Ijue SGR, mwarobaini wa uchumi wa Tanzania

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
SGR NDIO MWAROBAINI KATIKA KASI YA UCHUMI WA TANZANIA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Standard Geuge Railway (SGR) ni reli ya kisasa ambayo hutumia umeme. Ujenzi wa reli hii ya kisasa ya SGR tunaweza kusema inakuja kama mbadala iliyoachwa na Wakoloni. Historia inasema kuwa treni tunazotumia sasa na ambazo tumekuwa tukizifanyia marekebisho mara kwa mara zilijengwa kwa mara ya kwanza hapa nchini na koloni la Wajerumani. Utawala wa Kijerumani ulianza kuwekeza nguvu katika kujenga miundombinu ikiwepo treni ili kuweza kusafirisha mazao kutoka maeneo waliyokuwa wakilima na kusafirishia manamba. Hivyo njia ya treni ililenga maeneo ambayo Ujerumani walikuwa na masilahi nayo. Ilijengwa treni ya Dar es salaam hadi Mwanza na tawi lingine likaenda Kigoma na Tanga. Njia za treni Tanzania zilianza kujengwa miaka ya 1912.

Rais Magufuli baada ya kuapishwa alitangaza kuanza kufanya mapindizi kwenye sekta ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga reli ya kisasa maarufu SGR (Standard Gauge Railway)kwa maslahi makubwa kiuchumi.

Katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya SGR awamu ya pili, Morogoro-Makutupola, iliyofanyika 14, Machi, 2018, Rais Magufuli aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania imekuwa nchi ya pekee Barani Afrika katika kutekeleza mradi huo mkubwa kwa pesa za walipa kodi(Fedha za ndani).

"Kwa bahati nzuri, hivi karibuni tulitembelewa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na alishuhudia kwamba Tanzania tumetayarisha fedha zetu wenyewe, kwa nguvu zetu wenyewe, na walipa kodi ni watanzania wenyewe, Tsh Trillioni 2.8 na kutangaza tenda zilizokuwa wazi, makampuni zaidi ya 40 yalijitokeza kuwania tenda, na bahati nzuri kampuni Kutoka Uturuki ikashinda tenda hii", alisema Mh Rais na kusema kuwa Uturuki itatoa mkopo wa masharti nafuu kwa awamu zingine za ujenzi.

Kukamilika kwa ujenzi reli hii kunategemea kuleta ahueni kwenye usafiri kwani mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa saa 3 tu ikilinganishwa na saa 5 hadi 6 zinazotumika hivi sasa kusafiri kwa gari, na pia mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa saa 9 ikilinganishwa na saa 36 anazotumia sasa kwa kutumia treni. SGR pamoja na kuokoa muda wa safari, lakini itatibu ugonjwa wa kutengeneza barabara kila siku kwani mizigo mingi itasafirishwa kwa njia ya treni na kupunguza gari kubwa za mizigo barabarani.

Mradi huu unatarajiwa hadi kukamilika kwake utatumia gharama ya dola Bilioni 1.92, lakini ndio utakuwa mradi nafuu zaidi wa reli kufanyika Afrika Mashariki. Gharama hiyo ni nusu ya ile ambayo Kenya ilitumia kujenga awamu yake ya kwanza ya reli ya hivi karibuni kutoka Mombasa hadi Nairobi. Hata hivyo mradi wa Kenya asilimi 90 ya fedha walikopeshwa na Chini na mradi wa Ethiopia uliotumia dollars bilioni 4 pia ulifadhiliwa na China.

Sera ya Taifa ilikuwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025, lakini kutoka na ukweli kuwa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kusimamia nidhamu ya serikali Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati hata kabla ya muda uliokuwa kwenye makadirio. Lakini ni ukweli kuwa nchi haiwezi kufikia ndoto hiyo bila kuboresha miuundombinu ambayo ndiyo silaha ya kukuza uchumi. Ujenzi wa reli ni nguzo kubwa katika kuchochea na kupunguza gharama na muda wa safari kwa abiria na mizigo. Mataifa yenye nguvu duniani yamejengwa na kujikita katika kuwa na miundombinu imara kwenye utoaji wa huduma za usafiri wa haraka kutoka mji mmoja hadi mwingine. Rais alitambua kuwa Tanzania haiwezi kufanya Mapinduzi makubwa ya kiuchumi bila kufanya Mapinduzi kwenye sekta ya mawasiliano.

Serikali ya Tanzania imetambua kuwa Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo ni mlango wa nchi zingine katika kupitisha bidhaa kwenda na kutoka, hii ni fursa kubwa kwa taifa kuwekeza kwenye miundombinu imara ya usafirishaji kwa wakati, salama na kwa bei nafuu. Kutokana na uwepo wa bandari ya Dar es salaam, Tanzania imekuwa inatumika kama kiungo cha nchi nyingi Afrika kwenye usafirishwaji wa mizigo. Watafiti wa mambo ya usafirishaji duniani wanasema usafiri wa reli hupunguza gharama ya bidhaa kwa asilimia kati 30% hadi 40% na huwa ni kichocheo kikubwa cha uchumi kwa kuwa gharama za usafirishaji zinapungua.

Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa SGR ni Dares Salaam – Mwanza na itaunganisha mikoa ya Daressalaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Nchi za maziwa makuu kama Uganda, Rwanda, Kongo na Burundi. Pia usanifu wa awali na upembuzi wa kina waujenzi wa Tabora–Kigoma, kaliua – Mpanda– karema ili kuunganisha na ziwa Tanganyika pamoja na nchi za kongo, Burundi na Rwanda unaendelea na ujenzi wake.

Kuna faida nyingi zinazotokana na ujenzi huu wa SGR, zipo faida zinazoonekana kwa jicho la kawaida na zipo ambazo zinaonekana kwa jicho la kiuchumi. Mpaka sasa mradi wa SGR umetoa fursa za ajira kwa jamii zipatazo zaidi ya watu zaidi ya 10,000 za moja kwa moja ambapo asilimia 94 ni Watanzania na asilimia 48 ya wataalamu pia ni watanzania hivyo mradi huu umechangia kukuza vipato vya wananchi ambao wanashiriki katika ujenzi wa huu.

Mradi wa SGR umechangia katika pato la taifa na sera ya viwanda kufanya vizuri zaidi kwa maana mradi umeongeza mahitaji makubwa ya saruji na nondo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi hivyo kuvifanya viwanda vya ndani kupata soko la bidhaa zake. Inakadiriwa kuwa takribani mifuko ya sementi milioni 9,200,000 ambayo ni sawa na tani 600 zitatumika. Pia nondo kilo milioni 115 na Mataluma 1,400,000 kutoka kwa wasambazaji wa malighafi hizo takribani 500. Hivyo ni ngumu kutenganisha ukuaji wa viwanda vyetu vya ndani ambavyo vinatoa malighafi hizi na ujenzi huu wa SGR.

Unaweza kuona kwa kipande cha Dar es salaam tu mpaka Morogoro kiasi cha nondo kilo milioni 45 za kiwango cha BS 500 kinachozalishwa hapa nchini kinatumika na saruji mifuko trakribani million 3 na kwa kipande cha Morogoro Makutupora ni Kilo milioni 70, na saruji mifuko milioni 6.4 huu ni mchango mkubwa sana katika mtandao kutoka viwandani kwenda kwenye mradi ukihusisha wadau mbalimbali kwenye ununuzi na usafirishaji ambapo itahitaji mzunguko takribani 16,000 wa saruji.

Mradi wa SGR umezalisha kazi kupitia mfumo wa Supplying chain ambapo Wafanyabiashara katika Sekta ya usafirishaji wamefaidika na mradi wa SGR, baadhi ya watanzania wamekodisha magari yao pamoja na kushiriki moja kwa moja katika usafirishaji wa vifaa na mitambo mbalimbali, hali hii imechochea ukuaji wa kipato kwa wananchi wa Tanzania.

Wakandarasi wetu wa ndani wamepata kazi za kushiriki moja kwa moja katika kujenga mradi huu mkubwa na wa kisasa.

Kwa mjibu wa serikali zipo faida nyingi zitakazotokana na SGR utakapofika wakati wa uendeshaji.Faida hizo ni za kiuzoefu kutokana na tafiti zilizofanywa kutoka nchi zilizotutangulia. Serikali imetaja moja ya faida za ukamilishwaji wa SGR ni:-

Kuongeza soko la ndani na kuimarisha Shilingi ya Tanzania (economy localization) hii ni kutokana treni kutumia umeme utakaozalishwa nchini, kama tungetumia mafuta diesel ambayo ni lazima kuagiza ingeongeza gharama kubwa kwa uendeshaji na matumizi ya akiba ya fedha za nje na Matumizi ya umeme inapunguza garama mara tatu endapo ingetumika mafuta na hali hii itasaidia kupunguza gharama kwa Nchi.

Treni za kisasa zitaweza kupunguza mrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha mizigo inayowasili bandarini kusafirishwa kwa haraka na kuingizia mapato Nchi.

Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 barabarani ya mizigo.

Reli ya Kisasa itapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya magari makubwa kwenye barabara na kupelekea kupunguza ajali na kufanya barabara kuwa njia salama zaidi ya usafiri.

Uokoaji muda wa kusafiri kwa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani maeneo ambapo reli hiyo itapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, DRC na Kenya.

Kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara na pesa hizo Serikali itaweza kuboresha huduma za kijamii kwa kutumia pesa ambazo zingetakiwa kufanya matengenezo ya barabara ambazo zingeharibika kutokana na mzigo mkubwa.

Kuongeza ufanisi wa utendaji na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari mathalani Dar es salaam – Morogoro safari kuwa Saa1 na Dakika 15, safari ya DSM – DODOMA kutumia muda wa Saa 3 na treni itakua na uwezo wa kwendea mara 8 kwa siku Dodoma.

Kupunguza gharama za usafirishaji mizigo kwa wafanyabiashara inategemewa mara mradi utakapoanza gharama za usafirishaji wa mizigo itashuka kwa asilimia 40% na kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa na ushindani.

Kuchochea uanzishwaji wa viwanda katika maeneo mengine ya nchi, mradi utatoa uhakika wa usafirishaji wa malighafi na bidhaa na kuipatia fursa nchi kwenye uwekezaji wa miradi kwani ukiondoa Daresalaam na Pwani maeneo mengine ya nchi gharama za ardhi zipo chini.

SGR inachochea uanzishwaji wa miji midogo: sehemu zinazojengwa stesheni huwa zinaongeza chachu ya uanzishwaji wa makazi ya watu kutokana kuwa na uhakika wa usafiri. Maeneo ya Soga, Ruvu na Kwala kwa Mkoawa Pwani yatumike kupanga makazi ya watu na itaiongezea reli faida ya abiria na mizigo.

Asilimia zaidi ya 70 ya Watanzania huishi maeneo ya mashambani(Vijijini) wakishiriki shughuli za kilimo. Wanahitaji kuunganishwa na masoko ya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya mazao yao wanayoyazalisha. Kwa hivyo, umuhimu wa mfumo huu wa reli sio tu kuchochea ustawi maeneo ya mashambani bali pia kusaidia kubadilisha uchumi wa Taifa.

Kadhalika, kuna uwezekano matunda yasifikie kiwango kinachotarajiwa au yakachelewa kuonekana kinyume cha matarajio ya wengi, lakini ieleweke kuwa faida yake ni kubwa kwa Tanzania ya leo na kesho.
 
Hiyo kitu ni hasara kubwa na bado pesa itahitajika ili ifike rwanda, burundi na drc ili ilete faida. Yaani hayo matirioni yangewekezewa kwenye viwanda vya 50B kila mkoa angalau viwanda 2 tungeona faida.
 
Ina faida ila sio kwa mazingira haya sasa. Baba ameanzisha miradi kabla ya kujadili na watoto. Sasa hiyo miradi itaendeshwaje na anaowatengeneza hawapo tayari.
 
Hiyo kitu ni hasara kubwa na bado pesa itahitajika ili ifike rwanda, burundi na drc ili ilete faida. Yaani hayo matirioni yangewekezewa kwenye viwanda vya 50B kila mkoa angalau viwanda 2 tungeona faida.
multiplayer effect ya hii sgr ki uchumi ni kubwa zaidi kuliko unadhani.kuliko hivo viwanda ambavyo vingehitaji management ya hali ya juu ili viwe hai,unlike sgr.tulikuwa na viwanda vingapi tz na vyote vikowapi!!??
 
... tumekuwa na miarobaini mingi mno nchi hii lakini always matokeo hasi! Unaikumbuka gesi ya Mtwara mwarobaini wa umeme Tanzania? Tupe tathmini ya hiki kilichokamilika kuliko ambacho bado.
 
Ina faida ila sio kwa mazingira haya sasa. Baba ameanzisha miradi kabla ya kujadili na watoto. Sasa hiyo miradi itaendeshwaje na anaowatengeneza hawapo tayari.
watakuwa tayari watakapo anza kuona mabadiliko ya misosi dinning.baada ya hapo wataacha dharau kwa baba yao,na kufuata nyayo za baba yao.
 
... tumekuwa na miarobaini mingi mno nchi hii lakini always matokeo hasi! Unaikumbuka gesi ya Mtwara mwarobaini wa umeme Tanzania? Tupe tathmini ya hiki kilichokamilika kuliko ambacho bado.
nilitaka kukomenti hapa.ngoja nipite tu.ila tuwaache wazee wastaafu wapumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom