Ikulu yanuka ukabila? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yanuka ukabila?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Mar 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na Saed Kubenea

  RAIS Jakaya Kikwete sasa anatikiswa kwa tuhuma kwamba ikulu imekumbwa na ukabila, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa zinasema tuhuma hizo tayari ziko mezani kwake na zinamhusu mtendaji mkuu wa ikulu.

  Anayetajwa kuhusika na ukabila ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ambaye inadaiwa analinda watu wa mkoa anakotoka – Iringa.

  Lakini Luhanjo alipopigiwa simu kutaka kauli yake alijibu kwa sauti ya ukali, “Kwani kama wewe ni mwandishi wa MwanaHALISI ndiyo unipigie simu saa hizi?”

  Hiyo ilikuwa Jumamosi saa mbili usiku.

  Alipoelezwa kwamba gazeti liko tayari kukutana naye wiki hii wakati wowote atakapokuwa tayari, Luhanjo alijibu, “I will not talk with you for anything (Sitazungumza lolote na wewe).” Alikata simu.

  Hata hivyo chanzo cha taarifa hizi kinasema, “Luhanjo amejiimarisha kweli na anaweka watu wake kila eneo na wanataka kujenga himaya yao.”

  Luhanjo anahusishwa na upendeleo wa ukabila katika hatua ya serikali kuipa zabuni kampuni ya Peacock Hotels Limited kuendesha mradi wa hoteli katika jengo la Millennium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam.

  Inadaiwa Luhanjo ana mkono katika kubeba Peacock Hotels ambayo mmiliki na mkurugenzi mtendaji wake, Joseph Mfugale pia anatoka Iringa.

  Lakini Mfugale anakana kubebwa, akisema “Tulishindana tukashinda na kulipa dhamana, tena milioni nyingi – dola 165,000 (Sh. 171 milioni).”

  Alisema tatizo la fedha za dhamana walizotoa ni kwamba kulitokea mpango wa kuziiba ili tenda apewe mtu mwingine.

  “Waliposhindwa mpango wao, mkurugenzi wa raslimali aliamua kujiuzulu na sasa nasikia amepata kazi mahali pengine,” alidai Mfugale.

  Mfugale anasema fedha za dhamana zililipwa kupitia benki ya CRDB, tawi la Kijitonyama.

  Millennium Tower inamilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

  Mbali na Luhanjo, mwingine anayedaiwa kumbeba Mfugale ni Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Maimuna Tarishi ambaye pia anatoka Iringa.

  Tarishi ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya LAPF. Inadaiwa Mfugale aliwasilisha malalamiko kwa watendaji wa juu wa serikali kwa kile alichodai, “kuhujumiwa katika zabuni.”

  Tarishi hakupatikana kutoa maoni yake juu ya madai hayo. Katibu muhtasi wake aliyeko Dodoma alijibu kuwa Tarishi yuko Dar es Salaam na kwamba “simu yake ya mkononi aliisahau Dodoma.”

  Awali nyaraka za zabuni za Mfugale ziliwekwa kando kwa madai ya kukosekana dhamana ya benki, jambo ambalo alilalamikia.

  Imedaiwa kuwa baada ya Mfugale kulalamika, Luhanjo aliagiza uongozi wa TAMISEMI kufuatilia malalamiko hayo.

  Katika malalamiko yake, Mfugale anatuhumu Julius Mfukwe, ambaye alikuwa mkurugenzi wa vitegauchumi wa LAPF, kuchomoa nyaraka zake za dhamana za benki ili kubeba mmiliki wa Hotel ya Paradise.

  Tayari Mfukwe ameacha kazi katika mfuko huo na sasa ameajiriwa na Mamlaka ya Bandari nchini (THA).

  Alipoulizwa juu ya madai hayo ya Mfugale, Mfukwe alijibu kwa sauti ya upole, “Hii namba yangu umeipata wapi?”

  Alipoambiwa kuwa yeye ni mtu mkubwa anayefahamika, alijibu, “Kaka, nakushukuru lakini sina la kusema.”

  Alisema, “Mimi sipo huko tena. Siwezi kuongea chochote kinachohusu LAPF kwa kuwa si msemaji wao. Nakuomba uwatafute viongozi wa mfuko ndio watakueleza.”

  Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa kutoka serikalini, wakati wa ufunguaji zabuni ya kuendesha hoteli katika jengo hilo la Millennium Tower, Mfugale hakuwa ametimiza sharti la kuweka dhamana ya benki kama ambavyo tangazo la zabuni liliagiza.

  “Zabuni ilifunguliwa hadharani na kuhudhuriwa na kila muombaji. Huyu bwana hakuwa ameweka bond kwenye zabuni yake. Baada ya kuona kwamba amepoteza sifa, akaanza kutafuta msaada,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

  Kabla ya kukodishwa kwa Mfugale, hoteli ilikuwa inaendeshwa na kampuni ya African Sky kutoka Afrika Kusini. Kampuni inadaiwa iliondoka na deni la dola 400 milioni.

  Kwa utuki tu, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF ni Eliud Sanga na Meneja Mkuu ni Injinia G. Matovola wote kutoka Iringa.

  Kwa muda mrefu mkoa wa Iringa umetoa viongozi katika ofisi ya rais. Kwa mfano, Emilius Mzena, Augustine Mahiga na Hans Kitine wote kutoka Iringa, walikuwa wakurugenzi wa usalama wa taifa.

  Aidha, Kitine na Peter Siyovelwa wamewahi kuwa mawaziri ofisi ya rais wanaoshughulikia usalama wa taifa.

  Wengine ambao wanatoka Iringa na wako ofisi ya rais; na huenda kwa utuki tu ni Rajab Luhavi na Lumbila Fyataga ambao ni wasaidizi.

  Miongoni mwa watu mashuhuri kutoka Iringa ambao wamo katika nafasi za juu kimadaraka nchini ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

  Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la NIPASHE, Mchechu hakuwa miongoni mwa watu waliofanyiwa usaili kwa kuwa “hakuwa na sifa” ya kupewa kazi aliyoomba.

  Mchakato wa kumpata mkurugenzi mkuu wa NHC, ulisimamiwa na kampuni ya Price Water House Cooppers na uligharimu serikali zaidi ya Sh. 82 milioni.

  Hata hivyo, pamoja na kwamba Mchechu aliomba nafasi hiyo, hakuwa short listed (kuwa miongoni mwa waliopitishwa kwa kufanyiwa usaili).

  “Kwa hiyo serikali imetumia mamilioni ya shilingi za umma kwa kazi ambayo haikuwa na tija, kwa kuwa aliyeajiriwa hakufanyiwa usaili,” ameeleza mjumbe mmoja wa bodi iliyomaliza muda wake.

  Amesema serikali imelipa kampuni ya ushauri ya Price Water “lakini kazi yote iliyofanyika imetupwa kapuni.”

  Taarifa za baadaye zimesema kuwa uongozi wa NHC tayari umeidhinisha Mchechu kulipwa mshahara wa dola za Marekani 11,000 (Sh. 14 milioni) kwa mwezi, jambo ambalo linatajwa kuwa linaweza kuangamiza hata shirika lenyewe.

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mchechu ameacha malipo ya dola 16,000 kwa mwezi katika Benki ya Biashara Afrika (ABC) ambako alikuwa anafanyakazi.

  Haikufahamika kwa nini ameamua kuacha kazi penye mshahara mkubwa kuliko ule atakaokuwa anapata NHC.

  Source: Mwanahalisi, Issue No 181
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna dalili hizo zisizoweza kuthibitika kwa kuangalia hii habari!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ilisemekana kwamba Mwl Nyerere aliagiza ufanywse utafili kujua ni wananchi wenyeji wa mkoa gani waaminifu kuliko wengine hapa nchini. Majibu yakawa: Mkoa wa Iringa.

  Ndiyo aana wakaja watu wengi walioshika nyadhifa kubwa nyeti katika utawala hasa idara ya usalama. Isisahauliwe kwamba mkuruigenzi wa kwanza wa Taasisi ya kuzuia rushwa, Zakaria Maftah alkitoka huko huko.

  Kumbe hii si kweli, JKN alidanganywa baadhi yao walikuwa wezi tu -- kama vile Kitine, Balali.
   
 4. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dah! sasa inakuwaje hapa way foward please
   
 5. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  njaa ndio kila kitu.....dili ndio kwao pale pale ...hakuna jipya
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Kila kona Luhanjo,naona lisemwalo lipo na kama halipo laja,nchi hii kila mtu ni fisadi na kila aliye na nafasi huitumia kwa manufaa yake na tutake au tusitake hali hii haiwezi kubadilika hili ni zao la mfumo uliooza,kila kiongozi anaangalia masilahi yake na wapambe wake,Luhanjo siku hizi ndie amekuwa Mr fix ,kila sehemu ana mtandao wake na muungwana anamuangalia tu,huenda lao moja
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwanza huyu bwana nilisikia alikuwa kwenye likizo ya kustaafu nashangaa bado yupo ..huenda mkuu wa kaya anataka amalizie october then mwakan aje na mtu mpya..
  Hahaha mwana hapo umeniacha hoi duh!
   
 8. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  hmanA CHOCHOTE HAPA ,Kubenea is just another gun for hire to the highest bidder,amelipwa amchafulie jina CEO wa NHC,huy jamaa ni mchapa kazi,na ataweza kufanikisha kazi,isitoshe ni kijana na ametoka private sector,its time for a change,
  hawa consultant face eti price water na wengineo,ni matepeli wanatumia majina ya kampuni kubwa za ulaya,usahili gani wa milioni 82,huwa wanapewe tender na vigogo so ata maamuzi yao yanakuwa biased vilevile.
  kwa kifupi tumpe muda tuone changes ktk national housing.
   
 9. F

  Facts Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kumpakazia Kubenea. Yeye amenukuu tu, baadhi ya vyombo vya habari vilivyoandika kuhusu huyu fisadi wa NHC. Kwamba amepatikana kwa mizengwe. Sasa nakuambia ameteuliwa kutoka na nguvu ya Luhanjo. Huyu jamaa si mwadilifu kama unavyotaka tuamini. Alikuwa benki ya ABC ambayo ilitumika kupitisha mabilioni yetu ya EPA baada ya benki za nje kugoma kufanya kazi hiyo haramu.
   
 10. F

  Facts Member

  #10
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mtu wa RA huyu kama ilivyo kwa Luhanjo na Kikwete
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah si mchezo hii kali, nijuavyo wanyalukolo wagumu mno kuwabeba ndugu zao wawapo madarakani nina mifano mingi ya watu wapo kitaa na degree zao wanahaha kusaka ajira lakini ndugu zao wapo kwenye system na wanakula cake ya taifa lakini hawajawabeba hata siku moja.
   
 12. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  IKULU imelishangaa gazeti la Mwanahalisi na kukanusha habari zilizoandikwa Jumatano iliyopita na gazeti hilo zikidai kuwa kuna ukabila katika makazi na ofisi hizo za Rais.

  Habari za gazeti hilo litokalo mara moja kwa wiki zilimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, kuwa ndiye mhusika wa ukabila huo kwamba anawalinda watu kutoka mkoa anakotoka -Iringa.

  "Habari hii ni ya uongo na ya kizushi, inayostahili kupuuzwa na wananchi, kwa sababu habari hiyo ni ya kipuuzi na ya kutungwa, kama ilivyo sasa imekuwa tabia na desturi ya gazeti hili la Mwanahalisi.

  "Inasikitisha kwamba gazeti la Mwanahalisi ambalo lilianza kupata heshima, linadiriki kuzua habari ambazo hazina ukweli wala utafiti wowote," ilisema taarifa hiyo iliyotolewa juzi na Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, Dar es Salaam.

  Ilisema Luhanjo ni mtumishi mwadilifu wa umma na hajapata kujihusisha na ukabila katika utumishi wake wa muda mrefu wa umma.

  Isitoshe baadhi ya watu wanaotajwa katika habari hiyo kuwa walipata kuwa ama wako Ikulu kwa sasa kwa sababu ya kulindwa na Luhanjo, walikuwa Ikulu, wengine miaka mingi, kabla ya Luhanjo hajawa Katibu Mkuu Kiongozi mwishoni mwa mwaka 2005.

  "Hawa ni pamoja na Lumbila Fyataga ambaye amekuwa Ikulu tangu Awamu ya Tatu, Rajabu Luhwavi, marehemu Emilius Mzena, Balozi Augustine Mahiga na Hassy Kitine, wote hawa walifanya kazi Ikulu, kabla ya Luhanjo kuwa Katibu Mkuu Kiongozi," ilisema taarifa.

  Ilisisitiza kuwa ni jambo la kusikitisha na la aibu kwa mwandishi wa habari hiyo na mhariri wake, kuchapisha habari yenye upungufu mkubwa na wa wazi kama suala la watu wanaotajwa kuwa Ikulu kwa kulindwa na Luhanjo, wakati ukweli ni kwamba walikuwapo hata kabla ya Luhanjo.

  "Hili si jambo la kuhitaji waledi wa kupindukia au kubobea na tulitarajia waandishi wakomavu kujua kuwa masharti ya kwanza ya uandishi wa habari ni kuandika ukweli si porojo, uongo na uzushi wa mitaani," ilisema
   
 13. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #13
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kama kweli alikuwa ABC kwa mshahara wa 16,000$ na NHC alipwe 11,000$ ,mmmmh hapo mushkeli ,as i know so far watu always they demand the increases of salary and no the decrease, wadau tujadili hiki kipengele tunaweza pata jibu, kubenea anaweza kuwa sahii!
   
 14. k

  kashwagala Senior Member

  #14
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikiwa mmoja wa wafuatiliaji wa mambo na mwanamapinduzi wa chinichini wa nchi hii(we itisha mambo uone kama sintakuwa front) niliisoma hii habari siku gazeti lilipotoka nikaona iko too light,yaani haikuwa well researched na ndo maana jana ikulu walivyojibu ikaonekana kama wakoright vile! sio kwamba nawatetea hao waliobarikiwa sana kuliko watanzania wengine,au nimeasi na napingana na lililosemwa lakini maoni yangu ni kuwa ilitakiwa ifikishwe kwa uzito wake.
   
 15. F

  Facts Member

  #15
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikulu haijakanusha, bali imekuja na hoja za matusi. Kwa mfano, Ikulu inasema, " Isitoshe baadhi ya watu wanaotajwa katika habari hiyo kuwa walipata kuwa ama wako Ikulu kwa sasa kwa sababu ya kulindwa na Luhanjo, walikuwa Ikulu, wengine miaka mingi, kabla ya Luhanjo hajawa Katibu Mkuu Kiongozi mwishoni mwa mwaka 2005.

  "Hawa ni pamoja na Lumbila Fyataga ambaye amekuwa Ikulu tangu Awamu ya Tatu, Rajabu Luhwavi, marehemu Emilius Mzena, Balozi Augustine Mahiga na Hassy Kitine, wote hawa walifanya kazi Ikulu, kabla ya Luhanjo kuwa Katibu Mkuu Kiongozi..."

  Katika habari yote MwanaHALISI hawajasema kwamba hawa watu wameletwa na Luhanjo.
  Gazeti limesema, "Kwa utuki tu, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF ni Eliud Sanga na Meneja Mkuu ni Injinia G. Matovola wote kutoka Iringa.

  Kwa muda mrefu mkoa wa Iringa umetoa viongozi katika ofisi ya rais. Kwa mfano, Emilius Mzena, Augustine Mahiga na Hans Kitine wote kutoka Iringa, walikuwa wakurugenzi wa usalama wa taifa.

  Wengine ambao wanatoka Iringa na wako ofisi ya rais; na huenda kwa utuki tu ni Rajab Luhavi na Lumbila Fyataga ambao ni wasaidizi. Aidha, Kitine na Peter Siyovelwa wamewahi kuwa mawaziri ofisi ya rais wanaoshughulikia usalama wa taifa.Kwa kauli hii, inaonyesha kuwa huyu Salva hajui hata maana ya neno Utuki. Tuhuma za Luhanjo hapa ni ni kuingilia zabuni na kumbeba Mfugale ambaye hakuwa na sifa. Ndiyo msingi wa stori ya MwanaHALISI.

  Luhanjo ni mkabila na analundo la tuhuma. Salva hajajibu hoja badala yake ametaka kutetea mwabwana zake.
   
 16. F

  Facts Member

  #16
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salva jibu hoja acha matusi
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hapana cha kujadili hapa ili kumsaidia Kubenea katika kuburunda kwake. Hii habari haina chochote cha maana kwani imekuwa ikijichanganya changanya. Iweje mtu anaependelewa apitie hatuwa zote hizo za kisheria katika kuipata tenda aliyonyimwa iwapo kama upendeleo upo?. Halafu hili la kunyofoa watu wa sehemu fulani katika nyanja tofauti kuna maana gani kwani bado kuna sehemu nyengine nyingi ambazo unaweza ukakuta zinaongozwa na watu wa kutoka sehemu moja? Hizi ni isolated cases na hata hivyo ameshindwa kuonyesha kuwa nafasi hizo zilikingiwa kifuwa na Ikulu.
  Nafikiri amekosa habari kwa muda mrefu hivyo anaokoteza tu.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Upuuzi mtupu! magazeti ya Bongo jamani tafran tupu. Sasa ikiwa hawa wafanyakazi Ikulu ni watu kutoka Iringa inahusiana vipi na Ukabila yaani mtu akitoka Iringa basi lazima awe ni kabila fulani linaloleta Ukabila!
   
 19. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Gazeti limecheemsha hilo!sioni hoja ya maana hapo!
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hizi thread/ magazeti mengine . mhhhh

  Kumbe % kubwa ya habari za gazeti la mwanahalisi niTetesi. Ukiondoa Hoja ya bosi NHC ambayo tatizo sio ukabila ni mfumo uliotumika habari nyingine ni tetesi tena zisizokuwa na kichwa wala miguu[/B]

  Muandishi hajui human being wanakuwa appraised na vitu tofauti na selef estemm tofauti katika vipindi tofauti. Kuna wengine wanaacha kazi za kukaa kwenye madesk BOT na kwenda kutafuta kazi zenye challenge tena kwa mshahara mdogo.

  Ukiondoa Mfumo Mbovu uliotumika kumpata Msechu hata kama ni Kubenea akipewa kazi ya kuwa mkurugenzi wa TBC au BBC idhaa ya kiswahili hata kama watamlipa hela ndogo kuliko anyopata sasa hivi itakuwa vigumu kukataa.

  Sio kila Kinachoadikwa JF ni Information. Nyingine ni data tu waandishi wa kweli wanatakiwa wafanyie uchunguzi na kuhakiki. Sio kulisha watu sumu kwa agenda binafsi.

  Kama ni hivi kila mtu anaweza kuwa mwandishi.
   
Loading...