Ikifika 40 years kama hujafanikiwa ni ngumu kutoka...

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,530
Hivi inaweza kuwa kweli ukifika umri wa 40,na hakijaelweka(kufanikiwa kimaisha) ni ngumu kufanikiwa(utajiri) baada ya apo?karibuni kushare .
 
Ni ngumu kweli! Labda uokote fuko la hela njiani. Kwanza umri huo inatakiwa uwe ushaanza kula bata siku nyingi sio kuhustle
 
Nani amesema hayo? Kwangu mimi ni self belief tu. Ukiamua kufanikiwa utaweza kufanikiwa. Mwisho wa siku ni akili yako unaitumiaje kwa wakati huo....just out of curiosity, kwani Mengi na Mzee Ndesamburo wameanza kufanikiwa lini?
 
Nimekuwa specific kwa utajiri tu.Kufanikiwa kunajumuhisha mambo mengi ila nimelenga kipengele kimoja tu cha utajir.
ndugu yangu kama kufanikiwa nikuwa tajiri kuna source nyingi sana za kupata utajiri!
  • self made( mtu yeyote anaweza kujituma akazipata haijarishi umri)
  • illegal(mtu wa umri wowote anaweza akafanya illegal deal akatoka)
  • inheritance( ata mtu wa miaka hamsini anaweza kurithi mali za nduguze akawa tajiri)
  • luck( babu wa miaka sabini anaweza akacheza michezo ya kubahatisha,kamari akawa tajiri)
  • talent( mungu anatoa kwa wote haina umri hiyo kama kuwa musician,commedian etc)
sasa mpendwa umeshaona weakness ya point zako

ila kwangu mimi binafsi mafanikio nikuwa na amani moyoni! ndio kitu muhimu sana,sijui kwa wengine ngoja tusubiri waje wajuaji watatujuza vizuri
 
hujafa hujaumbika, never generalize. kila mtu ana jinsi ya kuchanga karata, na hii inajumlisha muda, wengine wanaweza kufika umri huo wakakata tamaa- lakini zaidi tuangalie stages. kama mtu amekuwa na juhudi tangu mwanzo e.g amesoma vizuri tu ameelimika, ni mambo tu hayajipi mapema na sio mlevi labda, sio mtapanyaji, huyo one day anaweza kutoka, wala usishangae hata akifika 60 anaweza ibuka ukashangaa. kuna vitu lukuki vya kuanalyse, unaweza kujaza kurasa chungu nzima kuelezea hili jambo, mazingira hayafanani. wengine wanapita short cut (wezi, michongo n.k), wengine wako slow but sure, wengine tough ways (mfano kilimo n.k), wengine huwezi amini, hawaibi hata kidogo, lakini ni kwa njia rahisi tu cha cha, unamkuta juu. kuna wengine wanaletewa hesabu wakiwa juu ya stuli wakipata, or kitandani wamepumzika. wengine wanatoka jasho ndipo wapate walao kidogo, juhudi inahitajika zaidi, bila kudespair.
 
hapa bongo mtu mwenye form iv au std 7 akiwa na TOYOTA Opa na kupanga upande mzima wa nyumba plus flat screen anakuwa amepass kuwa na mafanikio

Kumbe ndo hivyo?

Ndo maana nikauliza hapo juu, kufanikiwa ni nini na utajiri ni nini? Tusije kuchanganyiana mambo kabla ya kutoa basic definitions kwanza.

Watu walioendelea washaacha kufikiria utajiri kama material possesions, wanafikiria sana mambo ya experiences na responsibility, mambo ya kuwa na dunia safi zaidi/ kutunza mazingira, mambo ya kutumia muda vizuri, hususan na familia etc.

Lakini hawa ni hao ambao washapata wasaa wa kubadilisha mboga na flatscreens na ku flip vijumba na vigari na kusomesha watoto shule nzuri tayari.

Kwa sie naona bado tupo kwenye vi flatscreen na kupanga upande na kuendesha vi-Toyota tu?

Ted Turner, bilionea mkubwa Marekani ambaye alianzisha CNN na kati ya watu wenye ardhi kwa kiasi kikubwa zaidi Marekani, aliulizwa kuhusu maisha yake jambo ambalo angetaka kuboresha na analo regret, pamoja na utajiri wake wote, maisha yake ya ndoa yalikuwa na matatizo sana kiasi akasema angependa kama angekuwa na ndoa nzuri.
 
original.jpg
Bibi huyu yuko mara mbili ya miaka 4o ameshinda lotto na kuwa tajiri
Kwa hiyo dhana ya umri na kipata vitu viwili tofauti kabisa
 
Hata biblia imesema "wazee" wataota ndoto na "vijana" wataona maono.Umri wa maono ya kufanikiwa
ukishapita kinachobaki ni kuota ndoto tu za kufanikiwa wakati umeshachelewa.

miaka 40 uzee bado kabisa
 
Back
Top Bottom