Ijue sayari ya Jupiter kwa uchache

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
1: Sayari ya Jupiter ni sayari kubwa kuliko zote kwenye mfumo wa jua.Kwa makadirio ina upana kwa kilomita 142,000 kutoka kwenye Equator yake.Sayari ya jupiter ni kubwa kiasi ambacho unaweza kuzikusanya sayari zingine 7 zilizobaki na kuziingiza zikaenea ndani yake. Kwa dunia yetu, inaweza kuingia mara 1,300 ndani ya Jupiter. Kwa maana ingine, ili upate ukubwa wa sayari ya Jupiter basi kusanya dunia 1,300 ziunganishe kwa pamoja. Kama Jupiter ingekua na ukubwa mara 80 zaidi ya hivi ilivyo basi ingekua na sifa ya kua nyota.

2: Jupiter ni sayari ya tano kwenye mfumo wa jua. Jupiter inasifika Kia sayari ang'avu nyuma ya Venus. Kutokana na sifa hii, sayari ya Jupiter inaweza kuonekana kwa macho kutoka duniani pasipo na shida yoyote.

3: Jupiter ni sayari ilioundwa kwa gesi (Hydrogen na Helium).Pia Jupiter inasifa za kujizungusha yenyewe (Rotation) kwa kasi sana kuliko sayari nyingine yoyote kwenye mfumo wa jua.Inachukua masaa 10 tu kwa sayari ya Jupiter kumaliza mzunguko wake mwenyewe huku ikichukua miaka 12 kufanya mzunguko wake kati jua (Revolution)
Nb: Dunia inajizungusha (Rotation) kaa masaa 24 huku ikizunguka jua kwa siku 365.Kwa maana ingine, mwaka mmoja katika sayari ya Jupiter ni sawa na miaka 12 duniani
.
4: Jupiter inasifika kwa kua na kani kubwa ya mvutano (Gravitational force) kuliko dunia kwa zaidi ya 2.4 zaidi ya dunia.Kwa maana kama mtu ana uzito wa 100kg duniani,basi kwenye sayari ya Jupiter atakua 240kg.

5: Jupiter inasifika kwa kua na nguvu kubwa ya sumaku (Magnetic fields) hii no kutokana na mikusanyiko wa gas. Duniani, hydrogen ipo kama gesi lakini kwenye sayari ya Jupiter, hydrogen ipo kama maji.Hii ni kutokana na pressure kua kubwa. Kwa kadri ambavyo anizunguka, sayari ya Jupiter hua inanasa na kukusanya viwawe vidogo vidogo vinavyopita pembeni yake.

6: Jupiter ina jumla ya miezi 79 na zaidi na mine kati yao ni mikubwa kuliko hata dunia.Miezi mikubwa ya Jupiter ni pamoja na Europa,Callisto, Ganymede na Io. Kati ya miezi hiyo ni mwezi mmoja tu (Europa) inayozaniwa Luna uwezekano wa mwanadamu kuishi. Pia inazaniwa ndani ya Europa kuna unyevunyevu (maji) ambayo ndani yake kuna viumbe hai kama samaki nk.

NB: Sayari ya Jupiter inatajwa kama moja ya sayari pendwa sana kuzifanyia uchunguzi kwa wanasayansi.

FB_IMG_1664272167070.jpg
 
1) upana wa km142,000 kutoka kwenye equator yake.

Kutoka equator yake mpaka wapi?Hicho ni kipenyo au nusu kipenyo?

3) imeundwa na gesi pekee? Kwamba hakuna solid state objects kabisaaa? Yaani sayari nzima ni gesi tupu?

4) kama ukiwa na kg 100 duniani ukienda huko utakuwa na 240kg je ni kipi kitakuwa kimebadilika Kati ya mass na volume?

Hint: nimetumia namba ulizoweka wewe
 
Hakuna kinachobadilika Kati ya mass na volume, Gravitational force ndo inayobadilika ni kubwa ukiwa Jupiter *2.4 kuliko Ile ya dunian (kwa mujibu wa maelezo yake)

Hlo swal la kwanz tuendelee kumsubiri..
 
Issue ni mifano yake ya 100kg na 240kg. Hizo ni mass. Zinabadilika vipi wakati kitu ni hicho hicho?
 
Kiswahili cha kisayansi ni kihumu sana.

5: Jupiter inasifika kwa kua na nguvu kubwa ya sumaku (Magnetic fields) hii no kutokana na mikusanyiko wa gas. Duniani, hydrogen ipo kama gesi lakini kwenye sayari ya Jupiter, hydrogen ipo kama maji.Hii ni kutokana na pressure kua kubwa. Kwa kadri ambavyo anizunguka, sayari ya Jupiter hua inanasa na kukusanya viwawe vidogo vidogo vinavyopita pembeni yake
 
Why we see them up on our sky?
Where the space travelers (especially from earth to moon) went? Its sideways or upway?
its not true kwamba you see them up on our sky bcoz hata hiyo sky haiko up wala down ,dunia inavyofanya spining kila uelekeo utakaoelekea utaona sky na utaona ni up.the space traveller wanatoka nje ya atmosphere mpaka kwenye obirt ya dunia then wanaizunguka dunia kutafuta timing ya kutua mwezini au kwenda kwenye obirt ya mwezi kuzunguka huku wakifanya mission zao zilizowapeleka huko.ukiwa duniani utaona mwezi upo juu yako na wanaonda huko utaona wanaruka kwenda juu,na ukiwa mwezini utaona dunia ipo juu na kurudi duniani utaonekana unaruka kwenda juu
 
1) upana wa km142,000 kutoka kwenye equator yake.

Kutoka equator yake mpaka wapi?Hicho ni kipenyo au nusu kipenyo?

3) imeundwa na gesi pekee? Kwamba hakuna solid state objects kabisaaa? Yaani sayari nzima ni gesi tupu?

4) kama ukiwa na kg 100 duniani ukienda huko utakuwa na 240kg je ni kipi kitakuwa kimebadilika Kati ya mass na volume?

Hint: nimetumia namba ulizoweka wewe
Umenisaidia haya maswali
 
Back
Top Bottom