Ikulu, Dar: Rais Magufuli ataka Lugumi achukuliwe hatua. Kuna hela zimechezewa NIDA, achoka kutoa rambirambi

Hapo Mbowe anakusanya Ushahidi wa Udikteta.

Ila wewe mbunge unampingaje mwenyekiti wa Chama uliyeapa utiifu kwake?
 
Kwa kauli hizi za baba mwenye nyumba ni dhahiri shari kabisa bunge lingevunjwa.

1. "Wewe nimekufuatilia bungeni, unatetea Ilan ya CCM. Hauungani na wale wengine Mwingine anasema 'tukienda hivi tutashindwa', sasa kwanini bado upo humo? Si undoke? Unafanya nini humo?" - @MagufuliJP

2. "mwingine anataka popularity, eti atachomewa nyumba Walisema watafanya fujo. Wafanye waone. Nilimwambia waziri mkuu, wakafanye fujo waone. Kama kuna shangazi zake ndio ningeanza kupiga hao." - @MagufuliJP

3. "Nilimpigia simu waziri mkuu saa nane usiku. Katibu mkuu nikamuuliza, kuna wabunge wangapi wa CCM huko kusini? Akasema 17. Nikasema futa wote tuanze upya. Bado column tunayo ya kutosha. Hata waziri mkuu nae angeondoka, nae si wa huko kusini" - @MagufuliJP


Kiufupi serikali ndiyo inalisimamia bunge.
Zee la Vi-Wonder halitaki kukosolewa hata kama UNATANIA !
- Mrisho Mpoto anaisoma namba baada ya kujifanya anataka kulielekeza zee la vi-wonder nini cha kufanya
 
hizi ni kauli za hovyo sana, huwezi mwambia waziri mkuu kwamba nae angeondoka tu. wala si ubabe ni ujinga tu.
 
Kuna umuhimu gani wananchi kuendelea kuwachagua watu wanaopeana maelekezo kuwanyonya wananchi.
Wananchi hawakumchagua mbunge akatete chama ila wao.
 
Habari wakuu,

Rais Magufuli anatazamiwa kuwaapisha Kangi Lugola na wenzake walioteuliwa jana. Shughuli hiyo itafanyika Ikulu Dar Es Salaam leo hii saa tisa alasiri.

Walioteuliwa wote wanatakiwa kufika ukimbi wa Kikwete Ikulu saa saba mchana.

Tutajuzana hapa kinachojiri.

Karibuni sana..


UPDATES: 15:15hrs

Rais Magufuli ameshaingia ukumbini na wimbo wa taifa unaimbwa.



1. Anayeanza kuapa ni Makame Mbarawa ambaye anaapa kuwa Waziri wa Maji na umwajiliaji.

2. Isack Aloyce kamwelwe anaapa kuwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

3. Kangi Lugola anaapa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi

4. Mhe. Mussa Ramadhani Sima (Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini) anaapa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira.

5. Mhe. Omary Tebwete Mgumba anaapa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

6. Moses Mpogole Kusiluka ameapa kuwa Katibu Mkuu Ikulu

7. Mej Jen. Jacob Kingu anaapa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

8. Dkt. Rashid Adam Tamatamah anaapa kuwa Katibu Mkuu Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

9. Bw. Ramadhani Kailima anaapa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

10. Prof. Siza Donald Tumbo anaapa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Thomas Didimu Kashililah ambaye amestaafu.

11. Jaji Mbarouk Salim Mbarouk anaapa kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo.


12. Mhe. Jaji Mstaafu Thomas Mihayo anaapa kuwa kamishina wa tume ya Uchaguzi.

13. Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri anaapa kuwa Kamishina wa tume ya taifa ya uchaguzi.

14. Bw. Athumani Juma Kihamia anaapa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Ramadhani Kailima ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

15.Bw. Mohammed Ali Ahmed anaapa kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar.

=======

Waziri Mkuu: Nitumie nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu, pili niwapongeze viongozi wapya walioteuliwa. Mimi nitumie nafasi hii kuwataka viongozi walioapa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa. Rais amewaamini na jambo muhimu ni kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na chama tawala kupitia Ilani na maelekezo ya mheshimiwa Rais aliyoyatoa wakati anafungua Bunge.

Nendeni mkajifunze kwenye sekta zenu nini mahitaji, mnapokwenda mtakuta staff wenzenu ambayo mtashirikiana nao kutekeleza majukumu, tuma nusu ya awamu hii na juzi tumemaliza bajeti ikiwemo kupokea maoni na mapendekezo ya wabunge. Nina imani tutaanza kwa kasi nzuri kutikiza malengo ya watanzania.

Rais Magufuli: Hongereni kwa nafasi ambazo mmezipata pia hongereni kwa viapo ambavyo nimeangalia midomoni mwenu wote mlikuwa mnaviapa. Msimamizi mkuu wa ilani ya uchaguzi yuko hapa ambaye ni katibu mkuu, nina imani mlioteuliwa mtaenda kushirikiana na wenzenu katika majukumu ya kuwatumikia watanzania.

Kuna matatizo makubwa kwenye maji, Mheshimiwa Mbarawa tumekupeleka uko na ukali ukauendeleze kusudi watanzania waweze kupata maji. Watanzania wanateseka sana, tunapeleka pesa nyingi lakini hazitumiki, kalisimamie hilo ili miradi ya maji ikatekelezwe.

Kila mmoja katika wajibu wake akafanye hiyo kazi, mambo ya kubembeleza yasiwepo kwa sababu wananchi 2020 hawatatubembeleza na imebaki miaka miwili na nusu hivyo tumefika katikati.

Eng Kamwele umekuwepo pale kama Injinia na umeshiriki katika miradi mbalimbali hasa iliyofadhiliwa na wafadhili. Ukali ukaupeleke kule. Barabara ya Mtwara mpaka Masasi ikatengenezwe ikamilike, fedha zipo. Utengenezaji wa Feri katika ziwa Viktoria umechukua muda mrefu na fedha zipo. Flyover ya Ubungo ikamilike, ipo miradi mingi ambayo ipo pending.

TCRA wanafanya kazi vizuri lakini kasimamie wafanye kazi vizuri zaidi. Ndege tulizonunua sio za shirika la ATCL, tumewakodisha na tumezinunua kwa fedha za watanzania.

Wizara ya mambo ya ndani haijaniimpress, inafanya mambo ya hovyo. Huku juu sijawa impressed na lazima niwaeleze ukweli, nimekupeleka pale ukafanye kazi na wewe bahati nzuri ni askari.

Kupitia kamati ya Bunge ilifanya uchunguzi wa mikataba mbalimbali ikiwemo wa Lugumi, tulipewa maagizo na kamati ya Bunge na mpaka leo hayajapata solution. Mgari 777 yaliagizwa kupitia mkataba wa hovyo. Magari ambayo yameazwa kuletwa yameandikwa mapya lakini yametembea zaidi ya KM 4,000. Yapo hajaandikwa year of manufacture.

Nimempeka Kailima ambae alisimamia vizuri kwenye uchaguzi, ukishinda umeshinda na ukishindwa umeshindwa. Mkataba ni wahovyo hata bei ya magari ni ya hovyo, kuna mambo ya uniform hewa, niliowapeleka pale hawakutatua matatizo haya, mabilioni hayaonekani. Wewe kaa tuu yako mengi.

Kuna suala la NIDA, kuna pesa zilipotea kule hovyo hovyo, sijaona hatua ambazo zimechukuliwa. Kuna mambo yanafichwa fichwa. PCCB nao naona wanapachezea chezea, Ntaka leo tuambizane ukweli.

Nimechoka kutoa ranbirambi, mfano mzuri ni mkuo wa Mbeya, ndani ya wiki mbili wamefariki watu 40. Hakuna hatua hata za RPC kujiuzulu, si umpunguzie nyota ili ajue damu zilizomwagika pale. Kaaze na RPC wa Mbeya na RTO.

NGO, nyingine za hovyo na zinafanya mambo ya hovyo kinyume na maslahi ya watanzania. Tunahitaji NGO zinazofanya kwa maslahi ya watanzania na sio ya wenye NGO.

Promotion ya maaskari, nashukuru IGP naliangalia hili, kashughulikie hili. Vibali vya working permit vinatolewa kama njugu, kashughulikie hili. Kuna kesi watu wameshikwa Oysterbay wanatoa working permit wao na wana mitambo yao. Ilibidi taarifa nitoe mimi na mwenyewe na mmoja wa watuhumiwa ni mfanyakazi wa immigration. Haya yalitakiwa kufanya na waziri au naibu waziri, mnanichosha.

Sijui nizungumze mangapi, katika wizara zinazoongoza kwa madai ya hovyo yaliyopelekwa wizara ya fedha ni wizara ya mambo ya ndani. Magereza kawafanye wafungwa wafanye kazi, nchi nyingine duniani zinatumia wafungwa kuzalisha, hapa sisi tunawalisha, sasa ulimfunga wa nini.

Kuna mashamba hayatumiki, wafanye kazi kwelikweli. Mbona tumefanya amendment ya korosho, huyu wa mambo ya ndani mbona hapeleki kama wafungwa waliohukumiwa kifo sheria inawazuia kufanya kazi.

Wa kilimo, nakupongeza kwa mchango wako bungeni, mimi huwa naangalia hasa wa CCM wapo ambao huwa wanajisahau, unakuta mwingine anazungumza tukifanya hivi tutashindwa, kwanini unaendelea kuwa humu, si ondoka.

Wewe nakupongeza, ulisimama, Mwenyekiti alikuwa anajaribu kuzibaziba na kwa sababu mwenyekiti huyo huyo alihusika kuzitengeneza hizo sheria mbaya za wakati ule, alishiriki kuharibu hizo sheria akawa anakukatisha tamaa, nakupongeza, nikasema wewe unastahili hiki ulichokipata.

Wapo waliokuwa wanataka umaarufu kule bungeni wakawa wanasema watafanya fujo, nikamwambia waziri mkuu waache wafanye fujo. Nitaanzia kwenye jimbo lake kama kuna shangazi zake nitaanza kupia hao

Nilimuuluza mtwara na lindi kuna wabunge wangapinwa ccm akasema 17 nikamwambia bora waondoke wote. na nikambigia simu katibu waccm na kuongea nae kwamba tuanze mpango huo. Pampoja na yeye Waziri mKuu angeondoka na yeye si wa huko huko

na wakati wa kupitisha bajeti nilimuambia katibu mkuu nenda kaangalie wabunge wote wa ccm ambao hawatakuwepo bungeni na awatandike barua. " Katibu Mkuu umefanya hivyo?".

Katika yoooote nimesikia na kuelewa THOMAS BASHITE MIHAYO hahahaaa naona bashite mkuu wa mkoa kafurahi saaana
 
Nia ni njema, lakini Nauliza, Tanzania nadhani ni less than 10% or so ndio wana maji ya safi na salama.. (ya bomba). Sasa huyu Mbawala atatatua kero ya maji vipi maana over 90% ya watanzania hawana maji safi na salama ... Anaanzia wapi? Anaanzaje.
Kwa research ipi mkuu?
 
Wabunge 17 kuwapoteza siyo kitu kidog, labda kwa vile alishaapa kuwa "nikupe gari, mshahara etc halafu umtangaze mpinzani mshindi.." labda atumie mbinu hiyo katika uchaguzi.
CCM ni ileile.
Umesahau kuna aliesema sizihitaji kura za wafanyakazi?
 
Back
Top Bottom