ulaya12
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 834
- 908
Nimewaza hili jambo kuwa kama ikitokea umebaki peke yako Duniani utafanyaje,yaani unaamka asubuhi mkeo na watoto huwaoni,majirani huwaoni unakuta milango yote iko wazi,unachanganyikiwa unaamua kwenda mitaani nako pia unakuta Maduka yako wazi ila hakuna hata mtu 1,unajaribu kuwapigia Simu ndugu na jamaa lakini simu haiendi ,unawasha TV labda unaweza kupata taarifs yoyote kuhusu kilichojiri lakini haiwaki,unaamua kwenda Polisi ukatoe taarifa nako unakuta milango iko wazi hakuna hata mtu 1,unazidi kuchanganyikiwa ila bado unajipa matumaini kuwa unaweza ukakutana na watu au mtu wa kuweza kujadiliana kuhusu hii hali iliyotokea ndipo unapata wazo uende Benk kuu ukijipa matumaini kwamba pale piga ua masaa 24 Askari hawakosekani pale lakini unafika unakuta milango iko wazi ila hakuna Askari yeyote walala hakuna dalili ya kuwepo mtu,hatua ya mwisho unaamua kwenda Kwenye Nyumba nyeupe pale Magogoni ukiwaza kuwa wale wazee wa kazi huwa hawakosekani piga iwe jua iwe mvua lakini unafika unakuta Geti liko wazi na pako kimya humuoni mtu yoyote.hatimaye umechoka huna lakufanya unajipa matumaini uende Ubungo pale utakuta wasafiri,lakini unafika unayakuta Mabasi yamepaki ila humuoni hata mtu1na unakata tamaa kuwa umebakia peke yako sasa hadi hapo sijui utafanyaje.