Ikulu: Rais Kikwete akutana na viongozi wa vyama vya upinzani

Status
Not open for further replies.

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Ndugu wana JF , itakumbukwa kwamba leo ndiyo siku ambayo Muungano wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-MAGEUZI wanakwenda kukutana na Rais kumshinikiza asisaini mswada wa mabadiliko ya Katiba.

Waraka ambao umebeba hoja zao huu hapa:
WARAKA WA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI
KWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE
JUU YA
SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2013

Mheshimiwa Rais, Sisi Wenyeviti wa Taifa wa vyama vitatu, yaani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR-Mageuzi, tunakuandikia, kwa niaba ya vyama vyetu, kukushauri kutumia mamlaka yako chini ya ibara ya 97(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kukataa kuukubali Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 6 Septemba, 2013. Sheria hiyo sasa inasubiri ridhaa yako kabla ya kuanza kutumika. Ushauri wetu unatokana na imani yetu kwamba endapo Muswada huu utapata ridhaa yako na kuanza kutumika kama Sheria utakuwa na madhara makubwa kwa mchakato mzima wa utungaji wa Katiba Mpya, na kwa amani na utulivu wa nchi yetu kwa sababu zifuatazo.

1. USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA WANANCHI

Mheshimiwa Rais,
Tarehe 28 Julai, 2013, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Katiba, Sheria na Utawala ilianza vikao vyake vya kawaida kwa ajili ya kuchambua na kupokea maoni ya wadau mbali mbali juu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Katika kikao cha siku hiyo cha Kamati, katika wadau wa kitaasisi na binafsi wapatao 44 waliokuwa wamealikwa na Kamati ili kuwasilisha maoni yao juu ya Muswada huo, hakukuwa na mdau wa kitaasisi au binafsi hata mmoja aliyealikwa kutoka Zanzibar.

Aidha, ratiba ya shughuli za Kamati iliyokuwa imeandaliwa na Ofisi ya Katibu wa Bunge ilikuwa inaonyesha kwamba Kamati ingetembelea Zanzibar kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kutembelea miradi ya TASAF, Ofisi Ndogo ya Makamu wa Rais Zanzibar na Ofisi Ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano iliyoko Zanzibar.
Kutokana na kutokuwepo kwa wadau wa Zanzibar katika ratiba ya Kamati ya kupokea maoni ya wadau, na kwa sababu ya kuwepo kwa safari ya Zanzibar katika ratiba ya Kamati, Kamati ilipendekeza kwamba badala ya kwenda Zanzibar kutembelea miradi na Ofisi tajwa, Kamati iende Zanzibar kwa ajili ya kukusanya maoni ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu.

Aidha, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi ambao Kamati ingependa kupata maoni yao juu ya Muswada huu.
Taasisi hizo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (State University of Zanzibar – SUZA), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Tunguu, Chama cha Mawakili Zanzibar (Zanzibar Law Society – ZLS) na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zanzibar Female Lawyers' Association – ZAFELA). Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA), Shirikisho la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Zanzibar (Association of Non-Governmental Organizations of Zanzibar – ANGOZA) na Jumuiya ya Misikiti Zanzibar. Kwa watu binafsi, Kamati ilipendekeza kuonana na Profesa Abdul Sheriff, msomi maarufu wa historia kutoka Zanzibar. Hata hivyo, kwa sababu ambazo hazijawahi kutajwa wazi na rasmi na uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Kamati ilizuiliwa kwenda Zanzibar kukusanya maoni ya wadau hao. Huu ndio ulikuwa msingi wa hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba "... wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar."

Mheshimiwa Rais,

Suala la kukusanya na kusikiliza maoni ya wadau katika mchakato wa kutunga sheria ni jambo la lazima kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2013. Kanuni ya 84(2) ya Kanuni hizo inatamka wazi kwamba "Kamati iliyopelekewa Muswada itatoa matangazo au itatoa barua ya mwaliko kumwalika mtu yeyote afike kutoa maoni yake mbele ya Kamati hiyo kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo." Pamoja na ukweli kwamba Kamati ilialika wadau mbali mbali kufika mbele yake na kutoa maoni yao juu ya Muswada, hakuna taasisi wala mtu binafsi hata mmoja kutoka Zanzibar aliyealikwa na kufika mbele ya Kamati ili kutoa maoni yake. Kwa maana hiyo, hakukuwa na ushiriki wowote wa wadau kutoka Zanzibar. Suala la ushirikishwaji wa wadau wa Zanzibar katika Muswada huu sio jambo geni. Hii ni kwa sababu wakati Sheria mama inatungwa mwaka 2011, hoja ya aina hii hii ilitolewa Bungeni. Hoja hiyo ilipelekea mjadala wa Sheria hiyo kuahirishwa na Kamati kuelekezwa kwenda kufanya vikao na wadau wa Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma na ilifanya hivyo. Kwa hiyo, kwa vile Kamati ilikwenda Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau wakati huo, ilipaswa kwenda tena Zanzibar kusikiliza maoni ya Wazanzibari kuhusu marekebisho yaliyoletwa na Muswada huu. Hili halikufanyika.

2. USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mheshimiwa Rais,
Kuna ubishani mkubwa kuhusu kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mchakato wa kupitishwa kwa Muswada huu. Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano imetangaza hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu katika hatua zote za kupitishwa kwa Muswada, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenyewe imetoa kauli zenye utata mkubwa kuhusu suala hili.

Kwa mfano, wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amedai hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakari amesema hadharani kwamba ushirikishwaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ulihusu vifungu vinne tu vya Muswada huu.
Vifungu vingine vyote vya Muswada vilivyopitishwa na Bunge havikupelekwa Zanzibar na kwa hiyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa kwenye kupitishwa kwenye vifungu hivyo vingine.

Aidha, kwa barua yake yenye kumbu kumbu Na. OMPR/WKS/TS.7/1/62 ya tarehe 13 Septemba, 2013, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemwandikia Waziri Mkuu akimweleza kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa kikamilifu katika kupitishwa kwa Muswada huu. Hii ni licha ya Makamu wa Pili wa Rais kutangaza hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa. Kwa vyovyote vile, suala hili lina ubishani mkubwa ambao utatuzi wake unahitaji Muswada kurudishwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa upya. Endapo hili halitafanyika kama tunavyopendekeza, kuna uwezekano mkubwa kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kukataa kuridhia Muswada huu na hivyo kufanya utekelezaji wake kushindikana na mchakato wote wa Katiba Mpya kukwamishwa.

3.
BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mheshimiwa Rais,
Muswada uliopitishwa na Bunge umefanya mabadiliko makubwa kuhusu utaratibu wa kuunda Bunge Maalum la Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Marekebisho haya, Rais sasa atakuwa na mamlaka kisheria ya kuteua wajumbe 166 wa Bunge Maalum wasiokuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Pili, sio lazima tena kwamba wajumbe hao 166 watokane na makundi yaliyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hii ni kwa sababu, kwa marekebisho yaliyopitishwa na Bunge, Rais atapelekewa majina tisa kutoka katika kila taasisi iliyotajwa kwenye kifungu cha 22(1)(c) ili afanye uteuzi. "... Lakini kwenye uteuzi (huo)... (ni mtu) mmoja ndiye atakayefikiriwa kwenye uteuzi na si lazima apate." Haya ni maneno ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Angela Kairuki kama alivyonukuliwa kwenye Taarifa Rasmi ya Majadiliano Bungeni (Hansard) ya tarehe 6 Septemba, 2013. Na hivyo ndivyo kifungu kipya cha 22(1)(c) kinavyosomeka baada ya marekebisho ya Muswada huu!
Mabadiliko haya hayakuwepo kwenye Muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi Mei mwaka huu, na wala hayakutolewa maoni na wadau walioalikwa mbele ya Kamati.

Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikujulishwa juu ya marekebisho haya na wala haikuyatolewa maoni na msimamo wake.
Tatu, bado suala la makundi haya yaliyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) ni akina nani hasa linabaki bila majibu. Bado suala la kila moja ya makundi haya litawakilishwa na wajumbe wangapi katika Bunge Maalum linabaki bila majibu. Kukosekana kwa majibu ya maswali haya kunatoa mwanya kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum ambao hawawakilishi makundi ya kijamii yanayohitaji kuwakilishwa katika hatua hii muhimu ya kutunga Katiba Mpya kwa ajili ya nchi yetu. Aidha, kutokuwepo kwa majibu ya masuala haya kunatoa mwanya kwa mamlaka ya uteuzi, yaani Rais, kufanya uteuzi wa wajumbe watakaounga mkono matakwa ya mamlaka ya uteuzi au ya chama chake cha siasa juu ya Katiba Mpya.

4.
IDADI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Rais,
Kwa muundo wa Bunge Maalum la Katiba kama ulivyo kwa sasa chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge hilo litakuwa na jumla ya wajumbe 604, yaani, Wabunge 357, Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 81 na wajumbe wengine 166 waliotajwa chini ya kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria. Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Wawakilishi wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar peke yao watakuwa 438 au asilimia 72.5 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Wajumbe waliobaki na ambao wanatakiwa kuteuliwa na Rais ni 166 au asilimia 27.5 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Muundo huu unahakikisha kwamba Bunge Maalum la Katiba litatawaliwa na wawakilishi wa vyama vya siasa. Hii ni kwa sababu sifa kuu pekee ya mtu kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge au Mwakilishi Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.

Aidha, kwa muundo wa sasa wa Bunge pamoja na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, vyama vyenye uwakilishi katika mabunge haya ni sita tu. Vitatu kati ya vyama hivyo vina idadi ya Wabunge na Wawakilishi wasiofikia kumi. Katika vyama vitatu vilivyobaki, Chama cha Mapinduzi pekee kitakuwa na wajumbe 338 au asilimia 77 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotokana na Bunge na Baraza la Wawakilishi.
Ushawishi wa vyama vya siasa haushii hapo peke yake. Kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria kinalazimu kwamba katika wajumbe 166 watakaoteuliwa na Rais, kutakuwa pia na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu. Hii ina maana kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba watakaotokana na vyama vya siasa itakuwa kubwa kuliko zaidi asilimia 72.5 ya sasa. Hali hii isiporekebishwa itakuwa na maana kwamba Katiba Mpya itatokana na matakwa ya vyama vya siasa ambavyo idadi ya jumla ya wanachama wao haifiki milioni kumi kati ya Watanzania zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Kwa sababu hiyo, wadau karibu wote waliotoa maoni yao kuhusu Muswada huu mbele ya Kamati walipendekeza idadi ya wajumbe wasiokuwa Wabunge ama Wawakilishi iongezwe hadi kufikia theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum, au idadi ya Wabunge na Wawakilishi ipunguzwe hadi kufikia theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.
Kwa maoni yetu, kutokana na sababu mbali mbali, hakuna uwezekano wa kupunguza idadi ya wajumbe wanaotokana na Bunge au Baraza la Wawakilishi. Kwa maana hiyo, njia pekee ya kupunguza ushawishi wa vyama vya siasa kwenye Bunge Maalum ni kuongeza idadi ya wajumbe wasiotokana na Bunge na Baraza na vile vile wasiotokana na vyama vya siasa vilivyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria hadi kufikia walau idadi sawa na wajumbe wanaotokana na Bunge na Baraza la Wawakilishi. Hatua hii itafikisha idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum kuwa 876. Kwa kulinganisha na uzoefu wa nchi nyingine zilizopitia hatua hii ya kutengeneza Katiba Mpya kwa utaratibu huu, idadi hii sio kubwa sana kwa kulingana na mazingira halisi ya nchi yetu.

5.
UWAKILISHI WA ZANZIBAR KATIKA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Rais,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaliwa kwa kuunganisha nchi mbili zilizokuwa huru na zenye hadhi na haki sawa, licha ya tofauti zao za ukubwa wa eneo au idadi ya watu wake. Katiba Mpya ambayo mchakato wake umeleta mgogoro wa sasa inatakiwa kuakisi haki na hadhi sawa kati ya nchi hizi mbili. Kama ambavyo mtaalamu mmoja wa masuala ya sheria na Katiba na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambavyo amesema kuhusu mchakato wetu wa Katiba Mpya, "katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa." Hata hivyo, Mheshimiwa Rais, dhana hii ya haki na hadhi sawa kati ya Washirika wa Muungano haijazingatiwa wakati wa kupitishwa kwa Muswada huu. Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalum watakaotokana na wajumbe 166 walioainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) "... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao." Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55.

Kwa sasa Wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76.
Kwa ujumla, kwa hiyo, ili kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1) na (2) cha Sheria, Zanzibar itakuwa na wajumbe 214 katika Bunge Maalum, ambayo ni sawa na takriban 35% ya wajumbe wote. Dhana ya haki na hadhi sawa ilikubalika na kutekelezwa wakati wa kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Dhana hii inapaswa pia kukubalika na kutekelezwa wakati wa kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba.
Sisi tunaamini kwamba hoja ya usawa wa idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ina nguvu zaidi kuhusu Bunge Maalum kuliko ilivyokuwa kwa Tume. Hii ni kwa sababu, ni Bunge Maalum ndilo litakalokuwa na mamlaka ya kuijadili na kuipitisha Katiba Mpya kabla ya kupelekwa kwenye kura ya maoni ya wananchi. Upande wenye wajumbe wengi utakuwa na nafasi nyingi zaidi za kuzungumza kuliko upande wenye wajumbe wachache. Hii ina maana kwamba hoja za upande huo ndio zitakazosikika zaidi kuliko hoja za upande mwingine. Vinginevyo labda kuwe na masharti ya sheria yatakayolazimu kila upande wa Jamhuri ya Muungano uwe na fursa sawa za kuchangia katika mijadala ya Bunge Maalum.

Na kama itakuwa hivyo, kutakuwa na hoja halali kwamba wajumbe ambao hawatapata nafasi ya kuchangia wanaenda kufanya nini katika Bunge Maalum!
Kwa sababu hizi, tunapendekeza kwamba ‘hadhi na haki sawa' baina ya Washirika wa Muungano iliyotumika wakati wa kuunda Tume itumike vile vile katika kuunda Bunge Maalum la Katiba. Kwa maana hiyo tunapendekeza kwamba idadi ya wawakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum iongezwe hadi kufikia nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Hili linawezekana kwa namna mbili. Kwanza, kwa kuongeza idadi ya wajumbe waliotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) kama tulivyopendekeza.

Na pili, kwa kurekebisha kifungu cha 22(2) ili kisomeke kwamba idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar ‘haitapungua asilimia sitini na nne ya wajumbe hao.'
Kama pendekezo hili litakubaliwa, wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar wataongezeka kutoka 214 kwa mujibu wa Sheria ilivyo sasa, hadi 438, wakati idadi ya wajumbe wa kutoka Tanganyika nao watakuwa 438. Muhimu zaidi, Bunge Maalum litakuwa limetimiza matakwa ya usawa wa haki na hadhi kati ya Washirika hawa wa Muungano.

6. UTARATIBU WA KUPITISHA KATIBA MPYA KWENYE BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Rais,
Muswada huu umefanya marekebisho makubwa katika namna ya kupitisha vifungu vya Katiba Mpya katika Bunge Maalum la Katiba. Wakati kifungu cha 26(2) cha Sheria kama ilivyo sasa kinalazimu kwamba ili Katiba Mpya ipitishwe sharti ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wote wa kutoka Tanganyika na idadi hiyo hiyo ya wajumbe kutoka Zanzibar, marekebisho yaliyofanywa kwenye Muswada huu yameondoa sharti hilo.

Hii ni kwa sababu, kwa marekebisho haya, endapo theluthi mbili haitapatikana ndani ya Bunge Maalum la Katiba baada ya kupiga kura mara mbili, basi Katiba Mpya itapitishwa kwa wingi wa kawaida wa wajumbe wote wa Tanganyika na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wa kutoka Zanzibar.
Marekebisho haya yataleta matatizo katika upitishaji wa Katiba Mpya kwa sababu yanaondoa haja ya kupata muafaka na maridhiano katika kupatikana kwa Katiba Mpya. Hii ni kwa sababu upande wenye wajumbe wengi lakini ambao idadi yao haijafika theluthi mbili unaweza kuzuia jambo usilolitaka kwenye Katiba Mpya lisipite kwa kulinyima theluthi mbili ya kura na hivyo kulazimisha lipitishwe kwa kura ya wingi wa kawaida.

Kwa upande mwingine, kifungu cha 26(2) kama kilivyokuwa kabla ya marekebisho kinalazimisha muafaka na maridhiano na kinahakikisha kwamba Katiba Mpya itapita kwa kuungwa mkono na wajumbe wengi zaidi katika Bunge Maalum la Katiba. Katiba iliyopitishwa kwa muafaka na maridhiano ina nafasi kubwa zaidi ya kuheshimiwa na wadau wote kuliko Katiba iliyopitishwa kwa kura ya wingi wa kawaida. Katika kifungu hiki pia, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa na wala haikukitolea maoni na msimamo wake.

Aidha, wadau wa Tanganyika nao hawakushirikishwa kukitolea maoni kwa vile hakikuwepo kabisa katika Muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni na ambao ulipelekwa kwa wadau.

7.
UKOMO WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mheshimiwa Rais,
Kwa mujibu wa Sheria kama ilivyo sasa, Tume inatakiwa kukamilisha majukumu yake ya kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya na kuwasilisha ripoti kwa Rais mwezi Desemba ya mwaka huu. Baada ya kukamilisha majukumu hayo, Tume imekabidhiwa jukumu la kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge Maalum la Katiba na kutoa ufafanuzi utakaohitajika kwenye Bunge Maalum.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 33(2) cha Sheria, Tume imekabidhiwa majukumu ya kuendesha elimu kwa wapiga kura juu ya Katiba Mpya wakati wa mchakato wa uhalalishaji wa Katiba Mpya kwa kupitia kura ya maoni ya wananchi.
Katika kutekeleza majukumu haya ya baada ya kuwasilisha Rasimu na ripoti yake, Bunge lilipitisha jumla ya shilingi za Tanzania bilioni 2.362 kwa ajili ya posho mbali mbali za wajumbe wa Tume na Sekretarieti yake, pamoja na gharama nyinginezo wakati wa Bunge Maalum la Katiba. Kwa mujibu wa Sheria kama ilivyo sasa, ukomo wa Tume utakuwa pale ambapo Katiba Mpya itakuwa imepitishwa katika kura ya maoni ya wananchi. Sasa Muswada huu umefanya marekebisho makubwa kwa majukumu ya Tume na, kwa hiyo, ukomo wake. Kwa mujibu wa marekebisho haya, Tume itavunjwa mara baada ya kuwasilisha ripoti yake na Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Aidha, jukumu la kutoa ufafanuzi juu ya Katiba Mpya sasa litafanywa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au mjumbe mwingine yeyote wa Tume atakayealikwa kwa ajili hiyo na Katibu wa Bunge Maalum baada ya mashauriano na Mwenyekiti wa Bunge hilo. Na licha ya Bunge kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili hiyo, kazi ya Tume ya kufanya uhamasishaji na kutoa elimu kwa wapiga kura wakati wa kura ya maoni sasa imeachwa bila mwenyewe! Vifungu hivi pia havikuwepo katika Muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi Mei, na wala havikupelekwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wala kwa wadau wa Tanganyika kwa ajili ya maoni yao licha ya umuhimu wake.


Mheshimiwa Rais,
Katika kutekeleza majukumu yake, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imepata uzoefu mkubwa sana wa masuala muhimu ya kikatiba yanayoikabili nchi yetu. Rasimu ya Katiba Mpya ya Tume inatokana na uzoefu huo. Badala ya kuupoteza utajiri huo kwa kuivunja Tume kama inavyopendekezwa na Muswada huu, sisi tunapendekeza sio tu kwamba Tume iendelee kuwepo hadi Katiba Mpya itakapopatikana, bali pia ifanywe kuwa sehemu rasmi ya Sekretarieti ya Bunge Maalum. Hii itafanya Tume iwepo wakati wote wa mijadala ya Bunge Maalum kama sehemu ya kiutendaji ya Bunge hilo. Vile vile, badala ya kusubiri kuitwa kutoa ufafanuzi pale itakapohitajika kama ilivyo katika Sheria ya sasa, pendekezo hili litaifanya Tume itoe ufafanuzi na msaada kwa Bunge Maalum wakati wote wa mijadala ya Bunge hilo.

8.
KUINGIZWA KWA MAMBO AMBAYO HAYAKUJADILIWA WALA KUPITISHWA NA BUNGE

Mheshimiwa Rais,
Kuna jambo moja ambalo limetufadhaisha na kutusikitisha sana kuhusiana na Muswada huu. Katika mojawapo ya majedwali ya marekebisho ya Muswada yaliyopelekwa kwenye Kamati na baadaye Bungeni na Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Matthew M. Chikawe, kulikuwa na mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 22 ili kuweka utaratibu wa kuchagua Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ndiye atakayesimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo na kupitishwa kwa Kanuni zake. Mbele ya Kamati, Waziri Chikawe alipeleka Jedwali la Marekebisho lililoandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambalo lilipendekeza kuingizwa kwa kifungu kipya cha 22A kitakachompa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mamlaka ya kusimamia mchakato wa kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum.

Licha ya kuwa pendekezo hili lilikuwa jipya na halikuwepo kwenye Muswada uliotolewa maoni na wadau na uliopelekwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya maoni yake, pendekezo hili liliafikiwa na wajumbe wa Kamati.
Hata hivyo, ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati Bunge likiwa limeketi kama Kamati ya Bunge Zima kwa ajili ya kupitisha kifungu kwa kifungu, Waziri Chikawe aliwasilisha Jedwali lingine la Marekebisho lililoandikwa kwa lugha ya Kiswahili kuhusu kifungu hicho hicho cha 22A. Jedwali hili linasomeka kama ifuatavyo: "... Baada ya kuitishwa kwa Bunge Maalum, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Mapinduzi watasimamia mchakato wa kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum...." Majedwali haya mawili yanayotofautiana yaliingizwa Bungeni ili yajadiliwe na, kama yangekubalika, kupitishwa.

Hata hivyo, kwa ushahidi wa Taarifa Rasmi ya Majadiliano Bungeni (hansard) ya tarehe 6 Septemba, 2013, mapendekezo haya yanayotofautiana hayakujadiliwa wala kupitishwa na Bunge. Licha ya mapendekezo haya ya Serikali kutokujadiliwa wala kupitishwa, sasa yameingizwa kinyemela katika Muswada huu kana kwamba yalijadiliwa na kupitishwa na Bunge. Hivyo basi, kwa mujibu wa nakala ya Muswada wa Sheria hii ambayo tumefanikiwa kuipata, sasa kuna kifungu kipya cha 22A chenye vifungu vidogo viwili. Kwa mujibu wa kifungu hicho, sasa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ndio watakaosimamia mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum!
Marekebisho haya ya kifungu cha 22A cha Sheria yametushtua na kutufadhaisha sana sio tu kwa sababu yanamwingiza Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kwenye mchakato wa Katiba na hivyo kwenda kinyume na utaratibu mzima ulioko kwenye Sheria mama unaomtambua Katibu wa Baraza la Wawakilishi, bali pia umeonyesha jinsi ambavyo mambo ambayo hayakuwemo hata kwenye mjadala na hayakufanyiwa maamuzi na Bunge yameingizwa kinyemela kwenye Muswada unaoombwa kuusaini ili uwe Sheria ya nchi yetu!

Endapo utakubali kuusaini Muswada huu na kuwa Sheria utakuwa umebariki udanganyifu huu kwa taifa. Tunakuomba usiingie katika aibu na fedheha hii ya kubariki jambo ambalo halijajadiliwa wala kupitishwa na Bunge kuwa Sheria.

9. HITIMISHO

Mheshimiwa Rais,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekupa wewe kama Rais wetu mamlaka ya kuridhia Muswada uliopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa sheria. Bila shaka Katiba imekupa mamlaka haya kwa kufahamu kwamba Bunge hupitisha miswada ya sheria baada ya kuitafakari kwa kina na kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi yetu. Katiba yetu imekupa pia mamlaka ya kukataa kuridhia Muswada uliopitishwa na Bunge endapo, katika busara zako, utaona kwamba Muswada huo haukufanyiwa tafakuri ya kutosha na pengine haujazingatia maslahi mapana ya nchi yetu. Hatuna shaka vile vile kwamba mamlaka haya ya kukataa kuukubali Muswada wa aina hiyo yaliwekwa kwa kufahamu kwamba sio mara zote Bunge linazingatia maslahi mapana ya nchi ama kufanya tafakuri ya kutosha juu ya Muswada husika.

Kama tulivyoonyesha katika maelezo yetu, Muswada huu ni mojawapo ya Muswada wa aina ya pili, yaani, Muswada ambao haukufanyiwa tafakuri ya kutosha na wala haujazingatia maslahi mapana ya kupata Katiba Mpya ya nchi yetu kwa njia ya muafaka wa kitaifa na maridhiano ya wadau wote. Muswada huu hautajenga maelewano kuhusu namna ya kutatua matatizo ya Muungano wetu, wala hautaziba nyufa kubwa zilizojengwa katika mchakato huu. Badala ya kutuunganisha, Muswada huu utatugawa zaidi. Badala ya kutibu majeraha yetu ya kisiasa na kijamii, Muswada huu utayawekea chumvi na kuyafanya yawe makubwa zaidi.
Kwa ajili hiyo, tunakuomba utumie mamlaka yako kama Rais na Mkuu wa Nchi yetu chini ya ibara ya 97(2) ya Katiba, ukatae kuukubali Muswada huu na badala yake uelekeze urudishwe Bungeni kwa sababu ambazo tumezieleza katika maelezo yetu haya.

Tunaomba kuwasilisha,

----------------------------------------------------------------
Mh. Freeman A. Mbowe (MB)
MWENYEKITI TAIFA
CHADEMA
-----------------------------------------------------------
Prof. Ibrahim H. Lipumba
MWENYEKITI TAIFA
CUF
----------------------------------------------------
Mh. James F. Mbatia (MB)
MWENYEKITI TAIFA
NCCR-MAGEUZI

Karibuni kwenye mjadala wenye rutuba kwa mstakabali wa Taifa letu.
 
Kwa kuwa chama changu JAHAZI ASILIA akikupewa nafasi sitochangia chochote kwanza hiyo katiba isogezwe mbele mpaka 2020
 
Ndugu wana JF , itakumbukwa kwamba leo ndiyo siku ambayo Muungano wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-MAGEUZI wanakwenda kukutana na Rais kumshinikiza asisaini mswada wa mabadiliko ya Katiba.

Waraka ambao umebeba hoja zao huu hapa:

Kama kweli ni huu kuna maeneo kibao tungewashauri.Umechelewa kuletwa.Kwa sababu tayari wanaenda nao waende nao hatuna cha kuwashauri.Tutatoa ushauri wetu na sisi kwa Raisi baada ya wao kutoka kunywa chai na kupiga picha wakiwa wamekenua meno ikulu.
 
Hoja nzito sana hizo. Naweza kuona "mikono" ya Mh. Tundu Lissu na Prof. Abdallah Safari kwenye hizo hoja.
 
Rais ajipe muda wa kusoma mambo ya muhimu badala ya kusubiri kuambiwa, itapunguza sana utata...
 
haya yote yangefaa kujadiliwa bungeni sio ikulu. wapinzani wamefanya kosa kubwa kususia vikao vya bunge wakati linajadili mswada huu.

Rais ajipe muda wa kusoma mambo ya muhimu badala ya kusubiri kuambiwa, itapunguza sana utata...

wapinzani walishindwa nn kujadili mambo haya bungeni?? au wanatuona watz ni wajinga kwa kula kodi zetu ovyo

rais kikwete ni mtu muungwana sana. wape hao jamaa juice na kahawa
 
Kwa nini wanausambaza kabla hawajamuona rais, au hapa pia wanataka huruma yetu?
 
rais kikwete ni mtu muungwana sana. wape hao jamaa juice na kahawa

Na kweli hawa wanakwenda kunya chai, mbona walichokiandika hakina tofauti na walichokikataa bungeni.

Hoja nzito sana hizo. Naweza kuona "mikono" ya Mh. Tundu Lissu na Prof. Abdallah Safari kwenye hizo hoja.

Nimegundua wewe ndo wale wale wanachangia mada humu bila hata kusoma, umesoma saa ngapi kurasa zote hizi na kuona ni nzito? kwa uzito wa hoja unaupima kwa wingi wa kurasa? mbona sioni jipya humu?

Rais ajipe muda wa kusoma mambo ya muhimu badala ya kusubiri kuambiwa, itapunguza sana utata...
Utumbo ulioandikwa humu hata asiposoma ni sawa tu.
 
Ni jambo zuri na shukrani nyingi kwa Mh Rais wetu JK kwa kuona Umuhimu wa kukutana na Hawa wenye viti.
Mh Rais ameonesha nia ya dhati na nzuri kwa Taifa letu na Pia Hawa Waheshimiwa viongozi wameonesha nia nzuri na dhati kwa kusitisha maandamano!
Hizi ndio siasa Safi kwa mustakabri wa taifa letu!

Sio zile siasa za kusema hakuna tena nafasi ya wapinzani kwenda Ikulu kunywa Chai na Juice!
Rais ni wetu sote Watanzania na ni wetu sote vyama vyote na Ikulu ni makao ya Rais wetu wote Watz.
 
Ingawa napenda muswada huu kutazamwa upya kwa mustakabali wa Tanganyika... sikubaliani na hoja ya muungano inavyobanwa banwa.. watu wanatakiwa wapige kura za kuukataa au kuukubali muungano huu... kwangu mm muungano ulitakiwa kuvunjwa Jana na sio Kesho...
 
1383934_547444032009065_1619949742_n.jpg


baada ya juice , baadhi ya mambo yanayojadiliwa ni haya

1. USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA WANANCHI

Mheshimiwa Rais,

Tarehe 28 Julai, 2013, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Katiba, Sheria na Utawala ilianza vikao vyake vya kawaida kwa ajili ya kuchambua na kupokea maoni ya wadau mbali mbali juu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Katika kikao cha siku hiyo cha Kamati, katika wadau wa kitaasisi na binafsi wapatao 44 waliokuwa wamealikwa na Kamati ili kuwasilisha maoni yao juu ya Muswada huo, hakukuwa na mdau wa kitaasisi au binafsi hata mmoja aliyealikwa kutoka Zanzibar. Aidha, ratiba ya shughuli za Kamati iliyokuwa imeandaliwa na Ofisi ya Katibu wa Bunge ilikuwa inaonyesha kwamba Kamati ingetembelea Zanzibar kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kutembelea miradi ya TASAF, Ofisi Ndogo ya Makamu wa Rais Zanzibar na Ofisi Ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano iliyoko Zanzibar.

Kutokana na kutokuwepo kwa wadau wa Zanzibar katika ratiba ya Kamati ya kupokea maoni ya wadau, na kwa sababu ya kuwepo kwa safari ya Zanzibar katika ratiba ya Kamati, Kamati ilipendekeza kwamba badala ya kwenda Zanzibar kutembelea miradi na Ofisi tajwa, Kamati iende Zanzibar kwa ajili ya kukusanya maoni ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu. Aidha, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi ambao Kamati ingependa kupata maoni yao juu ya Muswada huu.

Taasisi hizo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (State University of Zanzibar – SUZA), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Tunguu, Chama cha Mawakili Zanzibar (Zanzibar Law Society – ZLS) na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zanzibar Female Lawyers' Association – ZAFELA). Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA), Shirikisho la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Zanzibar (Association of Non-Governmental Organizations of Zanzibar – ANGOZA) na Jumuiya ya Misikiti Zanzibar. Kwa watu binafsi, Kamati ilipendekeza kuonana na Profesa Abdul Sheriff, msomi maarufu wa historia kutoka Zanzibar.

Hata hivyo, kwa sababu ambazo hazijawahi kutajwa wazi na rasmi na uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Kamati ilizuiliwa kwenda Zanzibar kukusanya maoni ya wadau hao. Huu ndio ulikuwa msingi wa hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba "... wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar."

Mheshimiwa Rais,

Suala la kukusanya na kusikiliza maoni ya wadau katika mchakato wa kutunga sheria ni jambo la lazima kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2013. Kanuni ya 84(2) ya Kanuni hizo inatamka wazi kwamba "Kamati iliyopelekewa Muswada itatoa matangazo au itatoa barua ya mwaliko kumwalika mtu yeyote afike kutoa maoni yake mbele ya Kamati hiyo kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo." Pamoja na ukweli kwamba Kamati ilialika wadau mbali mbali kufika mbele yake na kutoa maoni yao juu ya Muswada, hakuna taasisi wala mtu binafsi hata mmoja kutoka Zanzibar aliyealikwa na kufika mbele ya Kamati ili kutoa maoni yake. Kwa maana hiyo, hakukuwa na ushiriki wowote wa wadau kutoka Zanzibar.

Suala la ushirikishwaji wa wadau wa Zanzibar katika Muswada huu sio jambo geni. Hii ni kwa sababu wakati Sheria mama inatungwa mwaka 2011, hoja ya aina hii hii ilitolewa Bungeni. Hoja hiyo ilipelekea mjadala wa Sheria hiyo kuahirishwa na Kamati kuelekezwa kwenda kufanya vikao na wadau wa Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma na ilifanya hivyo. Kwa hiyo, kwa vile Kamati ilikwenda Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau wakati huo, ilipaswa kwenda tena Zanzibar kusikiliza maoni ya Wazanzibari kuhusu marekebisho yaliyoletwa na Muswada huu. Hili halikufanyika.

2. USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mheshimiwa Rais,

Kuna ubishani mkubwa kuhusu kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mchakato wa kupitishwa kwa Muswada huu. Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano imetangaza hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu katika hatua zote za kupitishwa kwa Muswada, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenyewe imetoa kauli zenye utata mkubwa kuhusu suala hili. Kwa mfano, wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amedai hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakari amesema hadharani kwamba ushirikishwaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ulihusu vifungu vinne tu vya Muswada huu.

Vifungu vingine vyote vya Muswada vilivyopitishwa na Bunge havikupelekwa Zanzibar na kwa hiyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa kwenye kupitishwa kwenye vifungu hivyo vingine. Aidha, kwa barua yake yenye kumbu kumbu Na. OMPR/WKS/TS.7/1/62 ya tarehe 13 Septemba, 2013, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemwandikia Waziri Mkuu akimweleza kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa kikamilifu katika kupitishwa kwa Muswada huu. Hii ni licha ya Makamu wa Pili wa Rais kutangaza hadharani kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa. Kwa vyovyote vile, suala hili lina ubishani mkubwa ambao utatuzi wake unahitaji Muswada kurudishwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa upya. Endapo hili halitafanyika kama tunavyopendekeza, kuna uwezekano mkubwa kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kukataa kuridhia Muswada huu na hivyo kufanya utekelezaji wake kushindikana na mchakato wote wa Katiba Mpya kukwamishwa.

3. BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mheshimiwa Rais,

Muswada uliopitishwa na Bunge umefanya mabadiliko makubwa kuhusu utaratibu wa kuunda Bunge Maalum la Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Marekebisho haya, Rais sasa atakuwa na mamlaka kisheria ya kuteua wajumbe 166 wa Bunge Maalum wasiokuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Pili, sio lazima tena kwamba wajumbe hao 166 watokane na makundi yaliyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hii ni kwa sababu, kwa marekebisho yaliyopitishwa na Bunge, Rais atapelekewa majina tisa kutoka katika kila taasisi iliyotajwa kwenye kifungu cha 22(1)(c) ili afanye uteuzi. "... Lakini kwenye uteuzi (huo)... (ni mtu) mmoja ndiye atakayefikiriwa kwenye uteuzi na si lazima apate." Haya ni maneno ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Angela Kairuki kama alivyonukuliwa kwenye Taarifa Rasmi ya Majadiliano Bungeni (Hansard) ya tarehe 6 Septemba, 2013. Na hivyo ndivyo kifungu kipya cha 22(1)(c) kinavyosomeka baada ya marekebisho ya Muswada huu!

Mabadiliko haya hayakuwepo kwenye Muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi Mei mwaka huu, na wala hayakutolewa maoni na wadau walioalikwa mbele ya Kamati. Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikujulishwa juu ya marekebisho haya na wala haikuyatolewa maoni na msimamo wake.

Tatu, bado suala la makundi haya yaliyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) ni akina nani hasa linabaki bila majibu. Bado suala la kila moja ya makundi haya litawakilishwa na wajumbe wangapi katika Bunge Maalum linabaki bila majibu. Kukosekana kwa majibu ya maswali haya kunatoa mwanya kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum ambao hawawakilishi makundi ya kijamii yanayohitaji kuwakilishwa katika hatua hii muhimu ya kutunga Katiba Mpya kwa ajili ya nchi yetu. Aidha, kutokuwepo kwa majibu ya masuala haya kunatoa mwanya kwa mamlaka ya uteuzi, yaani Rais, kufanya uteuzi wa wajumbe watakaounga mkono matakwa ya mamlaka ya uteuzi au ya chama chake cha siasa juu ya Katiba Mpya.

4. IDADI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Rais,

Kwa muundo wa Bunge Maalum la Katiba kama ulivyo kwa sasa chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge hilo litakuwa na jumla ya wajumbe 604, yaani, Wabunge 357, Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 81 na wajumbe wengine 166 waliotajwa chini ya kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria. Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Wawakilishi wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar peke yao watakuwa 438 au asilimia 72.5 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum. Wajumbe waliobaki na ambao wanatakiwa kuteuliwa na Rais ni 166 au asilimia 27.5 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.

Muundo huu unahakikisha kwamba Bunge Maalum la Katiba litatawaliwa na wawakilishi wa vyama vya siasa. Hii ni kwa sababu sifa kuu pekee ya mtu kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge au Mwakilishi Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.

Aidha, kwa muundo wa sasa wa Bunge pamoja na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, vyama vyenye uwakilishi katika mabunge haya ni sita tu. Vitatu kati ya vyama hivyo vina idadi ya Wabunge na Wawakilishi wasiofikia kumi. Katika vyama vitatu vilivyobaki, Chama cha Mapinduzi pekee kitakuwa na wajumbe 338 au asilimia 77 ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotokana na Bunge na Baraza la Wawakilishi.

Ushawishi wa vyama vya siasa haushii hapo peke yake. Kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria kinalazimu kwamba katika wajumbe 166 watakaoteuliwa na Rais, kutakuwa pia na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu. Hii ina maana kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba watakaotokana na vyama vya siasa itakuwa kubwa kuliko zaidi asilimia 72.5 ya sasa.

Hali hii isiporekebishwa itakuwa na maana kwamba Katiba Mpya itatokana na matakwa ya vyama vya siasa ambavyo idadi ya jumla ya wanachama wao haifiki milioni kumi kati ya Watanzania zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Kwa sababu hiyo, wadau karibu wote waliotoa maoni yao kuhusu Muswada huu mbele ya Kamati walipendekeza idadi ya wajumbe wasiokuwa Wabunge ama Wawakilishi iongezwe hadi kufikia theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum, au idadi ya Wabunge na Wawakilishi ipunguzwe hadi kufikia theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.

Kwa maoni yetu, kutokana na sababu mbali mbali, hakuna uwezekano wa kupunguza idadi ya wajumbe wanaotokana na Bunge au Baraza la Wawakilishi. Kwa maana hiyo, njia pekee ya kupunguza ushawishi wa vyama vya siasa kwenye Bunge Maalum ni kuongeza idadi ya wajumbe wasiotokana na Bunge na Baraza na vile vile wasiotokana na vyama vya siasa vilivyotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria hadi kufikia walau idadi sawa na wajumbe wanaotokana na Bunge na Baraza la Wawakilishi. Hatua hii itafikisha idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum kuwa 876. Kwa kulinganisha na uzoefu wa nchi nyingine zilizopitia hatua hii ya kutengeneza Katiba Mpya kwa utaratibu huu, idadi hii sio kubwa sana kwa kulingana na mazingira halisi ya nchi yetu.

5. UWAKILISHI WA ZANZIBAR KATIKA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Rais,

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaliwa kwa kuunganisha nchi mbili zilizokuwa huru na zenye hadhi na haki sawa, licha ya tofauti zao za ukubwa wa eneo au idadi ya watu wake. Katiba Mpya ambayo mchakato wake umeleta mgogoro wa sasa inatakiwa kuakisi haki na hadhi sawa kati ya nchi hizi mbili. Kama ambavyo mtaalamu mmoja wa masuala ya sheria na Katiba na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambavyo amesema kuhusu mchakato wetu wa Katiba Mpya, "katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa."

Hata hivyo, Mheshimiwa Rais, dhana hii ya haki na hadhi sawa kati ya Washirika wa Muungano haijazingatiwa wakati wa kupitishwa kwa Muswada huu. Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalum watakaotokana na wajumbe 166 walioainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) "... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao." Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55. Kwa sasa Wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76.
 
Mleta uzi ndo wale mabinti wanaohongwa chips!! Baada ya Juice ndo nini? inamaana ikulu ndo kuna juice pekeee??
 
Nawapongeza wapinzani na rais kwa kujinyima kufanya mambo yao mengine na kukaa pamoja kujadili mustakabali wa nchi yetu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom