Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Luca Paguro

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
476
Reaction score
1,060
Hivi ni mimi peke yangu naliona hili?
Mbona nchi yetu masikini jamani. Mimi nimezaliwa Ruangwa huku Lindi mara nyingi nimeona watu wakipakandia Lindi kwa umasikini hususani mitandaoni, mimi nikadhani ni huku tu hali ni mbaya, mpaka nilivyopata exposure. Maeneo mengi nilizunguka zamani utotoni nikawa sipakumbuki ila miaka ya karibuni nimezunguka sana. So nilikuwa na observe, nione kwa nini watu wanasema Lindi masikini, huenda mikoa mingine ni tajiri

Advance nimesoma Mbeya, nikawa napita njia ya Ruangwa-Masasi-Songea-Mbeya
Kuanzia hapa Ruangwa ukiwa unaenda Songea, hapa kati watu wanaishi maporini kwenye nyumba za matope, nyingine wameezeka nyasi, mabati yana kutu maeneo mengine unaona kabisa hata huduma za msingi hawazipati. Yani kitu kizuri kuangalia ni nature tu, mazingira ya asili kweli Tanzania imebarikiwa

Ukifika Songea sasa, vijiji vyake udongo mwekundu halafu nyumba mbaya yani ukipaangalia kama Uganda. Bora Songea mjini pale kumeendelea halafu nyumba sio mbaya sana. Issue ipo kutoka Ruvuma kwenda Mbeya sasa, vijiji vyote humu kati vimejaa umasikini (bora hata Makambako niliona pana nyumba nzuri) ila nilipofika Mbeya nilibaki mdomo wazi, nikawa najiuliza hili ni jiji? Khaaa
Yani nyumba za matope zimetapakaa milimani kote mji umechafuka kila kona nikiangalia naona umasikini tu.

Sikuipenda hii njia, nikaanza kutumia route ya Dar, natoka home naenda Dar nakaa siku 2 au 3 hivi halafu ndo naenda Mbeya. Dar nilikuwa nafikia Kimara kwa bro, ana nyumba nzuri na mtaa wao mzuri ila umepoa sana. Nikawa natoka asubuhi naenda kuzurura maeneo mengine ya Dar. Aisee kumbe nako ni umasikini tu umejaa. Ila Dar bora kuna miundombinu ambayo inapendeza lakini kuna mitaa nilipita ina nyumba zina kutu, nyumba zimebanana yani hovyohovyo. Nikawa najiuliza ina maana ni mimi tu ndo naona hii nchi haiko sawa? Kutoka Dar hadi Mbeya nako nilisafiri mchana ili nione mazingira nako hivyohivyo tu ni umasikini, sikupenda hata nikawa nasafiri route za usiku

Mwezi May mwaka huu tulisafiri kwenda Kigoma. Jamani hii njia ndo niliona umasikini funga kazi, bora Lindi kwa kweli 🙌
Kuna vijiji vipo Morogoro huku mmh, utafikiri bado wanatawaliwa na mfalme. Tena bora Morogoro, Dodoma kuna vijiji niliona vijiji nyumba watu wamejenga na matofali ya kuchoma halafu juu wameegesha tu bati halafu juu ya bati wameweka matofali ili bati lisiezuliwe na upepo. Aisee, nilishangaa sana, Tabora kuna vijiji tumepita nikaona nyumba zimejengwa style kama nyumba za Kiafrika za nyasi ila tu zenyewe zimejengwa na bati kuanzia juu mpaka chini, zipo nyingi halafu zimekaa kama kambi za wakimbizi. Uzuri nilisafiri na treni, niliona kila kitu vizuri. Kutoka Dar to Kigoma kuna li ardhi likubwa tu limeachwa hamna hata mashamba, wala nini yani nchi kubwa ila hatujui kutumia ukubwa wetu. Nimefika Kigoma nako umasikini wa kutisha

Hata form 4 tulienda study tour Zanzibar, nako ni overrated. Ukitoa pale Stone Town, kuna maeneo ni mabaya. Mji umechoka mbaya, mabati yana kutu. Kuna sehemu Zenji ya masista inaitwa Machui ndo tulipata hostel za kulala sisi wanafunzi, yani hata internet shida, kubaya af ni dakika 30 tu kutoka Stone town. Pako kama Nachingwea. Network inasumbua, migomba mingi kama Bukoba yani pabaya tu.
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma

Hadi nimerudi mkoani kwetu Lindi, huku nako ni kubaya. Nyumba mbaya. Yani naona nchi yetu masikini tu kuanzia bara hadi visiwani

Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.

Lakini naona vita dhidi ya umasikini tumeishindwa kabisa. Nchi kubwa, resources nyingi ila inasikitisha. Tushukuru Mungu Bongo wananchi wake wavumilivu, wengi wanaonekana kuwa na furaha tu
 
Kwa hiyo mkuu unashauri tufanye nini
Tuache ufisadi na tuanze kutumia pesa zetu vizuri kusolve umasikini. Wananchi wapewe nafasi kubwa sana kuexpress shida zao na maoni yao
Viongozi tunaowapa nafasi wawe smart, wakiwa bungeni waweze kuunganisha akili zao kufikiria mustakabali wa taifa hili na jinsi ya kupunguza umasikini kwa kasi badala ya kufikiria kujitajirisha wao kwa maslahi yao wenyewe
Na tupunguze vikwazo vya uwekezaji mfano matozo yasiyo na maana ili kuattract wawekezaji kutoka nje ya nchi. Tuache kuishi kana kwamba umasikini sio tatizo Tanzania. Wengi wetu tumelipuuzia hili tatizo
Tufix system kwanza
 
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma
Kuhusu Zanzibar huwa najiuliza Wazungu wanakuja kutafuta nini huku.

Zaidi ya Beach ambayo ni natural hakuna kitu kingine kinachovutia
 
Tembelea na kilimanjaro,ila morogoro ni uvivu wa wakazi , wakuja wametoboa kirahisi sana pale moro
Kilimanjaro natamani nifike siku moja, kama chuo ningeenda ATC ingekuwa easy kwenda Kilimanjaro. Ila nina mpango wa kwenda mikoa yote ambayo sijakanyaga
Morogoro pale mjini tulipokatisha niliona pako poa tu kwa standard za Bongo, ila shida sanasana ni vijijini ambako ndio most of time unapaona ukiwa unasafiri
 
Kilimanjaro natamani nifike siku moja, kama chuo ningeenda ATC ingekuwa easy kwenda Kilimanjaro. Ila nina mpango wa kwenda mikoa yote ambayo sijakanyaga
Morogoro pale mjini tulipokatisha niliona pako poa tu kwa standard za Bongo, ila shida sanasana ni vijijini ambako ndio most of time unapaona ukiwa unasafiri
Wilaya za moro , kwanzia mvomero , kilosa, ifakara , zote hizo zina fursa za mtu kutoka kimaisha ni uvivu tu wa wakazi wa huko .
 
Kuhusu Zanzibar huwa najiuliza Wazungu wanakuja kutafuta nini huku.

Zaidi ya Beach ambayo ni natural hakuna kitu kingine kinachovutia
Hata mimi nashangaa, ila eventually wanaishia kupapenda. Labda kwa sababu wanafikia beach na hotels za kifahari, na wengine wanapenda kujua slave trade ndio wanaenjoy hivyo
Ila kwa wakazi wengi wa pale, Zanzibar ni sehemu tofauti kabisa
 
Kuna gepu kubwa sana kati ya tajiri na masikini Tanzania. Kubwa sana.
Tanzania matajiri wa kweli WACHACHE sana, wengi wapigaji tu na 10% za udalali wa kila kitu, pamoja na Rushwa. Na ndo maana huwezi kuona impact sana ya hao wanaojiita so matajiri.Hauoni kila mtu anakimbilia kwenye siasa, awe mbunge, sasa hivi hadi Udiwani watu wanataka kutoana macho -ni ujanja ujanja.
Middle class hapo imejaa mikopo na madeni sio mchezo....
Hii bongo watu wamechoka sana, na usishtushwe na magari sijui nyumba, hivyo vinaficha umaskini na hofu ya maisha kwa walio wengi.
 
Back
Top Bottom