VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Uvumi unakolea kuvuma. Uzushi unakolezwa na kuchagizwa kwa picha tengenezwa na halisi. Ukaribisho usio na vitisho unakaribia mwisho. Ni kumhusu Waziri Mkuu Mjiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Lowassa anatajwatajwa kama aliye njiani kujiunga na CHADEMA na baadaye kupeperusha bendera ya UKAWA kwenye ngazi ya Urais hapo Oktoba. Yaani,Lowassa ataingia kilingeni kupambana na CCM yake!
Lowassa,ni jana tu, amekaribishwa UKAWA na kuanza kusafishwa. Ikasemwa kuwa Lowassa ni msafi na aliyeponzwa na mfumo. Kauli mbilimbili toka kwa watu wawili: wale na hawa. Lowassa amesemwa,ametajwa na hata kutengenezewa picha za kikaoni na CHADEMA. Yeye amekuwa kimya. Hakuzungumza wala angalau kujitokeza hadharani. Amekuwa kimya hadi anatisha.
Ukimya wa Lowassa una mitazamo miwili. Wa kwanza, Lowassa anajipanga ili apangike na ndipo afunguke. Afanye kweli. Hapo uzushi utakuwa ukweli. Yale ya 'lisemwalo lipo...kama halipo laja' yatatimia. Huo ni Upande A. Mtazamo wa pili,upande B, ni kuwa yote yanayosemwa na kuandikwa ni uongo mtupu. Ndiyo maana Lowassa anajinyamazia tu akiwacheka wasiochoka kuhangaika!
Ikiwa kweli, yaani ukijidhihiri upande A, Lowassa atakuwa ni jiwe sambaratishi. La kuogofya. Atasambaratisha UKAWA/CHADEMA na CCM-anapokwenda na anapotoka. Wapo wanachama wa pnde hizo watakaohama. Wapo watakaobaki kimwili lakini kiakili wakiwa wametoka au kuwemo na Lowassa. Lowassa atachochea uhamaji au usaliti CCM. Wanaomkubali wanatamani kufika naye mbali. Hawajakata tamaa. Watahama naye CCM au kubaki kupika chakula humo na kumpelekea Lowassa. Na kura zitapigwa kwa Lowassa.
Atakapohamia hakutabaki salama. Wapo watakaomkimbia au kubaki naye kinafiki. Hawa ni wale wanaoamini kuwa Lowassa si msafi na hafai. Wa aina hii watasusa au kusuasua directly au indirectly. Kura zao zitapepea. Atakapohamia napo patatikisika na kusambaratika. Maji yatachafuka katika bwawa atakalotoka na hata kwenye bwawa atakaloingia. Mambo hayatabaki hivi hivi.
Hakika, Lowassa akihamia UKAWA atakuwa jiwe sambaratishi. Lakini, ijulikane ya kuwa CCM iko imara na tayari kwa mpambano wa Oktoba!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Aione: Kiherehere, Tetty