Ikulu yamshangaa Dk. Mahanga

Ikulu yamshangaa Dk. Mahanga

Makatibu wakuu 2 .manaibu 3 si angefanya 3 kwa tatu basi. Utwala wa makaratasi no management skills at all.
 
HOJA SI UKUBWA WA BARAZA, HOJA NI UKUBWA WA GHARAMA ZA KUENDESHA SERIKALI

Nimefuatilia jinsi ambavyo hoja yangu niliyoitoa juzi kwa nia njema ilivyojadiliwa nchini kwa kuungwa mkono na wengi na wengine kuipinga. Mimi nadhani hoja yangu isijadiliwe au kukanushwa kisiasa, bali iangaliwe tu kiuhalisia ili kusaidia Serikali ya Rais Magufuli.

Aidha najua sana kwamba katibu mkuu siyo mjumbe wa baraza la mawaziri. Lakini najua vile vile kwamba jina au cheo tu cha uwaziri si kila kitu kwenye kupunguza gharama za kuendesha serikali. Gharama za kuendesha serikali ni idadi ya mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara mbalimbali za serikali, na gharama zingine za kuendesha idara zao.

Na wala sijapinga mazuri anayofanya rais hadi sasa. Mbona pale rais alipofanya vizuri tumempongeza? Kwa mfano kutumbua majipu ambayo yaliivishwa tayari na serikali ya awamu ya nne. Vile vile alipopunguza idadi ya wizara na idadi ya mawaziri kutoka 29 kufikia 19 mbona tulipongeza? Na hapa tuliamini ni mwanzo wa kupunguza ukubwa na gharama za kuendesha serikali. Nasema mwanzo kwa sababu ukubwa na gharama za kuendesha serikali si kupunguza tu idadi ya wizara na mawaziri, bali kupunguza pia idadi ya makatibu wakuu ili kulingana na idadi ya wizara....ni kupunguza na kuunganisha idara mbalimbali za serikali na wakurugenzi wake. Ukifanya hivyo ndiyo unapunguza gharama za kuendesha serikali. Na hii ndiyo ilikuwa ahadi ya Magufuli kwenye kampeni.

Lakini kama ameona kwamba kuleta ufanisi serikalini lazima ajaze watendaji wengi kwenye wizara, kama anavyoendelea kufanya, aseme tu hivyo, lakini akijua hatua hiyo haitapunguza gharama za kuendesha serikali ambazo wabunge, hasa wa upinzani, wamekuwa wakipigia kelele kwenye serikali ya awamu ya nne.

Hata hivyo hili la kuleta ufanisi pamoja na kuteua makatibu wakuu wengi wanaoonekana wazuri kwa utendaji, kuna wizara ambazo hakushauriwa vizuri na akateua makatibu wakuu wale wale na kuwarudisha pale pale wakati walikuwa "mizigo" na walikwamisha mno sekta husika katika awamu ya nne. Hawa ni watu ambao rais au katibu mkuu kiongozi angeenda kwenye wizara zao leo na kuitisha kura ya siri ya wakurugenzi na wafanyakazi wote, asilimia 90 ya watumishi wote wangewakataa makatibu wakuu hao. Ni heri kukosea kuteua kwa mara ya kwanza kuliko kukosea kuteua "mizigo" iliyokuwepo.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi ya gharama za kuendesha serikali, nimesema na ninarudia kusema: bila kutakiwa kutoa takwimu hapa, gharama za waziri mmoja na ofisi yake ni ndogo sana kulinganisha na gharama za katibu mkuu mmoja na ofisi yake, kwani waziri tayari analipwa sehemu kubwa ya mshahara na marupurupu kutokana na yeye kuwa mbunge (na hapa niwajuze baadhi ya walionipinga kwamba waziri halipwi mishahara miwili - ya ubunge na ya uwaziri).

Na hapa hatujajadili mikanganyiko mingine ambayo haijawekwa wazi hadi sasa. Kwa mfano kutakuwa na afisa masuhuli mmoja wa wizara au maafisa masuhuli wawili au watatu kwenye baadhi ya wizara? Kwa kawaida wizara inakuwa na fungu (vote) moja; sasa katika hali hii kila idara ya wizara itakuwa na fungu (vote) tatu (ukiacha idara zinazojitegemea)? Je hili la afisa masuhuli mkuu wa wizara kutokuwepo haitaleta shida katika uwajibikaji? Na vipi katika kusimamiwa na bunge na kamati zake? Nani hasa mtendaji mkuu wa wizara atakayewajibika kwa bunge kwa mambo ya kisera ya wizara nzima? Wote watatu?

Hatua hii ya rais magufuli ya kuwa na makatibu wakuu wa vitengo (na siyo wa wizara) ingesubiri hoja ya kikatiba ya mawaziri kutokuwa wanasiasa (wabunge) ili wawe watendaji wakuu na wawajibikaji wakuu wa wizara (cabinet secretaries) kama ilivyo nchi ya jirani ya Kenya.

Lakini kwa sasa ningeshauri hoja hii iahirishwe halafu turudi tena kuijadili baada ya "taasisi" ya makatibu wakuu wapya kupangwa - kwa maana ya kila mmoja kupangiwa idara na wakurugenzi chini yake (na ninahisi kutakuwa na nyongeza ya idara). Na baada ya hapo uchambuzi wa gharama za kuendesha serikali hii ufanywe na ulinganishwe na gharama za uendeshaji wa serikali ya mwisho ya JK ambayo tayari ilikuwa inalalamikiwa kwa ukubwa wake.

Dr. Milton Makongoro Mahanga

Safi sana

This is the Opposition we need

Sio ule wa Dr Mihogo kutunishana misuli na Polisi....Tulichoka na siasa za kila siku kusumbuana na polisi...we need criticisms kama hizi.....RiHell Dr Mihogo

safi sana

cc MTAZAMO
 
Slaa aliposhindwa mkasingizia ni kwa sababu matokeo ya urais hayakubandikwa ukutani.

Mwaka huu yamebandikwa mkapigwa ,mmekeukia tena katiba!?!?!

Katiba itabadilishwa na mtapigwa sijui mtasingizia nini.

Hivi huko Pemba, Moshi, Arusha ikitumika katiba gani vile

Yaani bado huelewi tu

Mngeweza hata kuitoa Pemba na Mwanza yote lakini mnge u maintain Urais ...sijui kichwa chako kina funza...mbona mgumu kuelewa hivi
 
mi naic kweny makatib kalenga utendaji na uadilifu watu ambao hofu itakuwa kubwa kutimliwa watakapoenda kinyume kuliko mawazir wanaoweza kuvuliwa wakabaki na ubunge hajalenga matumiz ya pesa
Sasa alikuwa na maana gani kusema atapunguza ukubwa wa serikali na kubana matumizi?
 
Mahanga ana akili sana. Usiniulize ni kwa nini hakuzitumia alipokuwa waziri, maana kama wanashindwa kuzitumia akili za Jaji Warioba watakubali kuzitumia za Mahanga!!
 
Mahanga ana akili sana. Usiniulize ni kwa nini hakuzitumia alipokuwa waziri, maana kama wanashindwa kuzitumia akili za Jaji Warioba watakubali kuzitumia za Mahanga!!

Ukiwa ndani ya CCM unabaki kuwa mjinga tu.......Si unaona Makongoro alivyo Smart...Lakini ndani ya CCM wote mnakuwa ma tabula lasa
 
Ni mapema sana kumkosoa magu vile vile ni mapema mno kusifia sarakasi zinazoendelea kwa sasa hivi.
Magu amesimamia wizara ya ujenzi kwa miaka 20 tunaijua misimamo yake na kazi zake tunazijua. Nilimpigia kura Magufuli siyo kwa kubahatisha.

Ndio kwanza gia namba moja
 
Magu amesimamia wizara ya ujenzi kwa miaka 20 tunaijua misimamo yake na kazi zake tunazijua. Nilimpigia kura Magufuli siyo kwa kubahatisha.

Ndio kwanza gia namba moja

Na ndio ni wizara iliyooiingiza sana hasara serikali

Imagine kulipa Penalty za makusudi kwa wakandarasi.....Anyway...He was the best among wabovu wote wa CCM
 
Ukiwa ndani ya CCM unabaki kuwa mjinga tu.......Si unaona Makongoro alivyo Smart...
Yaani tangu wakati wa Kampeni nilikuwa nikisoma makala zake nikawa najiuliza alikosea wapi? Lakini jamaa zetu wanatulazimisha tuwe tunapiga makofi kwa kila alifanyalo bwana mkubwa. Mwenyewe Mahanga kasema hoja yake ijibiwe kitaalamu, sasa CCM wamewaachia kina "Kibajaji" wa humu JF wanajaza "Server" ya Jf kwa Porojo na Propaganda zao.
 
[QUOTE="Bukyanagandi, post: 15021107, membgemea makatibu watakuwa wangapi?[/mkuu unaposema inawezekana hiyo bado ni hisia zakotu.lakin muundo wa serikali ya inayowaongoza watu hauna usiri huo.hapa ni wazi alichofanya makufuli ni kuwalaghai wananch.kua ataundq serikali ndogo akijua wananch wanajua serikali ni mawaziri hakujua kua wananch wameelimika.
 
Sasa alikuwa na maana gani kusema atapunguza ukubwa wa serikali na kubana matumizi?
Dah! Nilitamani sana kujiunga CHADEMA lakini kwa michango ya kipuuzi ya wana CHADEMA humu JF na kwingineko nikaona ni vyema niwe sina chama.

Umeelezwa, makatibu wakuu wametoka 54 awamu ya nne hadi 49 awamu hii ya 5...kimantiki...idadi imepungua.

Kama ulifatilia kampeni za rais Dkt Magufuli...alisema atapunguza baraza la mawaziri...na amefanya hivyo. Kumbuka, baraza la mawaziri ukaliwa na mawaziri tu. Manaibu waziri na makatibu wakuu hawaingii kwenye baraza la mawaziri. Hii ipo kikatiba.

Kuhusu ukubwa wa serikali...unajua serikali inahusisha watendaji wote? Ikiwemo watumishi wa umma...kupunguza watumishi wa umna ndio kupunguza ukubwa wa serikali. Juzi juzi lilitolewa tangazo kuwa mashirika ambayo hayazalishi...wafanyakazi wake watatimuliwa...CHADEMA walikosoa. Sasa mnataka serikali ifanye nini labda?
 
Yaani Moderators wasipoangalia kwa uchangiaji wa kijinga hivi wa hawa vijana hili jukwaa halitakuwa tena "HOME OF GREAT THINKERS"

Yaani nashindwa kuelewa inawezekanaje hesabu ndogo hivi inawashinda watu?? Ndio maana mzee wao aliliona hili tatizo na ndipo akasema kipaumbele chake ni "ELIMU" "ELIMU" "ELIMU"....

- Serikali iliyopita mawaziri wote na manaibu ni 55
- Serikali mpya mawaziri wote na manaibu ni 35

- Serikali iliyopita makatibu wakuu wote na manaibu ni 54
- Serikali mpya makatibu wa kuu wote na manaibu ni 49

Hivi hapo gharama itabaki ile ile???? Hapo tumepunguza mishahara ya mawaziri 21 na makatibu wakuu 5. Kweli elimu elimu elimuuuu!!!!!

Yaani Kama hesabu rahisi hivi za kujumlisha na kutoa kisha kutafuta ulinganifu mtu hawezi si ni majanga haya wajameni????

Queen Esther

Dah! Nilitamani sana kujiunga CHADEMA lakini kwa michango ya kipuuzi ya wana CHADEMA humu JF na kwingineko nikaona ni vyema niwe sina chama.

Umeelezwa, makatibu wakuu wametoka 54 awamu ya nne hadi 49 awamu hii ya 5...kimantiki...idadi imepungua.

Kama ulifatilia kampeni za rais Dkt Magufuli...alisema atapunguza baraza la mawaziri...na amefanya hivyo. Kumbuka, baraza la mawaziri ukaliwa na mawaziri tu. Manaibu waziri na makatibu wakuu hawaingii kwenye baraza la mawaziri. Hii ipo kikatiba.

Kuhusu ukubwa wa serikali...unajua serikali inahusisha watendaji wote? Ikiwemo watumishi wa umma...kupunguza watumishi wa umna ndio kupunguza ukubwa wa serikali. Juzi juzi lilitolewa tangazo kuwa mashirika ambayo hayazalishi...wafanyakazi wake watatimuliwa...CHADEMA walikosoa. Sasa mnataka serikali ifanye nini labda?
 
Dah! Nilitamani sana kujiunga CHADEMA lakini kwa michango ya kipuuzi ya wana CHADEMA humu JF na kwingineko nikaona ni vyema niwe sina chama.

Umeelezwa, makatibu wakuu wametoka 54 awamu ya nne hadi 49 awamu hii ya 5...kimantiki...idadi imepungua.

Kama ulifatilia kampeni za rais Dkt Magufuli...alisema atapunguza baraza la mawaziri...na amefanya hivyo. Kumbuka, baraza la mawaziri ukaliwa na mawaziri tu. Manaibu waziri na makatibu wakuu hawaingii kwenye baraza la mawaziri. Hii ipo kikatiba.

Kuhusu ukubwa wa serikali...unajua serikali inahusisha watendaji wote? Ikiwemo watumishi wa umma...kupunguza watumishi wa umna ndio kupunguza ukubwa wa serikali. Juzi juzi lilitolewa tangazo kuwa mashirika ambayo hayazalishi...wafanyakazi wake watatimuliwa...CHADEMA walikosoa. Sasa mnataka serikali ifanye nini labda?
Ndg hawa watu wanaoitwa chadema wamefilisika kichwani baada ya kuondoka Slaa ,hawana wanachokisimamia kwa sasa.

Kila mmoja anatoka anavyojisikia yeye.

Huyu anatetea wakwepa kodi,
Mwingine anatetea ufisadi
Yule anatetea watu Wa mabondeni lkn wakisombwa na mafuriko analaumu ccm.
Mbowe anaficha mabilioni nje ya nchi lkn bavicha wanapongeza tu.
Mkurugenzi Wa kinondoni amesimamishwa kwa ubadilifu chadema wakapeleka kesi mahakamani eti ameonewa.

Viongozi Wa chadema wameteua viongozi Wa ccm kuwa viti maalumu chadema lkn bado bavicha wanasjangilia tu!?!?!?!?

Hivi chama chenye katiba yake kinaanzaje kuteua kiongozi Wa ccm kuwa mbunge Wake!?! Hakina wanachama,!?!?!
 
Yaani tangu wakati wa Kampeni nilikuwa nikisoma makala zake nikawa najiuliza alikosea wapi? Lakini jamaa zetu wanatulazimisha tuwe tunapiga makofi kwa kila alifanyalo bwana mkubwa. Mwenyewe Mahanga kasema hoja yake ijibiwe kitaalamu, sasa CCM wamewaachia kina "Kibajaji" wa humu JF wanajaza "Server" ya Jf kwa Porojo na Propaganda zao.
hoja hizi kina jingalao hawaziwezi..imagine thinking kama ya Lizaboni...kweli inaweza hoja hizi
 
y
Ndg hawa watu wanaoitwa chadema wamefilisika kichwani baada ya kuondoka Slaa ,hawana wanachokisimamia kwa sasa.

Kila mmoja anatoka anavyojisikia yeye.

Huyu anatetea wakwepa kodi,
Mwingine anatetea ufisadi
Yule anatetea watu Wa mabondeni lkn wakisombwa na mafuriko analaumu ccm.
Mbowe anaficha mabilioni nje ya nchi lkn bavicha wanapongeza tu.
Mkurugenzi Wa kinondoni amesimamishwa kwa ubadilifu chadema wakapeleka kesi mahakamani eti ameonewa.

Viongozi Wa chadema wameteua viongozi Wa ccm kuwa viti maalumu chadema lkn bado bavicha wanasjangilia tu!?!?!?!?

Hivi chama chenye katiba yake kinaanzaje kuteua kiongozi Wa ccm kuwa mbunge Wake!?! Hakina wanachama,!?!?!

wewe mbona mgumu sana kuelewa
 
hoja hizi kina jingalao hawaziwezi..imagine thinking kama ya Lizaboni...kweli inaweza hoja hizi
Wanadhani kujenga hoja ni kusema meneno mengi. Wanadai Magufuli alisema atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, kwao Baraza la Mawaziri linaishia kwa Waziri bila ya kujua waziri ni msimamizi wa wizara inayoendeshwa na Katibu Mkuu. Lengo la Magufuli lilikuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali na ndiyo kina Mahanga wanamtanabahisha kwamba kama ana Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu wa Kuu kwa kiwango hicho basi hakuna alichofanya!!
 
Dah! Nilitamani sana kujiunga CHADEMA lakini kwa michango ya kipuuzi ya wana CHADEMA humu JF na kwingineko nikaona ni vyema niwe sina chama.

Umeelezwa, makatibu wakuu wametoka 54 awamu ya nne hadi 49 awamu hii ya 5...kimantiki...idadi imepungua.

Kama ulifatilia kampeni za rais Dkt Magufuli...alisema atapunguza baraza la mawaziri...na amefanya hivyo. Kumbuka, baraza la mawaziri ukaliwa na mawaziri tu. Manaibu waziri na makatibu wakuu hawaingii kwenye baraza la mawaziri. Hii ipo kikatiba.

Kuhusu ukubwa wa serikali...unajua serikali inahusisha watendaji wote? Ikiwemo watumishi wa umma...kupunguza watumishi wa umna ndio kupunguza ukubwa wa serikali. Juzi juzi lilitolewa tangazo kuwa mashirika ambayo hayazalishi...wafanyakazi wake watatimuliwa...CHADEMA walikosoa. Sasa mnataka serikali ifanye nini labda?
54 kwa 49 ?na wewe ni mkurupukaji kama wenzako tu huna ulijualo zaidi ya ushabiki wa ki CCM
 
Back
Top Bottom