Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
IKULU PANA MNYAMA, SURA KAMA MWANANGU.
Nasema nawe kibabu, rafiki yake kileje,
Huwezi wajipa tabu, sijui hata ukoje?
Kwa chai takuadhibu, siulize nawezaje,
Jamii yako ya boflo, chai ni chako kiboko.
Utambe kibabu tamba, utabaki kuwa ngano,
Tamba mjini na shamba, takungoja kwa chano,
Kibabu hauwi mwamba, mbele ya haya meno,
Nguvu yako ya hamira, uko na nini kibabu.
Kote Unguja na Pemba, hata huku kwetu bara,
Kibabu weye watamba, na sandarusi za gwara,
Waununua umwamba, sihasa ni biashara,
Siasa yaweka mtu, sihasa ya mnunua.
Siha ya huyu kibabu, mwenzenu yanipa shaka,
Tembea yake ya tabu, mwendowe apepesuka,
Anahitaji tabibu, kwa joto atetemeka,
Ikulu pana mnyama, suraye kama mwanangu.
Njano5.
0784845394
0762845394 Whatspp