Ila bongo Movie bana, eti mfungwa anavaa hereni!

Sinema zetu hakika niza kwetu 😂🤣
F4CKFXeWwAAsJKo.jpeg
 
Wasanii wetu ni wavivu wa kusoma. Wenzetu kama msanii amepata kazi ya lawyer anakaa anajifunza jinsi lawyers wanavyokua. Directors nao wanahitaji shule maana wao ndio wanachangia vituko vya movie big times.
 
Kuna movie ya kibongo niliionaga kitambo kile, eti mtu kafa wamemueka kwenye Buti la gari (wanaenda kutafuta chimbo wamfukie). walivyofika wakafungua buti, cha kushangaza wakati wanamtoa marehemu kwenye buti, marehemu anawasaidia kushika mlango wa Buti usimbane (huku amekufa)
 
Si afadhali scene hiyo, nilichoka nilipo ona jini limenyunda kwa mguu toka ubungo kwenda mwenge, lilipofika Kivulini likachoka likaamua liombe lifti kwenye bajaji
Hujawahi kuona majambazi yanavamia nyumbani kwa tajiri afu yanavua viatu mlangoni?

Au hujawahi kuona jini linamfukuza mtu afu linazidiwa mbio linaamua kukodi bodaboda?
 
Katika mavitu yamenipita kushoto ni bongo movie. Yaani hawa ni vituko tu. Hata kuiga tu wameshindwa.

Hapo ujue mwisho wa hiyo movie huyo mfungwa lazima atakuwa tajiri. Halafu lazima ndio mtunzi huyo huyo,na ni director huyo huyo,na editer mwenyewe na staring mwenyewe. Na movie ametunga wiki hii mwezi ujao iko hewani.

Wakajifunze Nigeria,wale jamaa wako serious sana na kazi zao. Hawa kujishow tu ndio kazi yao. Sasa mfungwa hawataki kumuondolea uhalisia,wanamuacha na heleni na nywele zake na ndevu. Bongo movie ni vituko.
Na siku hizi baada ya kuona wamechemsha kwenye movie za maisha halisia yanayoonekana,wamegeukia movie za uchawi tu ksbb vitu vya kwenye uchawi sio halisia ni vya kubuni tu atakavyo,na kudanganya sana. Wanawapata tu wanawake na watoto,lakini hawawezi kuwapata wenye uelewa.
Nigeria nao wamezidi na mauchawi yao. Nimeacha kuangalia sinema zao tangu 2010.
 
Nigeria nao wamezidi na mauchawi yao. Nimeacha kuangalia sinema zao tangu 2010.
Labda kipindi hiki. Hata hivyo ukiangalia za uchawi za kwao ni kiasili kabisa,zinavutia kuliko za hawa bongo.
Hata hivyo tumeburudika sana na movie za Kinigeria kipindi cha akina Ramsey,Pastor Ken n.k. Unaangalia movie za Nigeria una-enjoy
Movie kama TRUE LOVE,ITMAITE STRANGE, PASTOR KEN,TO BE LOVED, n.k. Mtu anaigiza kijijini ni kijijini kweli. Anaigiza kuimba wimbo wa kuhuzunisha unakuhuzunisha kweli. Mtu anapigwa mpaka unaona amevimba kabisa
 
Bora nikatazama tomy and Jerry kuliko hizo sijui bongo movie.
Halafu kuna mtu anakwambia tupende vya nyumbani ni uzalendo!!
Wakitaka tuwe wazalendo, na wenyewe wakubali kwenda darasani kujifunza namna nzuri ya kutengeneza muvi za viwango vya Kimataifa.
 
Asee kilichonishangaza nikuona et mfungwa kwanza kavaa hereni pia kaachia ndevu na nywele . Sasa unajiuliza inamaana awa watu hawafanyi tafiti kwanza jinsi mambo yalivyo. We tangu lini mfungwa akavaa heleni
Halafu mfungwa mwenyewe ndozi nyeupe

Hiyo vaa yake ya heleni nashauri akakaguliwe diameter tena chini ya bunduki kuhakiki kama yuko vile anavyotakiwa kuwa
 
mimi sio mtabili,...lakini naweza ona kesho ya mtu anaeahusudu bongo movies na movies zilizotafsiriwa😂🤣🤣🙏🏃
 
Una uhakika hata wenzako wanaoangalia hizo bongo movie wanajiuliza maswali kama haya yako?.
Asee salam

Jana kuna filamu (bongo Movie) nilikua naangalia sasa kuna scene moja ya gerezani

Asee kilichonishangaza nikuona et mfungwa kwanza kavaa hereni pia kaachia ndevu na nywele . Sasa unajiuliza inamaana awa watu hawafanyi tafiti kwanza jinsi mambo yalivyo. We tangu lini mfungwa akavaa heleni

Nyingine niliona et mkuu wa kituo cha polisi ni koplo afu anampa maagizo inspector wa polisi asee

Nilichoona hawa watu ninawavivu ata kujua taratibu za mambo mbali mbali yanavyoenda. Emu ona picha mwenyewe

View attachment 2764715

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mada kama hizo ukiwakosoa Hawa vilaza wetu wa ccm wasanii wanadai wivu.
huwa sipotezi muda kubishana na watu hao ni hatari kwa afya yangu...nikiona tu mtu wa namna hiyo sihitaji kipimo kujua majibu atakayonipa kwa kila swali nitakalomuuliza.....waigizaji na watafsiri wa movies hapa bongo ni kiwakilishi tosha cha IQ ya watanzania wengi........nimewahi ongea na actor mmoja juu ya hili jambo kwa kina, nilichokuja gundua ni njaa, ulimbukeni wa usupastar, na marupurupu ya ngono wakiwa camps...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom