Ikulu ya Tanzania yahusishwa na Escrow

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,579
33,680
141128105653_tanzania_state_house_512x288_ikulu.jpg

Ikulu ya rais nchini Tanzania

Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.

Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.chanzo.http://www.bbc.co.uk/…/habari/2014/11/141128_ikulu_tanzania…
 
Hata anayeishi humo ikulu naskia ndio hivo hivyo...
 
Afisa wa Ikulu aliyetajwa ni yule aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo LA eapot, na wakati anauawa alikuwa na lumbesa LA Fedha ndani ya gari, kwahiyo ikulu itajiosha kuwa bwana Mbena hakutumwa na ikulu, yetu macho
 
Lini Mkuu hayoo mambo yametokea? Ni zamani?
 
Hizo Billion 306 za akaunti ipi maana ripoti ya CAG kuhusu akaunti ya escrow inaonesha kulikuwa na billioni 182 tu.

Jisomee: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-pac-wachukuliwe-hatua-kali-za-kisheria.html
 
It is really shame to have Jakaya Kikwete as a president.

Kikwete ni mwizi na hana uchungu na hii nchi.
 
Afisa wa Ikulu aliyetajwa ni yule aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo LA eapot, na wakati anauawa alikuwa na lumbesa LA Fedha ndani ya gari, kwahiyo ikulu itajiosha kuwa bwana Mbena hakutumwa na ikulu, yetu macho

Fafanua kidogo mkuu
 
Lini Mkuu hayoo mambo yametokea? Ni zamani?

~~~~~~~~
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru Alias Mbena ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?

~~~~~~~
 
Afisa wa Ikulu aliyetajwa ni yule aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo LA eapot, na wakati anauawa alikuwa na lumbesa LA Fedha ndani ya gari, kwahiyo ikulu itajiosha kuwa bwana Mbena hakutumwa na ikulu, yetu macho

HUNIJUI 04:17 30th April 2014
Watu waliokuwa wanatumia pikipiki wamempiga
risasi mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari na
kumpora begi na kisha kutokomea na pikipiki yao.
Mtu huyo amepigwa risasi na kufariki papo hapo.
 
Kafulila kaibua hili swala la Escrow march na mtu wa ikulu kauawa April (ndio aliyotoa go ahead),wakubwa wakaona issue ishabumburuka cha kufanya ni kumtoa kafala mbena aliyehidhinisha kwa niaba ya ikulu,marehemu haongei kwisha kazi tena.
 
Aisee...! Sasa naanza kuona ingawa macho bado yana ukungu...!
 
Inatisha!
Mimi tangu alipompaka tope Dr Salim Salim pale anagombea kupendekezwa na CCM, sikuwa na imani na maadili ya huyu jamaa.
Huyu anaweza kufanya chochote ili mradi afikie lengo lae. Ogopa mtu namna hiyo.
Kwa ongezo hili la kuuawa kwa Mbena, picha inatimia kabisa. Kila Mtanzania anayejihusisha na siasa achunge maisha yake.
 
Nadhani mzee kikwete angekuwa anapita hii site ya jukwaa la siasa huku JF nadhani angebadili style yake ya kuongoza...nafikil atakuwa anasoma sana magazeti ya bwana mmoja msukuma
 
Sisi watanzania tulimchagua Kikwete kuwa kiongozi wetu lakini cha ajabu ametusaliti.

Pole sana, mimj ni mtizedi, na nilimsikiliza kwenye mdahalo wake uliofanyika Serena kipindi kile cha kampeni za urais. Yaani Pamoja na yeye kupewa majibu na kuulizwa leading questions na wakina masako. still Alikuwa too low. Nisingeweza kumpa Kura yangu. Frankly.,
Dr. Slaa alimfunika sana.
Nashkuru mamilion ya watized waliliona ndio maana hawakumpa kura.
Uwe unasikiliza Sera kabla ya kiamua kupiga Kura.
Usituangushe 2015.
 
Back
Top Bottom