huwa mnajikaza tu

IMG_5257.jpg
 
basi ni kuumia kwa zamu

maana hata mtongozaji ukikataliwa inauma sana, tena wewe unaumia kuliko hata yeye.
Kuna utongozaji wa kisayansi wa kuchomekea kutesti zali.

Akikumwaga unaendelea na hamsini zako kwa kujibaraguza kuwa ule ulikuwa ni utani tu wa kawaida.

Ila mzee ukiingia mzima mzima eti "dada nakupenda", waeza usiyaamini masikio yako kwa nyodo utazonyewa.

Kuna wanawake wapo standby kudhalilisha watongozaji, nadhani huwa wanafanya mazoezi kabisa ya kutukana!
 
Ukiona mwanamke hakutaki kuanzia mwanzo ujue ameshakuona wewe huna lolote wala hutakuja kuwa na lolote.

Wanawake wana nusa bwana yani anaweza kukuona leo kapuku lkn anajua kbs akikupa miaka mitatu umekaa sawa na mambo yako yamenyooka.

Binafsi nina experience na watu wawili watatu walotoka mbali na waume zao wana shuhuda kbsa kwamba walijua watatoboa mzee
 
Hiyo ilinitokea back 2015.

Kuna manzi tulianza kudate, sema kwakua mimi najitafuta hamna ahadi ata moja namtimizia. Nakumbuka iPhone 6 ndio zipo...
Bora wewe umeongea ukweli.

Kuna muda wanaume tunapoona mambo hayaendi na mahusiano uliyonayo huyatendei haki, yaani humtimizii haja zake mpenzi wako, ni bora umuache kuliko kumtesa, hasa ukiwa na hawa wanawake wenye tamaa na wasio na uvumilivu, ukiona mwanamke wako kapunguza kukuvumilia na ahadi zako za uongo zisizo timia chakufanya na kwa faida yenu wote TEMANA NAE, yaani muache akatafute mtu sahihi wa kuwa nae na kumtimizia ndoto zake, ikiwepo kumuoa na kumuinua kimaisha.

Hii tabia ya kuwang'ang'ania wanawake kwamba wakuvumilie na wasikuache huu ni upumbavu, ukiona mambo hayaendi na mtoto wa watu nikama unampotezea muda na kumchakaza kwa ahadi feki, bora umpe nafasi ya kufanya uchaguzi wake na uhuru wa kwenda akutakako.

Mpe nafasi aende na hakikisha unapompa uhuru nae akakubali basi huyo si wako tena, hivyo basi tafuta pesa kwa nguvu na hasira, ukizipata usirudiane nae, hata kama ulimpenda vipi akitaka mrudiane kataa ikiwezekana mdhalilishe kwa aibu na ajione alikuwa mpumbavu asie na subira&uvumilivu, muoneshe mafanikio yako ili ajue kuwa Ilikuwa suala la muda tu wewe kupika nyakati ngumu.

Kataa kudharauliwa, kataa kuonewa, kataa kuchunwa, kataa kuwa msindikizaji wa ndoto za watu, kataa wanawake malaya na wasio na misimamo.

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke wa kichaga akupende alafu uje ushike mkwanja uoe mwanamke mwingine umuache?
Unachekesha mkuu
Kwamba lazima akuchomoe uhai 😅

Ndiyo muwe nao makini, mapema umwambie hapa tunadate kupunguzana upwiru tu na sio zaidi 😜
 
Back
Top Bottom