Ikulu yaacha kutumia YAHOO email, sasa wanatumia GMAIL

HNIC

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
1,898
Reaction score
2,202
Baada ya wana JF kuwasuta weee sasa wamebadili e-mail. sasa wanatumia GMAIL.

Si haba maana baada ya miaka 50 ya uhuru mwendo ndio huo na nina hakika mheshimiwa Rais anasoma hii maada na kuona jinsi gani watendaji wake walivyokuwa wanajua kutumia pesa.

Bajeti ya idara ya mawasiliano kwa mwaka ni dola milioni 10 lakini wameshindwa kuwa na e-mail zinazoeleweka

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA ( Sijajua Ikulu zanzibar kama bado wanatumia NETSCAPE au HOTMAIL)

Tazama hapa:

MICHUZI BLOG: RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI
 
naona kama vile mungu alisha tu abandon

tumebaki wenyewe tuuu
 
Mnaongozwa na kichwa nazi mnategemea mtakua na watendaji makini? Mwendo ni wakinazinazi tu.
 
acha dharau wewe

gmail ina matatizo gani?
 
Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ni vilaza. JK anahutubia leo, hotuba yake wanaitoa kesho mchana au kesho kutwa. JK anaongea na wageni wa Kiingereza wanapeleka taarifa kwa magazeti ya Kiingereza kwa Kiswahili, magazeti ya Kiingereza yakitafsiri hicho Kiswahili kurudi Kiingereza maana halisi inapotea. Hawako Twitter wala hawajui kutumia social networks. Angalia Kurugenzi ya Habari ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya inavyofanya kazi kiuweledi.
 
Baada ya wana JF kuwasuta weee sasa wamebadili e-mail. sasa wanatumia GMAIL.

Si haba maana baada ya miaka 50 ya uhuru mwendo ndio huo na nina hakika mheshimiwa Rais anasoma hii maada na kuona jinsi gani watendaji wake walivyokuwa wanajua kutumia pesa.

Bajeti ya idara ya mawasiliano kwa mwaka ni dola milioni 10 lakini wameshindwa kuwa na e-mail zinazoeleweka

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA ( Sijajua Ikulu zanzibar kama bado wanatumia NETSCAPE au HOTMAIL)

Tazama hapa:

MICHUZI BLOG: RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI

Ni kitu kisichoweza kueleweka kwamba Ikulu kupitia serikari haijawahi kutafakari kuwa na server zake wenyewe. Hivi hao wataalamu wa ict wanaolipwa malundo kuishauri serikari hata hawaoni aibu?
 
Wakuu washaiacha hii nchi iserereke yenyewe, itakakoishia ni Mungu tu ndo anajua.
Ova
 
hivi vitu vidogo sana infact hatuku viahidi kwenye kampeni

hizi za yahoo na gmail 2015 tunazi deactivate tunaondoka zetu

watakao kuja wata waanzishieni mnazozitaka(info@ikulu.go.tz)

cheeers
from magogoni
 
Sio hilo tu ndugu zangu hata kanuni ndogondogo za uandishi hawajui. Kwa mfano mwisho wa tangazo wameandika: Imetolewa na; Hiyo semicoloni siyo mahali pake hapo. Haikupaswa kuwepo. Pili, tarehe wameandika hivi: 16 Septemba, 2014. Hakuna mtindo wa kuandika tarehe wa namna hiyo. Walipaswa kuondoa hiyo koma. Mwezi ukikaa katikati hakuna tena kuweka koma. Au waanze na mwezi km wanapenda kutumia sana koma. Wangeandika hivi: 16 Septemba 2014 auSeptemba 16, 2014 au 16.9.2014. Naamini hili darasa ambalo ni elementary sana (Communication Skills ya sekondari) litakuwa limewafikia. Jamani ikulu ni shidaa!
 
Directorate of Communications ya Ikulu wamekaa kukimbilia tu safari za nje lukuki za JK wale per diem za $$. Ufanisi ni sifuri, lakini kwa kuwa bosi wao JK hajui tufauti ya mediocrity na professionals yote ni kheri tu waache waende mwendo huo huo amalize ngwe yake 2015
 
Ikulu kuna Kurugenzi ya Mawasiliano jina tu. Rais makini asingekubali wababaishaji wa mawasiliano ya umma namna hii. Miaka mingi kwanza Ikulu haina hata website, juzi tu e-govt agency ndio imeokoa jahazi na kuanzisha tovuti ya Ikulu. Miaka kadhaa eti Ikulu nzima wanatumia blogspot hawana tovuti rasmi. Utoto kweli huu.
 
Baada ya wana JF kuwasuta weee sasa wamebadili e-mail. sasa wanatumia GMAIL.

Si haba maana baada ya miaka 50 ya uhuru mwendo ndio huo na nina hakika mheshimiwa Rais anasoma hii maada na kuona jinsi gani watendaji wake walivyokuwa wanajua kutumia pesa.

Bajeti ya idara ya mawasiliano kwa mwaka ni dola milioni 10 lakini wameshindwa kuwa na e-mail zinazoeleweka

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA ( Sijajua Ikulu zanzibar kama bado wanatumia NETSCAPE au HOTMAIL)

Tazama hapa:

MICHUZI BLOG: RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI
Huko ni kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi...yahoo ni bora kuliko wenzake maana mara moja moja hua anaigomea NSA kutoa mawasiliano ya wateja wao.End the Lie – Independent News | Alternative News Daily
 
Back
Top Bottom