Iko wapi elimu yetu ya 1990-2005?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Elimu ambayo ukiwa class tree unakuwa una uwezo mkubwa wa kuandika maneno kupitia dictation? iko wapi elimu ya uandishi wa insha mtoto anamaliza class seven ana uwezo mkubwa wa kutunga story za kusisimua kupitia Insha.

Sina tatizo na elimu ya nyuma uko yaani sijawataja kwa sababu ndio wameshababisha ufisadi wa kutisha serikalini, wale waliosoma miaka ya 1940-1989 wanajua ni jins gani wamesababisha hasara kwa taifa letu.

Tuliosoma 1990-2005 wenge wako sector binafsi na waliopo serikalini hawajapata nafasi ya kulitumikia taifa ipasavyo lakini wengi tumefanya mapinduzi makubwa kwenye sector binafsi niko tayari kukosolewa ila naamini watu waliosoma kipindi iki wengi ndio wana uwezo mkubwa wa kuhoji mambo mengi.

Nani kazika elimu yetu? nini tatizo je walimu wanaandaliwa ipasavyo kama zamani? je wanafunzi ndio tatizo? nahitaji mjadala wa kitaifa.
 
Kabisa mkuuu, ile elimu ulikuwa unasoma na mtoto wa kiongozi yeyote kwenye hizi shule zetu za kawaida ila kwa sasa hata mwl wa primary kwa mshahara wake wa 390k hawezi kumsomesha mtoto wake kwenye shule anayofundisha yeye
 
Mjadala wa ubora wa elimu haujengwi kwenye hizo dhana za kufikirika za sijui insha na kusikiliza dictation.

Ubora wa elimu ni pamoja na usimikaji wa miundombinu, accessibility ya elimu, enrolment ya wanafunzi, idadi wa waalimu, aina ya mtaala na mengine mengi.

Kutoka miaka hiyo mpaka miaka hii, hayo yote yameboreshwa kwa kiasi gani? JIULIZE.
 
Mjadala wa ubora wa elimu haujengwi kwenye hizo dhana za kufikirika za sijui insha na kusikiliza dictation.

Ubora wa elimu ni pamoja na usimikaji wa miundombinu, accessibility ya elimu, enrolment ya wanafunzi, idadi wa waalimu, aina ya mtaala na mengine mengi.

Kutoka miaka hiyo mpaka miaka hii, hayo yote yameboreshwa kwa kiasi gani? JIULIZE.
Tunazungumzia ubora wa mwanafunzi anayemaliza shule. Leo hii kuna kila aina ya vitabu, kama ungekuwa mdau wa karibu wa elimu ungeona utofauti mkubwa tunaouzungumzia. Sio majengo wala idadi ya wanafunzi kwenye mashule.
 
Mzee baba wanasiasa wameharibu sana elimu yetu baada ya watoto wao kufeli na kushindwa kuenenda na mfumo uliokuwepo.

Inaumiza sana.
 
Elimu una maanisha kitu gani?
Kukariri mambo ya vasco da Gama au Area of rectangle

Hivi wewe bwege Integration au differential eqn ina msaada gani kwako?


Habari za majimaji War zina faida gani?


Kama kuna project yeyote ya kwenda sayari za Mars au Jupiter hapa Tanzania naunga mkono elimu iliishia mwaka huo 2004

Ila kama elimu ni kusoma habari za laws of Newton na kukariri basi kichwa chako komeyumba
Elimu mwisho ilikua 2004.

Baada ya hapo ni drama tu.
 
Elimu umeipima kwa kipindi cha umri wako na fikra zako?

Hata wakati ule Michaelangelo ameitwa na Papa pale Vatican alidharau watu waliomtangulia na kujenga sistene Chapel


Tulia mkuu kila dhama na kitabu chake, Leo kuna elimu bora hapa Tanzania kuliko wakati wowote ule kwani teknolojia ipo juu

Tatizo lako huna pesa la kupeleka watoto wako vyuo bora huko Canada na Marekani wakishamaliza form six au Four

Wewe ni maskini mtoto wako anasoma shule za wanyonge na wewe ni Mnyonge kama serikali invyosema inawapa elimu watu wanyonge

Tafuta pesa peleka mtoto int school of Tanganyika hutajuta

Leo Tanzania kuna elimu bora ya kisasa kupitia mitandao
 
You are right bro, Mleta mada ukimuuliza una miaka mingapi atakuambia amezaliwa zamani akimaanisha miaka ya 1980, Hajui kila mtu ana zamani yake hata wale waliozaliwa 2000 ni zamani kwa fikra zao

Mleta uzi ufikiri wake ni mdogo sana
Mjadala wa ubora wa elimu haujengwi kwenye hizo dhana za kufikirika za sijui insha na kusikiliza dictation.

Ubora wa elimu ni pamoja na usimikaji wa miundombinu, accessibility ya elimu, enrolment ya wanafunzi, idadi wa waalimu, aina ya mtaala na mengine mengi.

Kutoka miaka hiyo mpaka miaka hii, hayo yote yameboreshwa kwa kiasi gani? JIULIZE.
 
Afrika hatujawahi kuwa na elimu bora kamwe, ila tumewahi kuwa na wanafunzi bora mpaka wengine wamepenya America na kuitikisa dunia mfano Elon musk.Unapizungumzia elimu ya miaka ya 90 - 2000 unatukumbusha mateso ya kukaa chini,kitabu kimoja au vichache tu,walimu wachache hasa vijijini.Lack of materials ,poor library nk.Elimu Tanzania hakuna kipindi imewahi kuwa bora ndio maana familia zetu nyingi ni choka mbaya kwa sababu ya ignorance.

Elimu bado ni duni japo miundombinu imeboreka kidogo.Vitabu vimekuwa vikipekekwa mashuleni tangu awamu ya mkapa, majengo ya memm nk.

Tatizo kubwa lililopo Tanzania in Mtaala ulio duni duni duni.Kuna mambo yanafundushwa mpka unajiuluza yanafaida gani.Mfano Angola ilitawaliwa na nani, Mandela alitolewa gerezani mwaka gani!,Nyerer alikufa mwaka gani.

Anayejua tarehe hizo na asiejua tarehe hizo wanatofautiana nini ktk kupambana na maisha ya kisasa
Katika dunia ya Leo anayejua matarehe hayo na anayejua internet inafanyaje kazi mwenye faida ni wa internet kwa sababu elimu ipo kiganjani.

Elimu ya Tanzania na Afrika ni hovyo kulinganisha na wakati uliopo.

Wenzetu watoto wao wanaibuka kuanzia umri mdogo sisi tunaibukia ukubwani Hatuna wagunduzi wala notable people on earth.Hatujawahi kuwa na elimu bora bali wanafunzi bora.
 
Hapo kwenye kuhoji Nitawatetea kizazi cha sa hivi na elimu yake. Sa hivi vijana na watoto wana uwezo wa kuhoji sana tofauti na miaka ya nyuma. Wapo wajinga ndio, ila wapo werevu wakuhoji kweli kweli kuanzia Maswala ya Dini,elimu,siasa au michezo.

Pia hiyo elimu mnayo ilaumu sa hivi waloitengeneza ni hao mlikuwa bora wa miaka hiyo mnayosema. Swali kwani mtaala wa elimu umeanzishwa na hawa vijana wa leo? Bora tungesema walosoma 1990-2004 wameharibu mfumo wa elimu kwani usimamizi wao kwenye elimu juu ya vijana wao wa sa hivi wameshindwa kuusimamia ipasavyo.

Miaka hiyo tulilishwa uwongo mwingi kutoka kwa wanasiasa,walimu,familia n.k na tukakubali . Ila sa hivi vijana ni wepesi sana kuhoji mengi ambayo sisi tumekuja yajua tunamiaka 18.
 
Back
Top Bottom