Ikulu yaitisha mkutano na wanahabari Jumatatu 22 Desemba saa Tatu Kamili Asubuhi

Taarifa iliyotolewa hivi Punde na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam, imeeleza kuwa kumeitishwa Mkutano na waandishi wa habari Jumatatu asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkutano utafanyika saa tatu kamili asubuhi na kila chombo kimetakiwa kutuma Mwandishi pamoja na mpiga picha ambao wametakiwa kuwa tayari wameketi vitini ifikapo saa Mbili Unusu bila kuchelewa wala kukosa.

Agenda ya mkutano huo ni "SHUGHULI MAAUM" na hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa.

Ikumbukwe pia kwamba mchana Jumatatu Rais ataongea na wazee wa Dar es salaam.

Huenda (NARUDIA "HUENDA") Mkutano wa wazee ukatumika kufafanua yatakayotoka katika mkutano na wanahabari Asubuhi.

Kesho kuna kila dalili zinaonyesha kuwa wazeealioalikwa wamepewa maswali ya kuuliza. Maaana nasikia wameambiwa waende walioalikwa tu. Wengine wafuatilie kwa radio na TV.
 
Kimenuka aisee
 

Attachments

  • 1419195918148.jpg
    1419195918148.jpg
    58.1 KB · Views: 23,344
Ningekuwa na Uwezo ningempatia JK msuba awatimue wasaidizi wote pale IKULU... Wanamshauri nini? Kulikuwa na haja gani ya kuvuta muda wote huu na ku-create tension isiyokuwa ya Lazima? Kwani hao waliohusika ni lazima waendelee kuwa watumishi wa Umma? hawajui kuwa Cheo ni Dhamana? Napatwa wasiwasi mwingi sana kwanini wanaendelea kung'ang'ania ofisi za umma!!! CCM must go....
Tusijekushangaa wanaenda kufundwa namna ya kuja kurusha taarifa / mazungumzo yake na vikongwe wa Dar.
Hii nchi kila kukicha ni uvumbuzi tu
 
nadhani hili tamko la chadema limewachangaya waandishi wa hotuba ya raisi.

Haya ndio mahaba ya kijinga ambayo mtoto wa kiume hupaswi kuwa nayo. Hivi Ikulu imetangaza tangia lini kama jumatatu ndio kutakuwa na mkutano? Na hilo tamko la hilo genge jengine limetoka lini? Sasa ukisema Ikulu inaogopa hicho chama sijui utakuwa unaakili timamu ww?
 
I can feel this attention, yaan tenzi dume anapelekeshwa mchakamchaka ile mbayaa, nasema tena kesho tusitarajie chochot kwa jk juu ya mafisadi it is likely Jk ameshauriwa vibaya zaidi. tathmini yangu inanipa JK katika utendaji wake anwaamuami sana Muhongo na Tibaijuka this is all about.
 
Pro-Chadema kwa viroja Rais akiwa kimya wanalalamika Rais akifanya kazi yake kuwapiga watu chini wanalalamika tena wao ni kupinga kila kitu.

wanachosha sana,kutwa kulalamika kama mademu
 
Pro-Chadema hawataki rais awapige chini wizi wa Escrow.

teh teh teh
 
Back
Top Bottom