Ikulu yamshangaa Dk. Mahanga

Ikulu yamshangaa Dk. Mahanga

Magu amesimamia wizara ya ujenzi kwa miaka 20 tunaijua misimamo yake na kazi zake tunazijua. Nilimpigia kura Magufuli siyo kwa kubahatisha.

Ndio kwanza gia namba moja
Nyie subirini tu na makelele yenu muda so mrefu hatuta waona humu kwa aibu
 
12498611_1018094404921684_355653045_n.jpg
Huyu alikimbilia ukawa leo anajifanya mchambuzi wa siasa
Bora alivyoshindwa kura za maoni CCM hapa segerea
Alikuwa mbunge mzigo hapa Segerea
Kazi yake ilikuwa kutongoza sekretari wake tu huko wizara ya kazi
 
Wanadhani kujenga hoja ni kusema meneno mengi. Wanadai Magufuli alisema atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, kwao Baraza la Mawaziri linaishia kwa Waziri bila ya kujua waziri ni msimamizi wa wizara inayoendeshwa na Katibu Mkuu. Lengo la Magufuli lilikuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali na ndiyo kina Mahanga wanamtanabahisha kwamba kama ana Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu wa Kuu kwa kiwango hicho basi hakuna alichofanya!!
Hivi hujaelewa kweli majibu ya Sefue au umeamua kujitoa ufahamu?

Hoja ya Mahanga ingekubalika kama tu rais Dkt Magufuli angeteua makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu kuvuka idadi ya 54 ya serikali ya Kikwete...Lakini badala yake rais Dkt Magufuli amepunguza idadi ya makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu na kuwa 49 tu kwenye serikali yake.

Mnyonge mnyongeni...haki yake mpeni. Je, kutoka 54 hadi 49...idadi imepungua au imeongezeka? Ukipata jibu mwambie Mahanga akajifunze hesabu.
 
Swala alisema atapunguza idadi ya wizira na kapunguza Ila hakusema mkatibu wa kuu sasa nini mnataka Hpa kazi tu
 
Nani mwenye Vote kati ya waziri na Katibu wa wizara

Kuna uhusiano gani kati ya katibu mkuu kusimamia matumizi ya wizara kwa kuwa na vote na kupungua kwa idadi ya mawaziri? Kwa utaratibu wa zamani kila katibu mkuu alikuwa na waziri wake wa kumhudumia kutoka kwenye vote yake sasa kwa utaratibu wa sasa badala ya kuwa na mawaziri watatu tuna waziri mmoja akiwaongoza makatibu wakuu wake watatu; huoni mantiki ya kupunguza matumizi hapo?
 
Hiv watu wamesahau kauli z jpm?alisema ataunda serikali ndogo yenye wachapakaz,sasa serikal ndogo iko wapi,hata mawazir watafuta promo kwenye media wamekuwa wakurupukaji tu.
 
Nonsense! Jifunze kujenga hoja kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa imetolewa na chanzo rasmi cha serikali...Sasa sijui unataka nini cha ziada.
kwa hiyo kama kimetolewa na chanzo rasmi cha serikali ndio nini?acha ujuha wewe!!!escrow,epa na ufisadi wote ulitetewa na ikulu and yet kilichokuja kubainika ni disaster.
 
Kuna uhusiano gani kati ya katibu mkuu kusimamia matumizi ya wizara kwa kuwa na vote na kupungua kwa idadi ya mawaziri? Kwa utaratibu wa zamani kila katibu mkuu alikuwa na waziri wake wa kumhudumia kutoka kwenye vote yake sasa kwa utaratibu wa sasa badala ya kuwa na mawaziri watatu tuna waziri mmoja akiwaongoza makatibu wakuu wake watatu; huoni mantiki ya kupunguza matumizi hapo?
Wewe hujaelewa....Hapa hatusemi Katibu kumhudumia waziri

Lah....Kila katibu anakuwa na bajeti yake na kurugenzi zake...Meaning ukiongeza idadi ya makatibu unaongeza idadi ya wakurugenzi
 
Intention ni kupunguza gharama za kulipa mishahara hao watendaji wa serikali.
Je hao makatibu wanafanya kazi bure hadi sefue ashangazwe na kauli ya Mahanga??
 
Binafsi naona hiyo ni sahihi kabisa, kwa nje inaweza kuonekana ni wizara moja,kumbe kihualisia zimeungana wizara tatu,sasa hapo mkuu unategemea makatibu watakuwa wangapi?

Lengo la kuunganisha Wizara ni kupunguza ukubwa wa baraza, sasa endapo kama utaweka makatibu kulingana na ukubwa wa Wizara itakuwa haina maana ya kuziunganisha!!!!!

Hivyo tukubaliane kuwa Mh. Rais ameshindwa katika hili.
 
Kwani serikali ni nini? Maana unaposema nitapunguza Mawaziri wakati huo huo unaongeza utitiri wa watu wengine kwenye hiyo hiyo serikali unafanya nini sasa! Tuna serikali kubwa isiyo na tija kwa wananchi!!
 
Kwani tatizo nini
tunaangalia utendaji Na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom