Ikiwa mchakato wa Katiba mpya wa awali ulikwama kwa ubinafsi wa viongozi wa vyama vya siasa, kuna haja gani ya kuanzisha michakato mwingine?

Ikiwa mchakato wa Katiba mpya wa awali ulikwama kwa ubinafsi wa viongozi wa vyama vya siasa, kuna haja gani ya kuanzisha michakato mwingine?

Nani kakwambia kuwa katiba siyo kipaumbele cha wananchi? Au kwa sababu wengi humu wanakupuuza ndiyo sababu ya kuongea ujinga ujinga
wananchi wenyewe wanasema hivyo kupitia wawakilishi wao kwenye vyombo vya maamuzi gentleman.

ni ni haki na uhuru wa mdau yeyote wa JF kupuuza au kutopuuza mambo yanayopostiwa humu jukwaani bila kubabaika au kua na mihemko na makasiriko kama wewe 🐒
 
Kwasababu bado dhana na hali ya kususia imetanda miongoni mwa vyama vya siasa, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa ambavyo vimeamua kujitenga na michakato ya kidemokrasi na kujikita kutafuta pesa za matumizi ya viongozi wa vyama hivyo hususani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025.

Bilashaka yoyote hiyo inamaanisha katiba mpya sio kipaumbele cha wananchi bali pesa ndio kila kitu kwa baadhi ya vyama vya siasa, na kwahiyo hakuna haja kwa serikali kuanzisha mchakato wa gharama kubwa ambao mwisho wa siku unaishia njiani na hatimae kua hasara na mzigo kwa wananchi walipa kodi wa Tanzania.

Waliopewa dhamana ya uongozi wa taifa, ni muhimu zaidi wakajikita kutekeleza wajibu wao wa kikatiba wa kuwafanyia kazi waTanzania wote. hakuna sababu ya maana hata moja kuanzisha mchakato wa katiba mpya katika wakati wowote ujao, kwasababu baadhi ya vyama vya siasa wamejipanga kuvuruga michakato yote ya kidemokrasi ikiwa ni pamoja na uchaguzi mkuu kama walivyovuruga mchakato wa katiba wa awali kwa maslahi yao binafsi.

Kwa maoni yangu,
Serikali ijikite katika kuwatumikia waTanzania na kutimiza vipaumbele vya mahitaji yao ya kila siku kama vile maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, nishati, miundombinu n.k, kuliko kufuja pesa kwenye mambo ambayo si kipaumbele cha wananchi.

una maoni gani?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Kama Katiba mpya siyo kipaumbele cha Wananchi wa Tanzania kwa sababu tu wanatafuta pesa kwa nini Serikali inashindwa kuwawekea mazingira mazuri ili wananchi wote wawe na pesa na waache kumpamba mtu mmoja kwa mapambio kama yeye ndiyo kiini cha pesa zao na maisha yao? Je,ikitokea huyo mtu akifariki hao hao wananchi watatumia mbinu gani ku survive maana mwenye pesa za bure ameshakufa?Je,kabla yake maisha hayakuwepo Tanzania??
 
hakuna haja ya hayo yote gentleman ikiwa wanasiasa kwa ubinafsi wao hawaoni haja ya ya jambo hilo na wameamua kujitenga na michakato yoyote ya kidemokrasia.

sasa hiyo ibara ina umuhimu gani tena gentleman?🐒
Soma vizuri Ibara ya 13(2) na (5),pia soma 3(1) kwenye Katiba yetu ili upunguze upuuzi.
 
Mchakato na uandaaji wa Katiba mpya hautakiwi kuwahusisha wanasiasa, wanasiasa wanawaza maslahi yao kwanza. Wananchi kupitia viongozi wa dini na asasi za kiraia ndio watuwakilishe kwenye mchakato wa kuandika au kurekebidha katiba.

Vv
 
Marekebisho ya katiba ni muhimu ila wanasiasa wana vipaumbele vyao vya kipumbavu sana ndo maana mchakato hauwezi kufanikiwa. Katiba ikiwa nzuri hayo maendeleo kwa wananchi ni rahisi kupatikana. Kwa mfano kwa sasa kuna sheria nyingi zinazolalamikiwa hasa hizi za mambo ya kodi. Wananchi wengi wanaitupia lawama TRA na kusahau kuwa TRA ni watelekezaji tu wa sheria iliyotungwa na bunge. Wabunge wetu ni wa kulaumiwa ila nao kuwalaumu ni kupoteza muda kwa sababu wengi wao ni vilaza wenye elimu duni walioingia bungeni kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika. Kwa tulipofikia katiba ifanyiwe marekebisho na kuzuia vilaza kuingia bungeni.

Wanasiasa wao wanataka katiba ibadilishwe na kuongeza vyeo vya wao kupata ulaji. CHADEMA na wachumia tumbo wengine wanachotaka ni katiba iruhusu kuundwa serikali tatu na kuwepo kwa wabunge wawili kila jimbo. Yaani vipaumbele vyao ni maumivu makali mno kwa mwananchi mlipa kodi endapo watafanikiwa.

Ni bora kuendelea na katiba iliyopo kuliko kukubali matakwa ya CHADEMA na Jaji Warioba. Ile rasimu ya Warioba ilikuwa na mapungufu mengi mno.
Mbona hueleweki chawa ?
 
Soma vizuri Ibara ya 13(2) na (5),pia soma 3(1) kwenye Katiba yetu ili upunguze upuuzi.
Gentleman,
hiyo si ni sawa na kususia au kugomea michakato ya kidemokrasia tu,

hakuna haja ya kubabaika na kusumbua wananchi kwa habari ya katiba mpya kabisaa, ambayo sio kipaumbele chao kwa sasa na tuendako.

Ni muhimu kufahamu hili bila mihemko ambayo kwakweli ni useless na completely nonsense kwenye mijadala muhimu sana kama huu 🐒
 
Elewa kwanxa yaliyoandikwa kwenye ibara (8) ya katiba ili uache kubwabwaja kama mwehu
Propaganda za ccm hizo!! Kikwete aliitia kwapani rasimu ya Katiba ya Warioba baada ya kugundua kuwa ingepitishwa alikuwa a naelekea Ukonga ; kuhusu mambo ya Ufisadi aliyofanya na wafanyabiashara wakiwemo GSM/ Home Shopping Centre.
Sasa Wewe chawa acha propaganda kuwa wapinzani ndio walikwamisha Katiba mpya kupatikana! Kikwete kama Mwenyekiti wenu is guilty as charged.
 
Kama Katiba mpya siyo kipaumbele cha Wananchi wa Tanzania kwa sababu tu wanatafuta pesa kwa nini Serikali inashindwa kuwawekea mazingira mazuri ili wananchi wote wawe na pesa na waache kumpamba mtu mmoja kwa mapambio kama yeye ndiyo kiini cha pesa zao na maisha yao? Je,ikitokea huyo mtu akifariki hao hao wananchi watatumia mbinu gani ku survive maana mwenye pesa za bure ameshakufa?Je,kabla yake maisha hayakuwepo Tanzania??
Gentleman,
kua na pesa au kutokua na pesa Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu.

Lakini pia kua tajiri au maskini Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu.

ukiwa mvivu na mchagua kazi popote pale utapata tabu sana, utakua ni mtu wa kulaumu na mwenye chuki sana dhidi ya waliofanikiwa, Lakini pia ukiambiwa Ukweli unakua mkali kichizi dah!🐒
 
wananchi wenyewe wanasema hivyo kupitia wawakilishi wao kwenye vyombo vya maamuzi gentleman.

ni ni haki na uhuru wa mdau yeyote wa JF kupuuza au kutopuuza mambo yanayopostiwa humu jukwaani bila kubabaika au kua na mihemko na makasiriko kama wewe 🐒
Mim sina makasiriko, ila nakwambia ukweli. Wewe na Lucas Mwashambwa ni pipa na mfuniko
 
Mim sina makasiriko, ila nakwambia ukweli. Wewe na Lucas Mwashambwa ni pipa na mfuniko
binafsi sifahamu hilo gentleman,

Ila umahususi wa hoja mahususi uko pale pale kwamba, mchakato wa katiba mpya wa awali ulisusiwa na kuvurugwa na vibaka wa kisiasa,

je kuna haja gani ya kuanzisha mchakato mwingine wa gharama ambao ni wazi pia utasusiwa tu vile vile?

hilo ndilo la maana zaidi gentleman, ama wewe unasemaje kwa mfano?🐒
 
Gentleman,
hiyo si ni sawa na kususia au kugomea michakato ya kidemokrasia tu,

hakuna haja ya kubabaika na kusumbua wananchi kwa habari ya katiba mpya kabisaa, ambayo sio kipaumbele chao kwa sasa na tuendako.

Ni muhimu kufahamu hili bila mihemko ambayo kwakweli ni useless na completely nonsense kwenye mijadala muhimu sana kama huu 🐒
Katiba mpya siyo kipaumbele cha;-
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.CCM kwa vile katiba hii iliyopo ni ya kwao
3.Wana ccm kwa sababu watakosa ulaji
4.Machawa kwa sababu kazi yao ya kusifia viongozi itaisha automatically
5.Wajinga na mtoa mada akiwemo
6.Wapumbavu.Watu ambao hawataki mabadiliko.
7.Wezi wa mali za Umma
8.Mafisadi.
 
Propaganda za ccm hizo!! Kikwete aliitia kwapani rasimu ya Katiba ya Warioba baada ya kugundua kuwa ingepitishwa alikuwa a naelekea Ukonga ; kuhusu mambo ya Ufisadi aliyofanya na wafanyabiashara wakiwemo GSM/ Home Shopping Centre.
Sasa Wewe chawa acha propaganda kuwa wapinzani ndio walikwamisha Katiba mpya kupatikana! Kikwete kama Mwenyekiti wenu is guilty as charged.
Mimi sikuelwi unamaanisha nini?
 
Gentleman,
kua na pesa au kutokua na pesa Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu.

Lakini pia kua tajiri au maskini Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu.

ukiwa mvivu na mchagua kazi popote pale utapata tabu sana, utakua ni mtu wa kulaumu na mwenye chuki sana dhidi ya waliofanikiwa, Lakini pia ukiambiwa Ukweli unakua mkali kichizi dah!🐒
Kwa hiyo Mbowe na Zito Kabwe hawana pesa?
 
Katiba mpya siyo kipaumbele cha;-
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.CCM kwa vile katiba hii iliyopo ni ya kwao
3.Wana ccm kwa sababu watakosa ulaji
4.Machawa kwa sababu kazi yao ya kusifia viongozi itaisha automatically
5.Wajinga na mtoa mada akiwemo
6.Wapumbavu.Watu ambao hawataki mabadiliko.
7.Wezi wa mali za Umma
8.Mafisadi.
wewe orodhesha yote uliyonayo moyoni,
buti hoja mahususi mezani iko pale pale,

mchakato wa katiba mpya wa awali wa gharama kwelikweli, ulisusiwa na kuvurugwa kwa makusudi kwa ubinafsi wa vibaka na matapeli wa kisiasa,

je,
kuna haja ya kuanzisha mchakato mpya kwa gharama ile ile ya juu, hali ya kua kiwango cha kususia na kuvurugwa kwa mchakato huo kikiwa wazi kabisa gentleman?
 
Aliyekuwa na mamlaka ya kuifanikisha ni Rais wa awamu hiyo mbona sera za kuengua wapinzani kwenye chaguzi mnaziweza sana kwa nini hiyo Katiba mpya msingepitisha kwa namna yoyote ile.
 
Mkuu tunaongelea sera ya CHADEMA kuhusu kila jimbo kuwa na wabunge wawili. CCM haihusiki na hili. Au umeamua kuwa mpumbavu na kujifanya huelewi?
Narudia tena, hitimisho lako la wabunge wengi kwa mujibu wa cdm, ni mtazamo wako wa muundo wa kiutawala wa ccm wa sasa. Ndio nimekuambia acha kutoa majibu ya kwenye utawala wa cdm, kwa muundo huu wa kiccm. Kipi huelewi hapo?
 
Aliyekuwa na mamlaka ya kuifanikisha ni Rais wa awamu hiyo mbona sera za kuengua wapinzani kwenye chaguzi mnaziweza sana kwa nini hiyo Katiba mpya msingepitisha kwa namna yoyote ile.
mgombea wa uongozi yeyote yule asie kidhi sifa, vigezo na masharti ya kikatiba ataondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi bila mbamaba yoyote kwenye kila uchaguzi nchini.

hilo halina mjadala kabisa gentleman,
hatutakubali kuinajisi katiba kuruhusu watu wasio na sifa kugombea uongozi :NoGodNo:
 
Nimekuweka kwenye kundi la Wajinga kwa sababu unatetea upuuzi.Ina maana kila mtu anayegombea kwa tiketi ya chama kingine cha siasa hajui kusoma na kuandika vizuri???Siyo Raia wa nchi hii???Ni criminal?? Acha ujinga wewe.Rejea yaliyotendeka 2019 ndiyo uje na majibu sahihi.
 
Gentleman,
derby si ni jambo la bodi huru ya ligi, Serikali inawezaje kuingilia mambo ya michezo?🐒
Kwenye Derby ndio kuna msisimka,lakini kwenye siasa kuna masultani.
Ambao kama hujafika bei wanakuwa wakali kuliko Kaisali.Mara vuu muamala umeitika, wantakupamba kwa kila hali.

Nadhani we the people isiwe we the party ndio tutaenda vizuri Kidemokrasia.
Ni haramu kumuabudu mtu,sio Mungu.
Turudi kwa Mtikila kuwepo na wagombea binafsi.Mgombea binafsi atakuwa huru sio eti chama cha maandazi mwenyekiti hataki barabara ijengwe kwa kuwa hajakaribishwa "hakupewa bahasha"
 
Back
Top Bottom