Chombo cha Juice kusafiri miaka saba hadi sayari ya Jupiter

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Nadhani watu wengi wameshangaa kwa kiasi kikubwa kuhusu safari ya chombo cha anga cha Juice ambacho kitasafiri kwa miaka saba kuelekea katika sayari ya Jupiter kwenye baadhi ya Miezi yake

Safari za anga za mbali huwa ni ngumu sana kwasababu kubwa ya uwezo wa chombo kusafiri kwa kutumia nishati ambapo kikawaida kwa kutumia nishati chombo kitasafiri kwa haraka sana na kufika sehemu lengwa kwa muda mchache

Kadri unavyosafiri kwa kasi kubwa basi tambua ndipo uzito katika chombo chako unavyozidi kwasababu nishati huendelea kutumika na kupungua na kadri inapopungua basi uwezekano wa kasi kuwa kubwa unakuwa ni mdogo sana

Sasa kwa kutambua jambo hilo wanasayansi wakaamua kutumia aina nyengine ya njia ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa msaada mkubwa sana , Kwasasa tunatumia njia ya Gravitational Assist

Chombo husafiri kwa kutumia gravity assist ya baadhi ya sayari na magimba mbalimbali angani ambapo chombo kitaingia kwenye sayari mfano Venus na kutafuta msukumo mkubwa ambao hueza kukipa chombo kasi kubwa kuelekea katika eneo lengine mbali zaidi ulimwenguni

Chengine vyombo vya anga za mbali haviwezi kusafiri kwa njia ya mstari mnyoofu yaani njia ya moja kwa moja , kwasababu kama tutatumia njia ya moja kwa moja basi tutahitaji kuwasha mashine ili ziweze kuchoma nishati iliyoko ndani ya chombo , sasa suala hilo ni gumu kwakuwa vyombo huwa haviwezi kubeba nishati kubwa ndani yake .

Huwa tuna safiri kwa kwa njia ya kuzunguka kwenye magimba huku tukitoka na kuingia kwenye baadhi ya magimba na kuchukua nguvu na kasi ili kuweza kuelekea katika safari yetu

Chombo cha Juice kitasafiri kupitia katika orbit ya dunia yetu ambapo chombo kitaama na kwenda kuzunguka mwezi 2024 na baadae kitakusanya nguvu na kutoka mwezini na kuelekea katika sayari ya Venus 2025 na mwaka 2026 kitarudi tena duniani na kuzunguka dunia yetu na kukusanya nguvu kuelekea za kuelekea katika sayari ya Jupiter ambapo itakuwa ni mwaka 2029 katika muda wote huo kutakuwa kunasubiriwa kwa sayari ya Jupiter kukaa katika njia nzuri baina yake yeye na dunia yetu

Kanuni ya Newton first of motion inasema kuwa kitu kikiwa kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo tu mpaka pale kutakapotokea external force nyengine kutokea nje na kuja kuiharibia mwenendo wake wa mwendo

Sasa kwa kutumia kanuni hiyo basi tunaweza kusema kuwa kama chombo kitarushwa kwa kasi ya 4km kwa sekunde basi itaendelea na kasi hiyo hiyo mpaka pale chombo hicho kitakapo bugudhiwa na force nyengine kutokea nje

Chombo hutumia mafuta au nishati yake pindi tu itakapoingia kwenye gimba lengine ambapo huhitaji nguvu kubwa kuweza kuendana na kasi ya matabaka ya anga hewa ya kwenye sayari au gimba fulani

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1681648970881.jpg
 
Back
Top Bottom