Hizo simu zipo kibiashara zaidi, mfano c8 kiumbo na kamera kidogo imeboreshwa lakini tatizo lake ram ndogo na inataka network full ukiwa mbali kidogo na mnara haivumilii hata kidogo. Na J8 nayo iko vizuri kwenye RAM na mziki lakini ukiiangalia kwa undani hii cm touch yake sio bora km ya c8, alafu screen yake haijatulia sana ktk ubora pamoja na kupromotiwa sana. L8 imeboreshwa betri na housing yake ila shida za RAM inayo pia. W4 haina umbile zuri, na betri, camera, ram ndo haikuboreshwa ila kwa maswala ya network speed imeboreshwa sana. Nadhani kiu kubwa ya wateja ni kupata cm yenye Ram angalau GB 3, android 6.0, ukubwa screen 5.5, ROM GB 36. Betri 5000mah, nk nk. Na bei iwe nafuu