Ikiwa kweli: Lowassa atasambaratisha

Ikiwa kweli: Lowassa atasambaratisha

Kwanza siamini kama ni kweli CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi ya hovyo kama hayo lakini ikiwa ni kweli basi ni kama nashuhudia anguko la CHADEMA siku za usoni! Na hata Lowassa akismama kama mgombea urais na akashinda, serikali yake haitakuwa na legitimacy ya kupambana na ufisadi kama wapenzi wa CHADEMA wanavyoaminishana! Mtu aliyezungukwa na Chenge, Rostam na Karamagi atapata wapi ujasiri na moral authority ya kupambana na ufisadi! Watu wazima bila aibu eti wanatamka hadharani kwamba Lowassa ni msafi kwa kuwa hajafikishwa mahakamani! Ni hoja gani za hovyo kama sio za kipumbavu kama hii?!! Ina maana Rostam Aziz nae ni msafi? Chenge nae ni msafi? Karamagi nae ni msafi? Kikwete nae ni msafi? Anna Tibaijuka nae ni msafi? Mkapa nae pamoja na kuanzisha kampuni Ikulu na kujiuzia Kiwira nae ni msafi? Huyu na yule nao ni wasafi? Ni nani miongoni mwao amewahi kufikishwa mahakamani ikiwa hoja ni kwamba hajafikishwa mahakamani?

It's very unfortunately ikiwa haya yasemwayo yatatimia basi moja kwa moja CHADEMA itakosa uhalali wa kupambana na ufisadi na kimsingi, itakuwa imewasaliti wale wote ambao waliungana na CHADEMA kwa kuamini wana nia ya dhati! Rais ni nafasi kubwa sana kwenye taifa ambalo katiba yake imetoa madaraka makubwa mno kwa rais! Hivi Lowassa ndo ameshakaa pale Magogoni, ni nani mwenye ubavu wa kumdhibiti? Mbowe?

I am afraid habari hizi zikiwa za ukweli, si tu kwamba CHADEMA itakosa moral authority ya kuusemea ufisadi bali watakuwa wamekiweka rehani chama mikononi mwa wapambe wa Lowassa waliopo CCM na wale wanaomfadhili! Na ikitokea amesimama na bado CHADEMA ikashindwa, basi huo utakuwa ndio mwanzo wa anguko la CHADEMA kwa maana kitakachobaki ni kulaumiana kwa kuamini, kama si kumkaribisha Lowassa, si ajabu wangeshinda! Lawama zitakazokuja kutokana na ukweli kwamba wapo wana-CHADEMA mahiri ambao hawatakubaliana na upuuzi huu na hivyo kuamua kuachana na chama! Na ikiwa watashinda, CHADEMA itakuwa imetekwa na wana-Lowassa... hapatakuwa na mwenye ubavu wa kumtimua rais wa nchi, rais mwenyewe mwenye kariba ya Lowassa! Tusije kushangaa tukakuta akina Mbowe wanabadilika kuwa wapangaji kama ilivyokuwa kwa akina Mabere Nyaucho Marando mbele ya Mrema!!! Na hakuna kosa kubwa kama kumlinganisha Lowassa na Dr. Slaa kwamba hata Slaa alitoka CCM na baadae akaja kuisumbua!

Dr. Slaa ingawaje alitokea CCM lakini alidumu sana madhabahuni kuliko ndani ya CCM! Huyu hakuwa na watu CCM tofauti na Lowassa ambae ameanza kuusaka uraisi kupitia CCM kwa takribani miaka 25 sasa! Watu wa Lowassa alionao CCM ni watu wenye nguvu kwenye siasa za Tanzania! Mbowe na wenzake kamwe hawatakuwa na ubavu wa kuwadhibiti watu kama hawa! Miongoni mwa wagombea wote ambao walijitokeza CCM, sidhani kama kuna mgombea ambae ungemlinganisha na Lowassa kuwa kwake ndani ya chama! Wakati kuna kila dalili Dr. Slaa alitoka CCM kv alitaka kuwahudumia wananchi wake kwa namna yoyote ile, lengo la Lowassa ni kuupata urais kwa namna yoyote ile.... hizi ni two different goals!

But lastly, CCM sio wapumbavu... wanajua wanachofanya! Si kwamba hawakufahamu madhara ya kumkata Lowassa... lazima walikuwa na Plan B! Watu wasipoangalia itakuwa ni kama samaki aliyerushiwa chambo bila kufahamu chambo ile imeficha ndoana!!

Jipigeni kisu wenyewe na kama Lowassa atasimama kwa tiketi ya urais basi waombee wasishinde urais ila tu asababishe kupata wabunge wa kutosha manake akishachukua urais, balaa lake litakuwa si dogo! Na kama watafanya uendawazimu wa NCCR wa kumpatia na uenyekiti kabisa, then nitatangulia kusema R.I.P CHADEMA!

Kwa vyovyote vile hali ya kisiasa nchini haitakuwa kama ilivyo, inabadilika. Lowassa akitoka ndani ya CCM na kwenda upinzani na kama ataendelea ku 'command' heshima na mashabiki aliokuwa nao itabadilisha kabisa mfumo iwe ameshinda urais au hakushinda. Nafikiri na natumaini kuwa kuanzia uchaguzi huu na hasa baada ya uchaguzi tutaanza rasmi mfumo wa vyama vingi - yaani mfumo wa chama dola utaondoka.

Unayoyasema yote yana ukweli na tumeyaona nchi nyingi na hasa jirani zilizopitia huko tunakokwenda; wapinzania wanaungana kwa sababu wana 'common enemy' lakini baada ya hapo akishatoka wanarudiana wao. Kinachotokea tu ambacho ni kizuri ni kwamba mabadiliko hayo hayarudi nyuma yanasonga mbele. Kwenye suala la ufisadi katika siasa zetu, wewe mwenyewe umethibitisha katika andiko lako wote uliowataja kama mafisadi wanendelea kututawala na hata huyo aliyeko sasa kwa matarajio naye unasema ni fisadi! Kwa hiyo haina tofauti iwe fisadi anatawala kupitia chama tawala cha sasa au cha upinzani wote ni mafisadi tu.
 
Hofu yangu ni kwamba, mtu akiingia kwa ajili ya kutaka cheo badala ya itikadi basi kuna hatari ya kuvurugana siku za usoni! Kwanza, ikiwa Lowassa anasimama kama Rais na kushinda, huyu tayari ana ngome ya watu CCM... kuna hatari kukawa na competition kati ya waliokipigania chama na walowezi! Sitaki kuamini kwamba Lowassa atawaamini akina Mbowe kuliko maswahiba wake wa tangu zamani! Napata shida kuamini kwamba, pale Lowassa atakapohitaji ushauri wa kisheria atakimbilia kwa Lissu kwamba badala ya kwa Chenge... kwamba, litakapokuja suala la mikakati atakimbilia kwa Mbowe kwanza badala ya Rostam!! Lowassa alionesha jeuri moja wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM! Ingawaje yeye ana tuhuma za ufisadi, lakini bado aka-opt kuwachukuwa watuhumiwa wenzake wote na kuwa team moja... ukiangalia kwa haraka haraka mtu anaweza asione tafsiri yake lakini kwa mtazamo wangu ile ilikuwa ni kuudhirihishia umma kwamba "hatutishiki na tuhuma zemu!"

Kwamba there's no difference pale nilipotaja watuhumiwa wengine wa ufisadi sikuwa na maana kumbe hata sasa tunaongozwa na mafisadi so, there's no difference! Hoja hapa ni kwamba, CHADEMA wamejipambanua kama wanaopiga vita ufisadi! Sasa leo hii ukiona Lowassa ni sawa tu kwavile hajafikishwa mahakama yoyote basi ni sawa na kusema nchi hii haina vigogo mafisadi coz' hao wote niliowataja na wengine hakuna miongoni mwao aliepata kufikishwa mahakamani lakini tunawatuhumu kwa ufisadi! Sasa je, kesho na kesho kutwa itatoka wapi moral and political authority ya kusema kwamba Kikwete, au Chenge au Rostam ni mafisadi!!??
 
Kirahisi tu ni kuwa katika Siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu. Kuvurugana ni dhairi lakini ili uweze kupata mabadiliko lazima kuwe na kuvurugana - hii ni kanuni ya dhairi. Miaka ishiri na kitu ndani ya kilichosemwa "mfumo wa vyama vingi" wakati kwa hakika tukiwa katika mfumo halidia wa chama kimoja nafkiri inahitaji mabadiliko. Kuvurugana huku kunakotokea na kutakakotokea kutatupeleka kwenye mabadiliko ya kweli ya kuwa na mfumo halisia wa vyama vingi. Kiwango cha mvurugano itategemea pia makubaliano watakayokuwa wameyawekaa hao wapinzani na hiyo kambi ya Lowassa inayoingia. Hata hivyo hao wenyewe UKAWA ti bila ya Lowassa baada ya uchaguzi wawe wameshinda au wameshindwa watavurugana! Lakini yote kutaleta mabadiliko
 
VUTA-NKUVUTE,

..hoja zako zimetulia.

..lakini sisi wengine tuliochoshwa na kiburi. dharau, na vitimbi vya ccm kwa kweli hatuna jinsi ila kukubaliana na ukawa.

..tukiweza kuwatoa ccm madarakani hao wengine hawatatupa shida kuwaondoa ikiwa wataharibu kazi. Hayo ndiyo matumaini yangu.
 
Last edited by a moderator:
Maskini Slaa anatia huruma sana. Hivi kwa sasa kuna haja ya Slaa kuendelea kuwa na mlinzi tena! maana hana thamani tena!
 
Kirahisi tu ni kuwa katika Siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu. Kuvurugana ni dhairi lakini ili uweze kupata mabadiliko lazima kuwe na kuvurugana - hii ni kanuni ya dhairi. Miaka ishiri na kitu ndani ya kilichosemwa "mfumo wa vyama vingi" wakati kwa hakika tukiwa katika mfumo halidia wa chama kimoja nafkiri inahitaji mabadiliko. Kuvurugana huku kunakotokea na kutakakotokea kutatupeleka kwenye mabadiliko ya kweli ya kuwa na mfumo halisia wa vyama vingi. Kiwango cha mvurugano itategemea pia makubaliano watakayokuwa wameyawekaa hao wapinzani na hiyo kambi ya Lowassa inayoingia. Hata hivyo hao wenyewe UKAWA ti bila ya Lowassa baada ya uchaguzi wawe wameshinda au wameshindwa watavurugana! Lakini yote kutaleta mabadiliko
Si kila kuvurugana kuna maslahi and this has nothing to with urafiki na uadui wa kudumu kwenye siasa! Ile ya CUF na CHADEMA ndio unaweza kuweka kwenye kundi la "hakuna urafiki na uadui wa kudumu kwenye siasa" coz' wote wanapigania kitu kile kile.... kuindoa CCM madarakani hata kama approaches zitakuwa tofauti!!

Hili la sasa halina same cause... wakati mmoja lengo lake ni urais mwingine lengo lake ni kuiondoa CCM madarakani!! Hili la sasa ni tofauti na la CHADEMA na CUF au hata na NCCR bali linafanana na NCCR na Mrema 1995... kilichopo ni adui wa adui yako ni rafiki! Sitaki kuamini hata kidogo kwamba Mbowe anaweza kumuamini Lowassa and the opposite stands the same! Lowassa anaweza asishinde urais lakini anaweza ku-drive more and more MPs bungeni! Kwavile lengo la Lowassa sio kuiondoa CCM bali kupata urais, hata CHADEMA nao wanafahamu lengo hili la Lowassa! Akishindwa, hawatakuwa na shida nae tena sawa na ambavyo akina Marando walipokosa kuuona umuhimu wa Mrema baada ya kushindwa! Ikiwa Lowassa atashindwa, CHADEMA watahofu kuendelea kumfuga mtu ambae kila wakati watakuwa wanapata makombora kwa ajili yake!
 
VUTA-NKUVUTE,

..hoja zako zimetulia.

..lakini sisi wengine tuliochoshwa na kiburi. dharau, na vitimbi vya ccm kwa kweli hatuna jinsi ila kukubaliana na ukawa.

..tukiweza kuwatoa ccm madarakani hao wengine hawatatupa shida kuwaondoa ikiwa wataharibu kazi. Hayo ndiyo matumaini yangu.
JokaKuu

Ninakubaliana na wewe, shida ninayoiona hapa ni kuwa watu wamekosa kuwa na lengo moja, wapo wanaomtaka Rais kama Rais na wapo wanaotaka kubadili mfumo wa utawala wa kibabe, jeuri na mipasho mingi kama ulivyo wewe na mimi na wengine. UKAWA wanatakiwa wawaeleweshe wafuasi wao dhamira yao ya msingi ni ipi? maana katika UKAWA hata CCM wapo wafuasi ambao wako huko pasi kujua wako huko kwa lengo gani.

Tusiogope mabadiliko bali tuombee mabadiliko yenye amani na utulivu kwamstakabali wa taifa letu, ninaamini baada ya uchaguzi tutabaki wamoja kwa maana ya watanzania wenye itikadi tofauti
 
Last edited by a moderator:
Viongozi wetu wa CCM wameanza kuweweseka. Press ya leo imetudhalilisha

Mzee Tupatupa
 
VUTA-NKUVUTE

Mkuu hela ya Lowassainahamia kusambaratisha UKAWA kama vile ilivyotaka kusambaratisha CCM,ni vizuri wazee wa kitengo pale CCM waliliona hilo,kwa wanachosema viongozi wa UKAWA ni sawa na kula matapishi yao,yote hiyo ni tamaa,sasa nimeamini kuwa viongozi wa kisiasa wote ni wa aina moja,sijui wakati walipokuwa wanamsema Lowassa hapo mwanzo,kuna tofauti gani na hivi sasa,eti hajapelekwa mahakamani je wakati wakimsema na kumnanga alikuwa amepelekwa mahakamani?Ni ajabu akina Lipumba ,Mbowe,Makaidi,Slaa wakiwa watumwa wa pesa na utukufu wa magogoni,na hawataupata tumewashutukia.

Ww ndio umewashtukia mm sijawashtukia bado ila nimeishtukia CCM, Siasa ni mchezo, na ni nani aliyekudanganya kwamba kuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu katika siasa,Katika siasa rafki yako wa Leo ndio adui yako wa kesho na adui yako wa Leo ndio rafki yako wa kesho.Viongozi wangu Wa ukawa wanaijua siasa na wanajua upepo wa siasa unaenda vp kwasasa.Tukubali au tukatae lowasa ndio kiongozi anayekubalika kwa sasa kuliko yeyote yule,hata Leo hii lowasa angesimama kama mgombea binafsi angeshinda tuu na kutikana na hlo sio rahisi lowasa kukataliwa ndani ya ukawa,
 
Lowasa ni dhaifu ndugu ndio maana aling'ang'ania CCM,angekuwa na jeuri angetoka siku nyingi na kuanzisha chama chake,na ndio maana hata sasa kakimbilia chamakikubwa ambacho tayari kimejengwa na akina Slaa ,Lowasa hajiamini,angejiamini angeanzisha chama chake au angeenda TADEA au NLD au TLP ,mbona hakuenda huko ?anajua hana jeuri ya kufufua chamazaidi ya kutaka akute ''ugali'' mezani,angekuwa na jeuri angemwiga raisi Uhuru Kenyata ambaye alianzisha chama chake mwenyewe ndani ya mwezi mmoja,utanikumbuka Lowassa ataiota tu Magogoni au ataenda tu kunywa chai na si kwenda kufanya maskani,muda utafika.
 
Back
Top Bottom