Iko wapi thamani ya viongozi wa Upinzani? RIP Kamanda Mawazo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,075
114,602
Mungu baba uliye mbinguni unaona machungu ya mja wako napowasilisha ujumbe wangu kwa Watanzania.

Mauaji na ukatili wa Ndugu zangu kiitikadi sio jambo zito Tanzania.

Ndugu zangu hawa wameuawa mchana kweupe na wauaji wakijuliana.

Wenye nchi wako kimya kukumea haya,zile amri kwamba wahusika wapatikane wakiwa hai au wamekufa hazikuwahi kutolewa.

Baba unashuhudia kwamba Mauaji ya Mifugo kule Morogoro yakipewa uzito wa Matamko kuliko Kifo cha Kikatili cha Kaka Yangu kiitikadi Alphonce. Mawazo.

Kamanda Mawazo alichinjwa kikatili,kama walivyochinjwa wanyonge sita kule Sengerema,kama mashetani walivyokatili roho ya Afande Kinyagori au askari wengine ambapo misako ya hatari imeendelea dhidi ya makatili.

Mungu nawakabidhi kwako wakuu wa nchi upime kama wanafanya hivyo hata kwetu sisi.

Huwa nikikumbuka kifo cha Kamanda Mawazo roho ya ukatili hunijia,nakemea nakemea tokaaaaaa shetani tokaaaa!!

Mungu nawakabidhi kwako wauaji hawa kwa kuwa hawana mbabe hapa chini ya ardhi,ila ni wewe tu baba.
 
Alale pema Kamanda..Alipigana vita vilivyo vema.Mawazo yake na maandishi yake yatadumu waliofumba macho na kumdhihaki damu yake inaendelea kuishi.. Tunaendelea kuamini ipo siku watajitokeza wenyewe
 
Polis akifa mwenzao au wengine, ambao wanaonekana matighter wanawapata fasta wauaji, lakin sijui habar za ukawa, eeeh sahau ndugu yangu. Sasaiv ni mwendo wa kujilinda uwe na bastola yako kibindon mtu akijipendeza tu unazaa nae, maana hakuna namna nyingine tena! mambo ya kusubiri ulalamike ni ufala.
 
wahalifu huwa hamjifichi....!! waswahili husema " mchuma janga, hula na wa kwao"
 
Nyumbu wabinafsi sana,juzi wamechinjwa watu msikitini mpo kimyaaa,ina mana hakuna hata mmoja ukawa?acheni ubinafsi
 
Inaniuma sana, lakini naamini Mungu ataitaka damu yake kwa baadhi ya viongozi wa nchi hii. Kwa maana in heri yule aendae nyumba ya matanga, kuliko nyumba ya sherehe. Nakuambia hautapita mwaka Mungu atavipatiliza vizazi vyote vya wale waliohusika, na kuufumbia macho ukatili ule huku wakiwa na mamlaka mabegani mwao.
 
wahalifu huwa hamjifichi....!! waswahili husema " mchuma janga, hula na wa kwao"
Ishu sio uhalifu mkuu, polisi wameshindwa kuwalinda wananchi na mali zao, sasa watu waache wauwawe? Kuna matukio watu wameuawa kisiasa mengi tu, kuna watu wanauwawa na boda boda kila siku.
 
Mungu baba uliye mbinguni unaona machungu ya mja wako napowasilisha ujumbe wangu kwa Watanzania.

Mauaji na ukatili wa Ndugu zangu kiitikadi sio jambo zito Tanzania.

Ndugu zangu hawa wameuawa mchana kweupe na wauaji wakijuliana.

Wenye nchi wako kimya kukumea haya,zile amri kwamba wahusika wapatikane wakiwa hai au wamekufa hazikuwahi kutolewa.

Baba unashuhudia kwamba Mauaji ya Mifugo kule Morogoro yakipewa uzito wa Matamko kuliko Kifo cha Kikatili cha Kaka Yangu kiitikadi Alphonce. Mawazo.

Kamanda Mawazo alichinjwa kikatili,kama walivyochinjwa wanyonge sita kule Sengerema,kama mashetani walivyokatili roho ya Afande Kinyagori au askari wengine ambapo misako ya hatari imeendelea dhidi ya makatili.

Mungu nawakabidhi kwako wakuu wa nchi upime kama wanafanya hivyo hata kwetu sisi.

Huwa nikikumbuka kifo cha Kamanda Mawazo roho ya ukatili hunijia,nakemea nakemea tokaaaaaa shetani tokaaaa!!

Mungu nawakabidhi kwako wauaji hawa kwa kuwa hawana mbabe hapa chini ya ardhi,ila ni wewe tu baba.

Ni nani tena huyo embu funguka basi na sisi wengine pia tuchangie!
 
Bado unaendeleza swaga za Mawazo? Vipi kuhusu mauaji ya Chacha Wangwe na Regia Mtema? Kwani wao hawakuwa makamanda?
kweli mkuu naona kama kuna ubinafisi flani hivi,
chacha wangwe hatajwi popote kweli siasa ni kizungumkuti.
 
Back
Top Bottom