Ila bongo Movie bana, eti mfungwa anavaa hereni!

Gaitonde

Member
Sep 5, 2022
70
170
Asee salam

Jana kuna filamu (bongo Movie) nilikua naangalia sasa kuna scene moja ya gerezani

Asee kilichonishangaza nikuona et mfungwa kwanza kavaa hereni pia kaachia ndevu na nywele . Sasa unajiuliza inamaana awa watu hawafanyi tafiti kwanza jinsi mambo yalivyo. We tangu lini mfungwa akavaa heleni

Nyingine niliona et mkuu wa kituo cha polisi ni koplo afu anampa maagizo inspector wa polisi asee

Nilichoona hawa watu ninawavivu ata kujua taratibu za mambo mbali mbali yanavyoenda. Emu ona picha mwenyewe

Screenshot_20230928-083710.jpg
 
Katika mavitu yamenipita kushoto ni bongo movie. Yaani hawa ni vituko tu. Hata kuiga tu wameshindwa.

Hapo ujue mwisho wa hiyo movie huyo mfungwa lazima atakuwa tajiri. Halafu lazima ndio mtunzi huyo huyo,na ni director huyo huyo,na editer mwenyewe na staring mwenyewe. Na movie ametunga wiki hii mwezi ujao iko hewani.

Wakajifunze Nigeria,wale jamaa wako serious sana na kazi zao. Hawa kujishow tu ndio kazi yao. Sasa mfungwa hawataki kumuondolea uhalisia,wanamuacha na heleni na nywele zake na ndevu. Bongo movie ni vituko.
Na siku hizi baada ya kuona wamechemsha kwenye movie za maisha halisia yanayoonekana,wamegeukia movie za uchawi tu ksbb vitu vya kwenye uchawi sio halisia ni vya kubuni tu atakavyo,na kudanganya sana. Wanawapata tu wanawake na watoto,lakini hawawezi kuwapata wenye uelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom