sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Tukisema serikali hii inafanya kazi double standard mnatoa mapovu.
Jana mkuu wa mkoa wa Iringa alifanya ziara kutembelea kituo cha Sober house Iringa kilichoko jirani na shule ya msingi Tumaini na Ngome maeneo ya Semetema b kihesa,ziara ikiwa na lengo zuri tu,lakini ajabu leo hii asubuhi caterpillar la Manispaa limepita uwanja wa shule ya msingi Tumaini na kuchonga barabara ya kupita magari.
Swali watoto wetu wanaosoma hapo shule ya Tumaini na ngome wakacheze wapi ikiwa serikali imeingilia eneo lao la wazi na kuchonga barabara wakati kuna njia mbili zinazopita pembeni ya uwanja huo ambazo zingechongwa kusingeathiri maeneo hayo.
Iko wapi haki ya watoto kucheza ikiwa uhuru wao unaingiliwa? Tunaomba serikali ya mkoa ilitazame suala hili kwa umakini kuepuka tafrani inayoweza kutokea.