Ikulu yanuka ukabila?

Ikulu yanuka ukabila?

Na Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete sasa anatikiswa kwa tuhuma kwamba ikulu imekumbwa na ukabila, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa zinasema tuhuma hizo tayari ziko mezani kwake na zinamhusu mtendaji mkuu wa ikulu.

Anayetajwa kuhusika na ukabila ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ambaye inadaiwa analinda watu wa mkoa anakotoka – Iringa.

Lakini Luhanjo alipopigiwa simu kutaka kauli yake alijibu kwa sauti ya ukali, "Kwani kama wewe ni mwandishi wa MwanaHALISI ndiyo unipigie simu saa hizi?"

Hiyo ilikuwa Jumamosi saa mbili usiku.

Alipoelezwa kwamba gazeti liko tayari kukutana naye wiki hii wakati wowote atakapokuwa tayari, Luhanjo alijibu, "I will not talk with you for anything (Sitazungumza lolote na wewe)." Alikata simu.

Hata hivyo chanzo cha taarifa hizi kinasema, "Luhanjo amejiimarisha kweli na anaweka watu wake kila eneo na wanataka kujenga himaya yao."

Luhanjo anahusishwa na upendeleo wa ukabila katika hatua ya serikali kuipa zabuni kampuni ya Peacock Hotels Limited kuendesha mradi wa hoteli katika jengo la Millennium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Inadaiwa Luhanjo ana mkono katika kubeba Peacock Hotels ambayo mmiliki na mkurugenzi mtendaji wake, Joseph Mfugale pia anatoka Iringa.

Lakini Mfugale anakana kubebwa, akisema "Tulishindana tukashinda na kulipa dhamana, tena milioni nyingi – dola 165,000 (Sh. 171 milioni)."

Alisema tatizo la fedha za dhamana walizotoa ni kwamba kulitokea mpango wa kuziiba ili tenda apewe mtu mwingine.

"Waliposhindwa mpango wao, mkurugenzi wa raslimali aliamua kujiuzulu na sasa nasikia amepata kazi mahali pengine," alidai Mfugale.

Mfugale anasema fedha za dhamana zililipwa kupitia benki ya CRDB, tawi la Kijitonyama.

Millennium Tower inamilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mbali na Luhanjo, mwingine anayedaiwa kumbeba Mfugale ni Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Maimuna Tarishi ambaye pia anatoka Iringa.

Tarishi ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya LAPF. Inadaiwa Mfugale aliwasilisha malalamiko kwa watendaji wa juu wa serikali kwa kile alichodai, "kuhujumiwa katika zabuni."

Tarishi hakupatikana kutoa maoni yake juu ya madai hayo. Katibu muhtasi wake aliyeko Dodoma alijibu kuwa Tarishi yuko Dar es Salaam na kwamba "simu yake ya mkononi aliisahau Dodoma."

Awali nyaraka za zabuni za Mfugale ziliwekwa kando kwa madai ya kukosekana dhamana ya benki, jambo ambalo alilalamikia.

Imedaiwa kuwa baada ya Mfugale kulalamika, Luhanjo aliagiza uongozi wa TAMISEMI kufuatilia malalamiko hayo.

Katika malalamiko yake, Mfugale anatuhumu Julius Mfukwe, ambaye alikuwa mkurugenzi wa vitegauchumi wa LAPF, kuchomoa nyaraka zake za dhamana za benki ili kubeba mmiliki wa Hotel ya Paradise.

Tayari Mfukwe ameacha kazi katika mfuko huo na sasa ameajiriwa na Mamlaka ya Bandari nchini (THA).

Alipoulizwa juu ya madai hayo ya Mfugale, Mfukwe alijibu kwa sauti ya upole, "Hii namba yangu umeipata wapi?"

Alipoambiwa kuwa yeye ni mtu mkubwa anayefahamika, alijibu, "Kaka, nakushukuru lakini sina la kusema."

Alisema, "Mimi sipo huko tena. Siwezi kuongea chochote kinachohusu LAPF kwa kuwa si msemaji wao. Nakuomba uwatafute viongozi wa mfuko ndio watakueleza."

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa kutoka serikalini, wakati wa ufunguaji zabuni ya kuendesha hoteli katika jengo hilo la Millennium Tower, Mfugale hakuwa ametimiza sharti la kuweka dhamana ya benki kama ambavyo tangazo la zabuni liliagiza.

"Zabuni ilifunguliwa hadharani na kuhudhuriwa na kila muombaji. Huyu bwana hakuwa ameweka bond kwenye zabuni yake. Baada ya kuona kwamba amepoteza sifa, akaanza kutafuta msaada," kimeeleza chanzo cha taarifa.

Kabla ya kukodishwa kwa Mfugale, hoteli ilikuwa inaendeshwa na kampuni ya African Sky kutoka Afrika Kusini. Kampuni inadaiwa iliondoka na deni la dola 400 milioni.

Kwa utuki tu, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF ni Eliud Sanga na Meneja Mkuu ni Injinia G. Matovola wote kutoka Iringa.

Kwa muda mrefu mkoa wa Iringa umetoa viongozi katika ofisi ya rais. Kwa mfano, Emilius Mzena, Augustine Mahiga na Hans Kitine wote kutoka Iringa, walikuwa wakurugenzi wa usalama wa taifa.

Aidha, Kitine na Peter Siyovelwa wamewahi kuwa mawaziri ofisi ya rais wanaoshughulikia usalama wa taifa.

Wengine ambao wanatoka Iringa na wako ofisi ya rais; na huenda kwa utuki tu ni Rajab Luhavi na Lumbila Fyataga ambao ni wasaidizi.

Miongoni mwa watu mashuhuri kutoka Iringa ambao wamo katika nafasi za juu kimadaraka nchini ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la NIPASHE, Mchechu hakuwa miongoni mwa watu waliofanyiwa usaili kwa kuwa "hakuwa na sifa" ya kupewa kazi aliyoomba.

Mchakato wa kumpata mkurugenzi mkuu wa NHC, ulisimamiwa na kampuni ya Price Water House Cooppers na uligharimu serikali zaidi ya Sh. 82 milioni.

Hata hivyo, pamoja na kwamba Mchechu aliomba nafasi hiyo, hakuwa short listed (kuwa miongoni mwa waliopitishwa kwa kufanyiwa usaili).

"Kwa hiyo serikali imetumia mamilioni ya shilingi za umma kwa kazi ambayo haikuwa na tija, kwa kuwa aliyeajiriwa hakufanyiwa usaili," ameeleza mjumbe mmoja wa bodi iliyomaliza muda wake.

Amesema serikali imelipa kampuni ya ushauri ya Price Water "lakini kazi yote iliyofanyika imetupwa kapuni."

Taarifa za baadaye zimesema kuwa uongozi wa NHC tayari umeidhinisha Mchechu kulipwa mshahara wa dola za Marekani 11,000 (Sh. 14 milioni) kwa mwezi, jambo ambalo linatajwa kuwa linaweza kuangamiza hata shirika lenyewe.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mchechu ameacha malipo ya dola 16,000 kwa mwezi katika Benki ya Biashara Afrika (ABC) ambako alikuwa anafanyakazi.

Haikufahamika kwa nini ameamua kuacha kazi penye mshahara mkubwa kuliko ule atakaokuwa anapata NHC.

Source: Mwanahalisi, Issue No 181

Iringa ni kabila ama mkoa?Iringa kuna wahehe,wabena nk....Kwahiyo weka wazi kama ni upendeleo wa aina gani,kama wote waliopendelewa ni wahehe,ama wote ni wabena,then hilo linakuwa ni ukabila moja kwa moja.Kama waliopendelewa ni mchanganyiko wa makabila hayo,basi huo ni upendeleo based on mkoa wanaotoka na hapo si ukabila moja kwa moja.
 
Upuuzi mtupu! magazeti ya Bongo jamani tafran tupu. Sasa ikiwa hawa wafanyakazi Ikulu ni watu kutoka Iringa inahusiana vipi na Ukabila yaani mtu akitoka Iringa basi lazima awe ni kabila fulani linaloleta Ukabila!

Mkandara.. ndio maana wakati fulani nilihoji ukabila ni nini hasa? Kwenye mawazo ya watu wengi (kama inavyoonekana kwenye MwahaHalisi) ukabila ni Idadi! NI sawa kabisa na wale wanaoenda TRA na kukuta wachagga wakadai ni ukabila, wakaenda JWTZ na kukuta kuna wakurya wengi watasema ukabila na wakienda Mwanza, na kukuta wasukuma wengi kwenye ofisi mbalimbali wakasema ni ukabila, Ukabila ni vitendo vya kupendelea au kutoa fursa ya upendeleo kwa watu wa kabila lako huku ukipuuzia makabila mengine. Kwa mfano kwenye mada hiyo hatujui ratio ya watu wa mikoa mingine in relation to hao wa Iringa.

pointi umeitoa nzuri siyo wote wanaotoka Iringa ni Wahehe au Wabena..
 
Na Saed Kubenea
Taarifa za baadaye zimesema kuwa uongozi wa NHC tayari umeidhinisha Mchechu kulipwa mshahara wa dola za Marekani 11,000 (Sh. 14 milioni) kwa mwezi..................Mchechu ameacha malipo ya dola 16,000 kwa mwezi katika Benki ya Biashara Afrika (ABC) ambako alikuwa anafanyakazi..........
Possibly those figures in red were typed wrongly, siamini kama hakukuwa na typing error......ila kama ni kweli hasa ile ya Dolari 11,000 basi kweli Maisha Bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Sasa ndo naamini Mshauri Mkuu wa Ikulu (yupo Back office) LAZIMA atakuwa huyu hapa

sheikh-yahyabc.jpg
 
Hivi kama kweli NHC watamlipa $11000 kwa mwezi huyu mtu ,is this GOOD VALUE FOR MON
Kama ni private company hapa sawa,lakini kama NHC iko chini ya serikali ,this is really stupidity!
 
Mpaka karne hii jamani bado tunaongelea ukabila...tutafika? mbona kama tunarudi nyuma
 
Kama Ukabila upo usiongelewe? Mi nadhani the best way to abolish this stupidity ni kuwaweka hadharani wote wenye vitabia tabia kama hivi vya ukabila. Kama ambavyo tunafanya kwa majambazi, wala rushwa, wasambaza ukimwi kwa makusudi na wengineo. Unapoukalia kimya eti kwa kuhofia utaambiwa unarudi nyuma ni kutokujua wajibu wako.
 
Hivi kama kweli NHC watamlipa $11000 kwa mwezi huyu mtu ,is this GOOD VALUE FOR MON
Kama ni private company hapa sawa,lakini kama NHC iko chini ya serikali ,this is really stupidity!

It is not stupidity kumlipa hivyo kama kweli shirika lina tija. ILO ilifanya tahimini tanzania wafanyakazi inatakiwa walipwe at least laki 5 kama sikosei.

Tujiulize KCC hapo NHC wanalipwa shilinngi ngapi? na je kwa nini wasilipwe zinazowatsoha kwa level yao.Kuliko kulalamika Nehemia anapata mshahara mmkubwa tulamikie wa KCC wanaopata mdogo.
 
Kama hao watu wanasifa zinazofaa na wanachapa kazi vizuri tatizo lipo wapi?
 
Mkandara.. ndio maana wakati fulani nilihoji ukabila ni nini hasa? Kwenye mawazo ya watu wengi (kama inavyoonekana kwenye MwahaHalisi) ukabila ni Idadi! NI sawa kabisa na wale wanaoenda TRA na kukuta wachagga wakadai ni ukabila, wakaenda JWTZ na kukuta kuna wakurya wengi watasema ukabila na wakienda Mwanza, na kukuta wasukuma wengi kwenye ofisi mbalimbali wakasema ni ukabila, Ukabila ni vitendo vya kupendelea au kutoa fursa ya upendeleo kwa watu wa kabila lako huku ukipuuzia makabila mengine. Kwa mfano kwenye mada hiyo hatujui ratio ya watu wa mikoa mingine in relation to hao wa Iringa.

pointi umeitoa nzuri siyo wote wanaotoka Iringa ni Wahehe au Wabena..

Naomba niongezee hii Definition ya M. Mwanakijiji:
Ukabila ni vitendoi vya kupendelea au kutoa fursa ya upendeleo kwa watu wa kabila lako wasiokuwa na uwezo huku ukipuuzia watu wa makabila mengine wenye uwezo.

Nimeongeza maneno machache ili kuiimarisha zaidi maana ya ukabila. Mimi ukiniambia kuwa wasukuma au wamasai ndio wazuri katika kusimamia mradi fulani na taifa likapiga hatua, sitakuwa na shida hata kama shirika lote litakuwa na wasukuma au wamasai watupu.

Kwa miaka mingi Jeshi letu la wananchi limekuwa na watu wengi kutoka mkoa wa Mara na limeendelea kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Ukiniuliza mimi juu ya ukabila jeshini nitakuona una wendawazimu. kuna tatizo gani? Uwezo wanao na hakuna wengine wameonyesha uwezo wakaacha kupewa nafasi.

Ukabila wa siku hizi.
Ni mtandao, kila anayepata nafasi anataka aweke watu wake sehemu nyeti hata kama hawana uwezo. Matokeo ni nchi kwenda mrama kwenye kila idara. Matatizo yote tunayoyaona leo ni mtandao, hakuna ambaye yuko tayari kumkemea mwana mtandao mwenzake, kumfukuza mwanamtanadao mwenzake, kumkaripia mwanamtandao mwenzake, sasa tatizo liko mpaka kwenye vyombo muhimu kabisa katika uendeshaji wa nchi. UKABILA WA MTANDO NDIO UKABILA MBAYA KABISA KWA NCHI YETU KWA SASA. unauwa uwajibikaji na kuleta kujipendekeza.
 
hmanA CHOCHOTE HAPA ,Kubenea is just another gun for hire to the highest bidder,amelipwa amchafulie jina CEO wa NHC,huy jamaa ni mchapa kazi,na ataweza kufanikisha kazi,isitoshe ni kijana na ametoka private sector,its time for a change,
hawa consultant face eti price water na wengineo,ni matepeli wanatumia majina ya kampuni kubwa za ulaya,usahili gani wa milioni 82,huwa wanapewe tender na vigogo so ata maamuzi yao yanakuwa biased vilevile.
kwa kifupi tumpe muda tuone changes ktk national housing.

Atayepata kazi hiyo malipo ni usd131,000/year=Tsh170, 000,000/year. Hivyo basi Price water kulipwa million82 utaona ni fair kabisa kwa kulingana na hiyo hadhi ya watu wanaowasahili.
Hata hivyo nashangaa kwa nini mishara yetu ipo juu kiasi hicho na bado hilo ni shirika la umma.
 
hmanA CHOCHOTE HAPA ,Kubenea is just another gun for hire to the highest bidder,amelipwa amchafulie jina CEO wa NHC,huy jamaa ni mchapa kazi,na ataweza kufanikisha kazi,isitoshe ni kijana na ametoka private sector,its time for a change,
hawa consultant face eti price water na wengineo,ni matepeli wanatumia majina ya kampuni kubwa za ulaya,usahili gani wa milioni 82,huwa wanapewe tender na vigogo so ata maamuzi yao yanakuwa biased vilevile.
kwa kifupi tumpe muda tuone changes ktk national housing.

Naona huna points za kutetea hoja yako. Hata kama Kubenea ni muongo, hapo amepanga matukio kama inavyotakiwa na kamuweka wazi Luhanjo.

Muokoe kwa kutumia points. Usieme huyu mchapa kazi yule ni kijana na ... so what? procedure hazikufuatwa, period.

Luhanjo amecheza mara nyingi rafu za aina hii. faida kwake ni udhaifu wa serikali tu lakini kama si hivyo, he is no useful to this country. Mpeni ubunge maana nasikia anautafuta.
 
Na Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete sasa anatikiswa kwa tuhuma kwamba ikulu imekumbwa na ukabila, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa zinasema tuhuma hizo tayari ziko mezani kwake na zinamhusu mtendaji mkuu wa ikulu.

Anayetajwa kuhusika na ukabila ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ambaye inadaiwa analinda watu wa mkoa anakotoka – Iringa.

Lakini Luhanjo alipopigiwa simu kutaka kauli yake alijibu kwa sauti ya ukali, "Kwani kama wewe ni mwandishi wa MwanaHALISI ndiyo unipigie simu saa hizi?"

Hiyo ilikuwa Jumamosi saa mbili usiku.

Alipoelezwa kwamba gazeti liko tayari kukutana naye wiki hii wakati wowote atakapokuwa tayari, Luhanjo alijibu, "I will not talk with you for anything (Sitazungumza lolote na wewe)." Alikata simu.

Hata hivyo chanzo cha taarifa hizi kinasema, "Luhanjo amejiimarisha kweli na anaweka watu wake kila eneo na wanataka kujenga himaya yao."

Luhanjo anahusishwa na upendeleo wa ukabila katika hatua ya serikali kuipa zabuni kampuni ya Peacock Hotels Limited kuendesha mradi wa hoteli katika jengo la Millennium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Inadaiwa Luhanjo ana mkono katika kubeba Peacock Hotels ambayo mmiliki na mkurugenzi mtendaji wake, Joseph Mfugale pia anatoka Iringa.

Lakini Mfugale anakana kubebwa, akisema "Tulishindana tukashinda na kulipa dhamana, tena milioni nyingi – dola 165,000 (Sh. 171 milioni)."

Alisema tatizo la fedha za dhamana walizotoa ni kwamba kulitokea mpango wa kuziiba ili tenda apewe mtu mwingine.

"Waliposhindwa mpango wao, mkurugenzi wa raslimali aliamua kujiuzulu na sasa nasikia amepata kazi mahali pengine," alidai Mfugale.

Mfugale anasema fedha za dhamana zililipwa kupitia benki ya CRDB, tawi la Kijitonyama.

Millennium Tower inamilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mbali na Luhanjo, mwingine anayedaiwa kumbeba Mfugale ni Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Maimuna Tarishi ambaye pia anatoka Iringa.

Tarishi ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya LAPF. Inadaiwa Mfugale aliwasilisha malalamiko kwa watendaji wa juu wa serikali kwa kile alichodai, "kuhujumiwa katika zabuni."

Tarishi hakupatikana kutoa maoni yake juu ya madai hayo. Katibu muhtasi wake aliyeko Dodoma alijibu kuwa Tarishi yuko Dar es Salaam na kwamba "simu yake ya mkononi aliisahau Dodoma."

Awali nyaraka za zabuni za Mfugale ziliwekwa kando kwa madai ya kukosekana dhamana ya benki, jambo ambalo alilalamikia.

Imedaiwa kuwa baada ya Mfugale kulalamika, Luhanjo aliagiza uongozi wa TAMISEMI kufuatilia malalamiko hayo.

Katika malalamiko yake, Mfugale anatuhumu Julius Mfukwe, ambaye alikuwa mkurugenzi wa vitegauchumi wa LAPF, kuchomoa nyaraka zake za dhamana za benki ili kubeba mmiliki wa Hotel ya Paradise.

Tayari Mfukwe ameacha kazi katika mfuko huo na sasa ameajiriwa na Mamlaka ya Bandari nchini (THA).

Alipoulizwa juu ya madai hayo ya Mfugale, Mfukwe alijibu kwa sauti ya upole, "Hii namba yangu umeipata wapi?"

Alipoambiwa kuwa yeye ni mtu mkubwa anayefahamika, alijibu, "Kaka, nakushukuru lakini sina la kusema."

Alisema, "Mimi sipo huko tena. Siwezi kuongea chochote kinachohusu LAPF kwa kuwa si msemaji wao. Nakuomba uwatafute viongozi wa mfuko ndio watakueleza."

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa kutoka serikalini, wakati wa ufunguaji zabuni ya kuendesha hoteli katika jengo hilo la Millennium Tower, Mfugale hakuwa ametimiza sharti la kuweka dhamana ya benki kama ambavyo tangazo la zabuni liliagiza.

"Zabuni ilifunguliwa hadharani na kuhudhuriwa na kila muombaji. Huyu bwana hakuwa ameweka bond kwenye zabuni yake. Baada ya kuona kwamba amepoteza sifa, akaanza kutafuta msaada," kimeeleza chanzo cha taarifa.

Kabla ya kukodishwa kwa Mfugale, hoteli ilikuwa inaendeshwa na kampuni ya African Sky kutoka Afrika Kusini. Kampuni inadaiwa iliondoka na deni la dola 400 milioni.

Kwa utuki tu, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF ni Eliud Sanga na Meneja Mkuu ni Injinia G. Matovola wote kutoka Iringa.

Kwa muda mrefu mkoa wa Iringa umetoa viongozi katika ofisi ya rais. Kwa mfano, Emilius Mzena, Augustine Mahiga na Hans Kitine wote kutoka Iringa, walikuwa wakurugenzi wa usalama wa taifa.

Aidha, Kitine na Peter Siyovelwa wamewahi kuwa mawaziri ofisi ya rais wanaoshughulikia usalama wa taifa.

Wengine ambao wanatoka Iringa na wako ofisi ya rais; na huenda kwa utuki tu ni Rajab Luhavi na Lumbila Fyataga ambao ni wasaidizi.

Miongoni mwa watu mashuhuri kutoka Iringa ambao wamo katika nafasi za juu kimadaraka nchini ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la NIPASHE, Mchechu hakuwa miongoni mwa watu waliofanyiwa usaili kwa kuwa "hakuwa na sifa" ya kupewa kazi aliyoomba.

Mchakato wa kumpata mkurugenzi mkuu wa NHC, ulisimamiwa na kampuni ya Price Water House Cooppers na uligharimu serikali zaidi ya Sh. 82 milioni.

Hata hivyo, pamoja na kwamba Mchechu aliomba nafasi hiyo, hakuwa short listed (kuwa miongoni mwa waliopitishwa kwa kufanyiwa usaili).

"Kwa hiyo serikali imetumia mamilioni ya shilingi za umma kwa kazi ambayo haikuwa na tija, kwa kuwa aliyeajiriwa hakufanyiwa usaili," ameeleza mjumbe mmoja wa bodi iliyomaliza muda wake.

Amesema serikali imelipa kampuni ya ushauri ya Price Water "lakini kazi yote iliyofanyika imetupwa kapuni."

Taarifa za baadaye zimesema kuwa uongozi wa NHC tayari umeidhinisha Mchechu kulipwa mshahara wa dola za Marekani 11,000 (Sh. 14 milioni) kwa mwezi, jambo ambalo linatajwa kuwa linaweza kuangamiza hata shirika lenyewe.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mchechu ameacha malipo ya dola 16,000 kwa mwezi katika Benki ya Biashara Afrika (ABC) ambako alikuwa anafanyakazi.

Haikufahamika kwa nini ameamua kuacha kazi penye mshahara mkubwa kuliko ule atakaokuwa anapata NHC.

Source: Mwanahalisi, Issue No 181

1. Naunga mkono wanaosema Iringa sio kabila ni Mkoa Mkubwa tu na una makabila mengi, kuna Wahehe, Wazungwa, Wabena, Wawanji, Wakinga, nk nk nk.
2. ni ratio ipi ya ku justfy kuwa Ikulu imejaa watu wa Iringa? 80% impossible!

hili tatizo la kuongelea ukabila linaturudisha nyuma sana. linaleta maana kama mhusika hawezi kazi aliyopewa na kuwa aliingizwa kwa kubebwa. Ila kama mtu aliomba mwenyewe na ana vyeti? na anaiweza kazi inakuwaje anahusishwa na ukabila?? hivyo utafiti ufanyike na si mtu kuamka tu na kubwabwaja.

ukabila?? ukabila?? ukabila??
BADO TUNAONGELEA UKABILA MPAKA MIAKA HII YA LEO
wenzetu wanakimbia sie tunarudi nyuma
 
Sioni kosa kama watu wame qualify kufanya kazi hizo Ikulu.Tukumbuke pia kwa jinsi ilivyo TZ leo, kuna makundi mengi ambayo interest zao zinapoonekana kukwama wanatafuta jinsi ya kuwatengenezea wapinzani wao skandali.
What is important ni kuangalia kila habari katika dimensions zote, hata ikibidi three dimensions ili kuwa na uhakika kujua ukweli.
 
Na Saed Kubenea

“I will not talk with you for anything (Sitazungumza lolote na wewe).”
Source: Mwanahalisi, Issue No 181
tehetehe......!1!
hahahahaha........!!!
haaaaaaaaaaah!!!!
Mambo ya ung'eng'e wa KMK! Bora kiswahili kitumike kufundisha tu
 
Ikulu haijakanusha, bali imekuja na hoja za matusi. Kwa mfano, Ikulu inasema, " Isitoshe baadhi ya watu wanaotajwa katika habari hiyo kuwa walipata kuwa ama wako Ikulu kwa sasa kwa sababu ya kulindwa na Luhanjo, walikuwa Ikulu, wengine miaka mingi, kabla ya Luhanjo hajawa Katibu Mkuu Kiongozi mwishoni mwa mwaka 2005.

"Hawa ni pamoja na Lumbila Fyataga ambaye amekuwa Ikulu tangu Awamu ya Tatu, Rajabu Luhwavi, marehemu Emilius Mzena, Balozi Augustine Mahiga na Hassy Kitine, wote hawa walifanya kazi Ikulu, kabla ya Luhanjo kuwa Katibu Mkuu Kiongozi..."

Katika habari yote MwanaHALISI hawajasema kwamba hawa watu wameletwa na Luhanjo.
Gazeti limesema, "Kwa utuki tu, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF ni Eliud Sanga na Meneja Mkuu ni Injinia G. Matovola wote kutoka Iringa.

Kwa muda mrefu mkoa wa Iringa umetoa viongozi katika ofisi ya rais. Kwa mfano, Emilius Mzena, Augustine Mahiga na Hans Kitine wote kutoka Iringa, walikuwa wakurugenzi wa usalama wa taifa.

Wengine ambao wanatoka Iringa na wako ofisi ya rais; na huenda kwa utuki tu ni Rajab Luhavi na Lumbila Fyataga ambao ni wasaidizi. Aidha, Kitine na Peter Siyovelwa wamewahi kuwa mawaziri ofisi ya rais wanaoshughulikia usalama wa taifa.Kwa kauli hii, inaonyesha kuwa huyu Salva hajui hata maana ya neno Utuki. Tuhuma za Luhanjo hapa ni ni kuingilia zabuni na kumbeba Mfugale ambaye hakuwa na sifa. Ndiyo msingi wa stori ya MwanaHALISI.

Luhanjo ni mkabila na analundo la tuhuma. Salva hajajibu hoja badala yake ametaka kutetea mwabwana zake.
Jina lako wala haliendani na hoja ulizozijenga hapa natamani jina lako lingekuwa udaku badala ya kuwa facts. Ikulu imetukana tusi gani katika hizo rangi ulizoweka? Hao wote waliopo kwenye hizo nafasi umewaassess ukagundua hawana qualification? Umeangalia vyeti vyao ukaona kwamba hawakustahili kuwa huko. Tuache kuleta hoja zisizo na msingi bwana, hangaika na wewe tengeneza CV yako nzuri, ukaombe kazi Ikulu. Bila shaka utapata, siyo kujiingiza kwenye malumbano ya kidaku kama ya Kubenea.
 
Naona huna points za kutetea hoja yako. Hata kama Kubenea ni muongo, hapo amepanga matukio kama inavyotakiwa na kamuweka wazi Luhanjo.

Muokoe kwa kutumia points. Usieme huyu mchapa kazi yule ni kijana na ... so what? procedure hazikufuatwa, period.

Luhanjo amecheza mara nyingi rafu za aina hii. faida kwake ni udhaifu wa serikali tu lakini kama si hivyo, he is no useful to this country. Mpeni ubunge maana nasikia anautafuta.
Hivi ni hoja gani aliyoijenga Kubenea inayoonyesha kwamba Luhanjo ameshiriki kuweka watu Ikulu? Wewe umeisoma hiyo habari na kuielewa? Luhanjo ameshiriki kumfanikisha Mfugale apate tenda ya kuendesha hotel milenium tower sasa huko ni Ikulu? Ni wapi Kubenea amethibitisha kwamba kuna mfanyakazi wa Ikulu yupo pale kwa sababu ya Luhanjo? Au ni mahali gani panaposema Luhanjo ndo amemteua Mkurugenzi wa NHC. Huu ndo wehu tunaousema siku zote?? Wewe unajenga hoja kutokea wapi? Au unaangalia tu kichwa cha habari ambacho kinaonyesha kabisa kimeandikwa kisiasa na kwa fitina? Huyu Kubenea sasa hivi keshapoteza mwelekeo, anafaa sasa kuandika habari kwenye magazeti ya uwazi, ijumaa na risasi.
 
hmanA CHOCHOTE HAPA ,Kubenea is just another gun for hire to the highest bidder,amelipwa amchafulie jina CEO wa NHC,huy jamaa ni mchapa kazi,na ataweza kufanikisha kazi,isitoshe ni kijana na ametoka private sector,its time for a change,
hawa consultant face eti price water na wengineo,ni matepeli wanatumia majina ya kampuni kubwa za ulaya,usahili gani wa milioni 82,huwa wanapewe tender na vigogo so ata maamuzi yao yanakuwa biased vilevile.
kwa kifupi tumpe muda tuone changes ktk national housing.

Tunahitaji kweli mabadiliko lakini mabadiliko yasiyofata taratibu ni uhuni ambao hauwezi kuvumilika.Kabla ya kuanza kumtetea huyo CEO mpya wa NHC ni nzuri ungejua hao wengine waliopigwa chini wanauzoefu na elimu ya kiwango gani.Tusipende kutetea vitu kwa sababu vinahusu vijana!
 
Jina lako wala haliendani na hoja ulizozijenga hapa natamani jina lako lingekuwa udaku badala ya kuwa facts halafu hoja mbofumbofu tu. Ikulu imetukana tusi gani katika hizo alama ulizoweka? Hao wote waliopo kwenye hizo nafasi umewaassess ukagundua hawana qualification? Umeangalia vyeti vyao ukaona kwamba hawakustahili kuwa huko. Tuache kuleta hoja zisizo na msingi bwana, hangaika na wewe tengeneza CV yako nzuri, ukaombe kazi Ikulu. Bila shaka utapata, siyo kujiingiza kwenye malumbano ya kidaku kama ya Kubenea.

Ebu fikiri wewe....yaani elimu hizo wanazo watu toka Iringa tu nchi hii....yaani watu toka Iringa ndo wana-CV nzuri....ebu kuwa serious.Yaani kwa mfano TRA inapokuwa na wachaga kuanzia juu mpaka mtendaji wa kawaida kabisa tuseme nini.....yaani kuwa hao ndo watu pekee wanaostahili kufanya kazi TRA au ndo wao wanakuwa wanajua majibu ya interviews zote in advance?

Kwanini hiwe kwa Luhanjo....mbona nafasi hiyo hiyo alikuwa nayo Lumbanga,Rupi mbona hapakuwa na malalamiko hayo.Penye moshi........lisemwalo.....!
 
Back
Top Bottom