Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 36,155
- 30,829
Kwasababu bado dhana na hali ya kususia imetanda miongoni mwa vyama vya siasa, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa ambavyo vimeamua kujitenga na michakato ya kidemokrasi na kujikita kutafuta pesa za matumizi ya viongozi wa vyama hivyo hususani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025.
Bilashaka yoyote hiyo inamaanisha katiba mpya sio kipaumbele cha wananchi bali pesa ndio kila kitu kwa baadhi ya vyama vya siasa, na kwahiyo hakuna haja kwa serikali kuanzisha mchakato wa gharama kubwa ambao mwisho wa siku unaishia njiani na hatimae kua hasara na mzigo kwa wananchi walipa kodi wa Tanzania.
Waliopewa dhamana ya uongozi wa taifa, ni muhimu zaidi wakajikita kutekeleza wajibu wao wa kikatiba wa kuwafanyia kazi waTanzania wote. hakuna sababu ya maana hata moja kuanzisha mchakato wa katiba mpya katika wakati wowote ujao, kwasababu baadhi ya vyama vya siasa wamejipanga kuvuruga michakato yote ya kidemokrasi ikiwa ni pamoja na uchaguzi mkuu kama walivyovuruga mchakato wa katiba wa awali kwa maslahi yao binafsi.
Kwa maoni yangu,
Serikali ijikite katika kuwatumikia waTanzania na kutimiza vipaumbele vya mahitaji yao ya kila siku kama vile maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, nishati, miundombinu n.k, kuliko kufuja pesa kwenye mambo ambayo si kipaumbele cha wananchi.
una maoni gani?🐒
Mungu Ibariki Tanzania