Ikitokea CHADEMA wakatangaza kuahirisha UKUTA kesho, je watatoa sababu gani? Na je wataeleweka?

Pasco unataka kusema Ukuta haujafanyika? Ukweli ni kuwa Ukuta tayari umefanyika kwa zaidi ya 90% kwa kumshirikisha mheshimiwa Raisi, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, makamanda wa Polisi na wanaccm wote. Pia viongozi wa dini na Msajili wa vyama wote wameshiriki. Kipengele kilicho baki ni kidogo tuu cha kuingia barabarani, lakini nacho kimetimizwa kwa kiwango fulani kwa Polisi nchi nzima kutoka na silaha zao na kuzunguka mijini na jua kali huku vitambi vyao vikitoka jasho.
Hata vyombo vya habari mashuhuri duniani vimezungumzia kwa kina kuhusu Ukuta. Jee malango ya moyoni na akilini hayajatimia? Lengo lilikuwa kuwaambia watawala kuwa kuna ukiukaji wa sheria na katiba, ujumbe umefika hata kama umejibiwa kwa ubabe na vitisho. Na ni mjinga tuu ndiye anaweza kuambiwa jambo na asitafakari kwa vile ana upanga mkononi.
Jambo ambalo Chadema wamewaweza watawala ni kuwaambia KUANZIA TAREHE 1/9 maandamano yataanza na kuendelea hivyo hata wakisema tumeahirisha hatuanzi tarehe hiyo nina hakika kuna watu wanaweza kufa kwa pressure kwani walishajiandaa na vifaa vyao kupambana tarehe hiyo na tension itakuwa kubwa tukio hilo lisipofanyika.
Ni aibu kujiandaa kimapambano kwa raia wako utadhani tumeambiwa Malawi wanatuvamia siku hiyo.
 
ImageUploadedByJamiiForums1472587915.245498.jpg

Kama ni midundo ya Ukuta wameshaicheza sana na sasa wamechoka hata wakiachwa sawa tuu
 
Kwani UKUTA wa chadema au wa Watanzania wote? Nchi hii yetu sote madhila hawayapati Chadema tu. Kususia au kukosa kuhudhuria maadamano ya UKUTA ni sawa na kuisaliti Tanzania yetu. September 1 UKUTA upo palepale
 
Sehemu ambazo ambazo ukawa wana nguvu ni dar-es-salaam, mbeya, arusha na kilimanjaro.... Lakini huku kwingine kulikobakia hakuna mtu mwenye habari nao....
Mtwara ndo kabisa, hawawezi kujaribu....
Kukifanyika maandamano maeneo hayo tu nchi inaanguka Misri ilikuwa cairo na alexadria na utawala ukaanguka so usidharau
 
Kwani UKUTA wa chadema au wa Watanzania wote? Nchi hii yetu sote madhila hawayapati Chadema tu. Kususia au kukosa kuhudhuria maadamano ya UKUTA ni sawa na kuisaliti Tanzania yetu. September 1 UKUTA upo palepale
Mimi kama mwananchi wa kawaida sioni udikteta wa Magufuli zaidi zaidi naomba azidishe ukali kidogo ili mafisadi yaendelee kulia lia.. Sasa nikaandamane ili nipate nini cha kunisaidia kwenye maisha yangu zaidi ya ushabiki wa kipuuzi tu huko.
 
We unataka wafanyeje? waombe kibali wakati polisi wamekataza shuguli za siasa, mikutano na maandamano ya amani? Unavyofikiri wewe chadema waende mahakamani kutafuta haki hiyo wakati ccm wanayo free of chaqge. Una uhakika mahakama itaenda tofauti na ccm na rais wao wanavyotaka?
 
Itaelezwa kuwa Chadema imepata taarifa ya kiinteligensia ya kilichopangwa kufanywa na jeshi la Polisi siku hivyo, hivyo baada ya kukijua, ni kichaa tuu ndio angeendelea kuwashawishi watu waandamane!.

Hili litakuwa goli la kisigino & wananchi watawaelewa na kukubaliana nao.
 
We unataka wafanyeje? waombe kibali wakati polisi wamekataza shuguli za siasa, mikutano na maandamano ya amani? Unavyofikiri wewe chadema waende mahakamani kutafuta haki hiyo wakati ccm wanayo free of chaqge. Una uhakika mahakama itaenda tofauti na ccm na rais wao wanavyotaka?


Mbona Domo kaya mnamsifia kushinda kesi kila siku?
 
Huyu jamaa mjanja sana, baada ya kukutana na mfalme kisha kuteta mawili matatu kwa lugha ya mfalme sasa anashusha uzi wenye maswali kupima upepo ili mfalme ajue atafanya nini. Kazi ipo.
 
Wanabodi,

Leo ndio siku ya mwisho kwa Chadema kutuma maombi rasmi ya kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kuhamasisha UKUTA, wakati tukisubiri taarifa rasmi ya Chadema kuhusu maandalizi ya mwisho, ambapo jeshi la polisi litatangaza rasmi kama limeombwa vibali na kama limekubali au kukataa, Chadema nao kuna taarifa muhimu inatolewa kesho.

Jee ikitokea Chadema wakaitisha Press Conference ya kusitisha maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima. Jee watakuja na sababu gani? !, na jee wataeleweka? !.

Hili likitokea, zitatolewa sababu za msingi sana ikiwemo mkutano wa Eddo na Magufuli, Mkutano wa Msajili, vitisho vya polisi, na hoja kubwa zaidi ni Chadema kuuthibitishia umma kuwa sio chama cha shari, fujo, vurugu bali ni chama cha heri, kinachohubiri upendo, amani na utulivu ikiwemo utii wa sheria bila shuruti na pia kinathamini uhai na uhuru wa watu wake kuliko kitu kingine chochote!.

Itaelezwa kuwa Chadema imepata taarifa ya kiinteligensia ya kilichopangwa kufanywa na jeshi la Polisi siku hivyo, hivyo baada ya kukijua, ni kichaa tuu ndio angeendelea kuwashawishi watu waandamane!.

Hizi harassment za jeshi la polisi kwa viongozi wa Chadema ndio dalili ya awali ya kilichopangwa, hivyo kwa kuwapenda zaidi Watanzania na kutanguliza mbele maslahi ya taifa, hivyo wameamua kuyaahirisha kwa muda maandamano hayo na kutoa nafasi kwa meza ya mazungumzo! .

Jee utakubali maandamano yasitishwe kwa sababu zozote zile? !.

Pasco

Yaahirishwe tuuu! Kwani dhana ya UKUTA imeshaeleweka na ni wao wenyewe wameicheza ngoma bila kujua! This is called PUBLICITY IN THE MAKING! Akili ndogo haiwezi kuitawala kubwa kamwe! Asante kwa waliosaidia kuutangaza UKUTA bila wao wenyewe kujua wamesaidia kampeni hiyo kueleweka mpaka vijijini, kuliko hata waasisi wa UKUTA. HAahahahhahhaha.
 
Huu uzi una uchonganishi wa kitoto. Unataka kuwaona chadema kesho barabarani iliweje wakati polisi na bunduki kubwa na wanajeshi watakao sambaa kufanya 'usafi' wamesambazwa nchi nzima?

Wakati huo hata kamati kuu chadema hairusiwi kufanya mkutano hata itoe press nini kifanyike. Acha uchochezi na mawazo ya kitoto, lla pia mkitaka kuona hicho mnachotaka kuona mtakiona si mbali sana. mtoto akililia wembe mpe (japo siamini ktk hili)
 
Back
Top Bottom