Ikitokea vyama viwili tofauti vikashinda Bara na Visiwani, je Tanzania itabadili jina?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Ni wachache mno wanaojua kuwa hii nchi ama hili Taifa letu la Tanzania hapo mwanzo lilikuwa linaitwa Tanganyika mpaka hapo mwaka1964 Tanganyika ilipoungana na Zanzibar na kuunda Taifa ama nchi ya Tanzania.

Watanganyika wakawa wepesi kulisahu jina lao la asili la Tanganyika lakini kwa wazanzibar ikawa ngumu...Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere alijitahidi sana kwenye hilo na sisi tulikuwa tukiita Zanzibar Tanzania visiwani

Viongozi waliofuatia hili hawakulipa uzito na taratibu Zanzibar ikaanza michakato ya kuwa taifa kamili.,..kwa wasiofahamu ili mahali pajulikane kama taifa ama nchi kamili inahitaji mambo kumi makuu.

1. Mipaka
2. Uongozi kamili
3. Wimbo wa taifa
4. Bendera ya nchi
5. Chombo cha uwakilishi wa wananchi(bunge)
7. Chama cha siasa
8. Jeshi
9. Sarafu
10. Mgawanyiko wa kiutawala.

Kwasasa ili Zanzibar iwe dola kamili inahitaji kipengele kimoja tu SARAFU. Wenzetu walituzidi akili pamoja na udogo wao..kamwe hawakukubali jina jipya la Tanzania lifunike la zamani la Zanzibar lililotoholewa toka neno Zenjiber, .kwahiyo basi ikitokea kukawa na matokeo tofauti ya ushindi wa vyama kwenye uchaguzi mkuu na muungano ukavunjika ama kuunda setikali tatu kwa upande wa Jina Zanzibar hawataathirika na chochote.

Tatizo kubwa ambalo ni vigumu mno kulimeza ni kama sisi wa bara tutakubali na kuweza kulibadili jina letu pendwa la Tanzania kuwa Tanganyika!
 
Ukionea aibu asili yako ni utumwa kichwani. Hii inawasumbua sana wa Tanganyika kulionea aibu jina letu la asili.

Lakini ninachojuwa ni kuwa siku moja Zanzibar itaondoka katika muungano huu. Ipo miungano mingi ya aina hii iliyovunjika. Mifano Yugoslavia, USSR, Senegambia etc. Kuna kizazi kitakuja kuhoji uhalali.
 
Mshana Jr,

Ikitokea hivyo kutakuwa na options mbili in the long run.

1. Muungano utakuwa wa serikali tatu lakini hautadumu miaka mitano.

2. Muungano utakuwa historia na Zanzibar itaenda kuchukua nafasi yake UN.
 
Tutaendelea na jina hilihili TANZANIA!

ambaye anaushahidi kuwa neno tanzania lilizaliwa kutoka maneno mawili tanganyika+zanzibar auweke hapa. Halafu njia iliyotumika kuliunda ilkkuwa?
 
Hili swala nilisema kuwa ndio sababu CCM bara inailinda CCM Zanzibar kufa kupona. CCM bara ikiamua kuiacha CCM Zanzibar ijipiganie, Upinzani lazima uchukue nchi, na ukichukua nchi wakati bara imebaki CCM hakuwezi kuwa namaelewano.

Huu Muungano mnauona wa Serikali mbili kiuhalisia ni wa Serikali Moja. Lisemwalo na JMT, SMZ haiwezi kwenda kinyume.
 
Tutaendelea na jina hilihili TANZANIA!
ambaye anaushahidi kuwa neno tanzania lilizaliwa kutoka maneno mawili tanganyika+zanzibar auweke hapa. Halafu njia iliyotumika kuliunda ilkkuwa?
UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru.

Hata hivyo, katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine, michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye historia hizo.

Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa shuleni.

Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.

Lakini ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.

Ilikuwaje?

"Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo," anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza:

"Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichuka karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote."

"Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya," anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.

Kupata jina Tanzania

Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.

"Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,"anasimulia Dar.

Anabainisha kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika yanaishia na IA mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia, Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.

"Nilituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani," anasema Dar.

Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.

"Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda,

"Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini, nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi sana," anaeleza.

Tuzo

Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.

Pamoja na kuibuka mshindi wa ubunifu huo na hadi leo jina la Tanzania alilolibuni yeye linaendelea kutumika, lakini Dar anadai kuwa mchango wake huo kwa taifa ni kama hautambuliwi na Serikali imemsahau katika kuandika historia ya taifa la Tanzania.

"Sijui kwa nini sitambuliwi tangu wakati huo? Hakuna chochote kinachoelezea uhusika wangu katika kupata jina la Tanzania na ukiwauliza watu, wengi watakwambia ilikuwa ni Nyerere aliyeleta jina Tanzania, hii inaumiza," anasema akilalamika.

Tanzania ya sasa

Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere, Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani.

"Ni kama imepita miaka mingi sana tangu kifo chake. Watanzania wamesahau kila kitu alichokiota Mwalimu Nyerere. Nakumbuka moja ya vita kubwa aliyopigana ni dhidi ya rushwa, yeye aliichuki rushwa lakini kwa sasa, rushwa imekua kama ndiyo tafsiri ya maisha ya Tanzania. Hakuna kitu kinachoweza kufanyika kwa urahisi hata kama ni haki ya mtu, bila kutoa rushwa," anasema.

Anaongeza kuwa: "Mwalimu Nyerere alikua ni rafiki ya baba yangu na walikua wakionana na kuongea, nakumbuka siku moja kulikuwa na sherehe nyumbani na kwa kuwa tulikuwa watoto, nilimhudumia chai Mwalimu.

"Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumuuliza baba yangu; Lini Malaria itaisha nchini hii? Baba alimjibu kuwa, kamwe malaria haitaisha ikiwa hakutakuwa na kujitolea kwa kila mmoja wetu, bila kumtegea mwengine," anasema.

Katika kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Dar anaishauri Tanzania iendeleze misingi ya maisha ambayo Hayati Mwalimu Nyerere aliisimmamia, ikiwamo umoja na mashikamano, ili kuondoa tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri.

"Tunaona namna ambavyo matajiri wanendelea kuwa tajiri zaidi, wakati maskini wanazidi kudidimia. Kama kungekuwa na ushirikiano kati ya watu hawa wawili, tofauti kati yao ingekuwa ndogo au isingekuepo kabisa," anaeleza.

Anashauri pia kuwepo na sanamu za utambulisho ya Baba wa Taifa kila mahali, ili kulienzi jina lake liishi milele.

"Kwa ninavyomjua Mwalimu natamani jina lake liishi milele na litangazwe lijulikane dunia nzima," anasema.

Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar.

Dar ni baba wa mtoto mmoja, ambapo kwa zaidi ya miaka 40 sasa amekuwa akiishi nchini Uingereza alikoenda kwa ajili ya kusoma kabla ya kuwa raia wa nchi hiyo.

Mbunifu huyo wa jina la Tanzania ni Mhandisi wa Masuala ya Redio, kazi anayoifanya nchini Uingereza, akieleza kuwa katika kuienzi nchi yake, nyumba yake iliyopo mjini Birmingham, ameipa jina la Dar es Salaam, ikiwakilisha ubini wake, pamoja na Jiji la Dar es Salaam
 
Tutaendelea na jina hilihili TANZANIA!
ambaye anaushahidi kuwa neno tanzania lilizaliwa kutoka maneno mawili tanganyika+zanzibar auweke hapa. Halafu njia iliyotumika kuliunda ilkkuwa?
Huyu ndie mbunifu wa jina TANZANIA

FB_IMG_15974779704653072.jpg
 
Muungano upo kwa mujibu wa katiba, taratibu za kuvunja muungano zinaeleweka theluthi mbili bara na theluthii mbili visiwani.
 
Back
Top Bottom