Ikiwezekana Mahakama zinazotembea zitumike kama mwarobaini wa kutatua makosa ya kubambikiwa barabarani (Traffic case)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,408
Katika vitu au kesi ambazo Mahakama inayotembea ingezikumbuka; ni kesi za makosa barabarani!

Kuna makosa ambayo unakuta trafiki anambambika mtu (Dereva) ili asaini/ akatae kwa ajili ya kupeleka mahakamani!

Tena mamlaka yamempa trafiki huyo huyo mbambikaji uwezo hata wa kumuweka ndani (In side the cell/lockup) dereva anayesubiri kupelekwa mahakamani.

Hebu jaribu kuwaza mtu anawahi shughuli zake halafu anakutana na kadhia hii ya kupotezewa muda wakati wakisubiri kwenda mahamani siku kadhaa mbele. Utagundua hapo rushwa HAITAEPUKIKA!

Ujio wa mahakama zinazotembea ni matarajio yangu zingeanza kushughulika na kesi kama hizi; Ili mnaposhindwana, Mahakama inaitwa kwa simu kama ambulance!

Mnapaki mzigo pembeni hapo hapo site kesi inasikilizwa, mashahidi wanasikilizwa hapo hapo site hukumu inatoka bila kupotezeana muda!

Pia Mahakama zinazotembea zinaweza kutumika kutoa hukumu za malipo ya bima kwa watoa BIMA wasumbufu!

Hebuwaza ukiendesha gari pasipo BIMA/au BIMA ikiwa imeexpire unavyokamatwa fasta; lakini ikitokea mwenye gari kapata ajali (accident) polisi hawamkamati mtoa BIMA msumbufu anayechelewesha fidia ya malipo kwa Mteja wao.

Kwahiyo hapo unaona waziwazi kabisa polisi wanajali kusimamia malipo ya kuingiza tu, ya kutoa inakuwa kama haiwahusu wakishamaliza kupima ajali basi.

Hivyo Mahakama pia iweke utaratibu wa hukumu ya kulipwa fasta mteja wa BIMA na malipo yanapocheleweshwa yawe na penalty inayopanda kila siku!

Mahakama hii ingeweza kabisa kupunguza kero kama hizi na zingine
 
Back
Top Bottom