Ikulu, Dar: Rais Magufuli azungumza na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito

Kwa jinsi Kikao kinavyoendelea natabiri kuwa leo jioni au Kesho asubuhi kuna Wakubwa wa Tanesco Makao Makuu, UWURA na Mikoani na hata Wizarani wanaenda Kutumbuliwa. Siku hizi Mheshimiwa Rais amebuni mbinu mpya ambapo akishapata tu Madudu ya Watendaji wake huwa hawatumbui Kwanza na badala yake anawatega kisha anawasakizia kwa Watu ili wasemwe vibaya halafu hapo hapo apate sababu ya Kuwatumbua na asilaumiwe au kuonekana mbaya.

Nawaomba Wakubwa wa Tanesco, UWURA na Wizara ya husika ya Nishati kuanzia sasa waanze Kuaga na Kujiandaa Kisaikolojia kwani kuna Watu wanatafutwa na leo ndiyo Siku yao ya Kupatiwa sababu ili Waondolewe katika Nafasi zao hizo husika.
 
Kama Karitas Kyando wa kutoka Njombe hayuko kwenye huo mkutano, akatafutwe. Yeye ndiye mwanzilishi wa kwanza wa huu mradi. Alienda Sido wakamtengenezea Turbine, akaunganisha na altenator akaanza kugenerate umeme. Alivyokuja Dar, alielekezwa kwangu nikamsaidia kupata vifaa vya umeme kwa ajili ya kufanya distribution. Nadhani ni huko Lujewa/ Ludewa...
Kifupi kwenye huo mkutano Kama hakuna Padri Katoliki utakuwa uonevu.Kwenye hiyo miradi wako vizuri mno
 
Hapo kinachoongelewa Ni wabunifu wa mitambo ya umeme wa maji Sio wanunuzi wa mitambo ya micro hydro power ya maji toka ulaya na kuja kuifunga Tanzania
Ubunifu kwa uelewa wangu ni invention,hapa sioni an inventive step zaidi ya design and construction of. micro turbine.Design siyo invention!
 
Anatoa milioni kumi kwa kila mbunifu kuwaongezea mitaji, kama wanaweza kwa nini wasisitishe ujenzi wa stiglers ili wawape hela za kutosha na vyanzo vipo vingi ili kuokoa kukopa hela nyingi za mradi wa stiglers gorge? na tutabaki na mbuga yetu ya selous?
 
Bwana pwagu amesoma mpaka la saba anafahamu mpaka level lakini Tanesco walimdharau hata Jenista walitaka CV yake kwanza, wakati yeye ni la saba tu wakamdharau..Akatokea mjerumani akamsaidia, wasomi wa nchi hii wana dharau sana ndio maana mambo hayaendi.
 
Mh. Rais ametoa milioni 5 kwa wabunifu wawili wagawane, yaani MH. alikuwa na fedha za zawadi kabisa, TANESCO lazima kuna mtu anatumbuliwa, ila kuna watanzaia wako vizuri sana. Inabidi sasa mh. aachanae na maprofesa na wanasiasa, kwenye utendaji atumie wataalamu hata ambao hawajenda shule. Maprofesa wa jalalani hawana faida kwa nchi hii.
 
Back
Top Bottom