Ijue Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 - 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ijue Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 - 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jul 11, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2010 – 2015

  UTANGULIZI
  1. Katika Uchaguzi wa kushindanisha vyama vingi vya siasa ili kutwaa Dola na kuunda Serikali kila Chama hutarajiwa kuandaa Ilani ya Uchaguzi. Ilani hutafsiri na huelezea Sera za Chama kuhusu maeneo muhimu ya siasa, uchumi na jamii na hutoa maelezo fasaha kuhusu mikakati ya utekelezaji wa sera zinazonadiwa pindi wagombea wake wakifanikiwa kushinda.

  Aidha hutoa ahadi kwa Wananchi kuhusu mambo ambayo Chama kitaelekeza na kusimamia Serikali kutekeleza. Kwa hiyo Ilani ya Uchaguzi ni Maelezo ya Sera katika kipindi husika, na inalenga kuwaeleza Wananchi ni mambo gani Chama kitafanya iwapo kitashinda Uchaguzi na kuunda Serikali. Ilani hii ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 hadi 2015 inalengo hilo hilo…………..

  Hali ya Nchi yetu
  Pamoja na mafanikio mengi tuliyopata na changamoto zilizojitokeza, tuna fursa kubwa ya kuendelea kujenga uchumi wa kisasa ili kumudu ushindani katika mazingira ya utandawazi na kuongeza tija kwa kasi zaidi…………

  Pata
  Ilani ya CCM 2005 - 2010 na
  Ilani ya CCM 2010 - 2015........Attached below
   

  Attached Files:

 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Thanks mkuu Luteni, lemme go thru it
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwandishi atakuwa hajui maana ya 15%... maana asilimia 15% ya 2005 haiwezi kuwa the same kama ya 2015... b'se hiyo asilimia ina-take base ya sasa. ... siasa bwana... I bet they won't meet that.... 15% is that huge....
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Luteni, tunashukuru sana kwa Ilani. Maswali uliyouliza ni ya msingi. Lakini hiyo ilani tunayebahatika kuiona ni mimi na wewe, ambao yumkini wengi wetu hatupigi kura.

  Wapiga kura kule vijijini hawapewi kabisa hiyo nafasi ya kuiona ilani ya uchaguzi. Na hata wakiiona, hawawezi kuchambua mambo kama haya.

  Ndiyo maana siku zote huwa naamini kwamba CCM haitakaa iwakomboe watanzania kutoka katika dibwi la umaskini kwa kuwa umaskini na ujinga wa Watanzania ndiyo mtaji wa CCM kisiasa.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,842
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa kwa kuahidi ni kiboko, yaani wangekuwa wanatekeleza hizi ilani zao tungekuwa mbali sana.
  Kuna maeneo yanayonikera kwa kurudia rudia katika ilani zao zote bila kutekelezwa kila mwaka yanatajwa hivyo hivyo mfano:-
  - kukamilisha maandalizi na kuanza ujenzi wa daraja la kigamboni
  - kuanzia mabasi ya kasi dar es salaam (DART)
  - kupanua mtandao wa barabara DSM
  - Kuunganisha umeme wa grid ya Taifa Makambako - Songea
  - kujenga daraja la mto kilombero

  haya yamekuwa ni maneno tu katika ilani zote pasipo utekelezaji.

  Jambo la pili hivi kweli tunauwezo wa kujenga international airports zote hizo kwa wakati mmoja?
  JNIA (kujenga jengo jipya la abiria na majengo ya huduma) Songwe Mbeya (kukamilisha ujenzi), Bagamoyo (upembuzi), Msalato Modoma (kuanza ujenzi), Mwanza na Mtwara (ukarabati na ujenzi) na ukarabati wa viwanja Mafia, Arusha, Mpanda, Sumbawanga Bukoba, Kigoma, Tabora na Shinyanga.
  Haya yote yanaweza kufanyika katika miaka mitano? kwanini tusitoe kibaumbele katika viwanja vichache na tukaanzisha shirika jipya la ndege? forget about ATCL
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unachosema Nemesis ni kweli kuna mambo mengi sana wamerudia au wamekopi Ilani zilizopita sijui huwa hawana muda wa kuandaa mpya wanakopi and paste tu.

  Ukiipitia vizuri kuna kitu kimenifurahisha sana wanasema baadhi ya mafanikio ya Ilani iliyopinta ni pamoja na kuhamishia makao makuu ya Chama cha mapinduzi Dodoma. Sina uhakika kama kweli yametoka pale Lumumba, hata ikiwa kweli makao ya chama yanaingiaje hapo kinachotakiwa ni shughuli za serikali kuhamia Dodoma si chama.
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naomba kuwaomba wana JF tujitokeze kwa wingi 31 Oct 2010 tujibu hizi kejeli za CCM kwa kuchagua wabunge wa upinzani angalau wafikie 60% ya wabunge wote.

  Nilikuwa nasikiliza wakati Pinda akieleza utekelezaji wa ilani iliyopita sikuamini aliyokuwa anasema. Nilijaribu kuwauliza watu wengine juu ya utekelezaji wa ahadi za 2005-2010 wote tukawa na maoni yale yale kuwa hawajafikia hata 40% ya malengo lakini wao wanajinadi ile mbaya na kwa maoni yao (CCM) wamefikia zaidi ya 95% ya malengo.
  Kwa maana hiyo kama tunataka maendeleo lazima tubadilishe serikali, maoni yangu ni kwamba tufanye mabadiliko haya kwa awamu mbili ya kwanza iwe 2010 ambapo wabunge wengi wawe wa upinzani na 2015 rais atoke chama kingine, lakini siyo CCM.

  Nawakilisha
   
 8. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwenye ya mwaka 2005 atuwekee hapa tuweze kuoanisha. Muda wa kuchezeana umekwisha!
   
 9. M

  MJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi
  wanaofuzu elimu ya msingi ili waandaliwe kujiajiri wenyewe

  Nikinukuu hapa lengo la kuwapeleka hawa sekondari limekwisha wanajichanganya wenyewe? Hizi bla bla tulikwisha choka nazo.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  10. Kwa kutekeleza haya, Chama cha Mapinduzi kitakuwa kimeandaa mazingira ya kuondoa unyonge na shida zinazowasibu wananchi wake zinazotokana na umaskini na uchumi ulioduni. Aidha Ilani hii itakuwa kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuhakikisha kuwa inaitoa Tanzania kutoka uchumi ulio nyuma na tegemezi na kupambana na umaskini kwa hamasa, dhamira na kasi kubwa.

  Naota, naota nadanganywa hooooo Mbaraka Mwishehe
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ni swali tuu la kijinga, mnapokataa kuwa hawakufikia 95% mnatumia vigezo gani? Mfano mimi binafsi ofisi yangu nimefungua January 2006, nina jumla ya wafanyakazi watano (5) hivyo katika ajira milioni moja(1,000,000) zitakuwa zimebakia 999,995; Jee mbali na ofisi yangu ni biashara ngapi mpya zimefunguliwa kati ya January 2006 hadi leo? Kwa nini lengo la ajira 1,000,000 lisiwe limefikiwa.

  Ni mawazo yangu wala sipo kwenye politics, hata class monitor sijawahi kupata cheo hicho, sana sana kusimamia kanisani.
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jul 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nime-attach hiyo Ilani ya CCM, 2005 - 2010.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jul 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimefurahi sana kuwa mambo ya Sheria hayahusiani na dini yoyote bali hapa yanalengwa maslahi ya umma, maana Serikali haina dini!
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hongera.

  Kama hiyo 95% ndiyo imetufikisha hapa tulipo tuna kazi ya kufanya....

  Niambie kitu kingine ambacho unadhani kimetekelezwa kwa zaidi ya 50% with hard reality siyo hizi bla blah za takwimu zisizo na mashiko
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Naomba msaada wa Tafsri ya Katiba ya CCM Toleo la 2010: Sehemu ya Kwanza: Malengo ya Chama

  12) Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa Uchumi wa Taifa.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu.... samahani kama hii mada imejadiliwa

  NImeambiwa kwamba CCM wameondoa kigamboni bridge kwenye ilani yao!!! Je ni kweli? na kama ni kweli, hii ina maana gani kwa multibillion cosmopolitan City plan that is circulating around the country adn some potential investors community?

  Na hii ina maana gani kwenye suala la ahadi na utekelezaji?

  what about land grabbing ?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Great thinker plz fafanua kwa takwimu
   
 18. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Mbezi (Morogoro road)-Malambamawili-Kinyerezi-Banana (Km
  14.0); Ubungo Bus Termanial-Mabibo-Kigogo Round about (Km 6.4)

  barabara hizi tayari iko kwenye ujenzi au hatua zaq mwisho kukamilika sasa sijui hii ilikuwa ilani ya 2005-2010 au 2010-2015 nilitegemea kuwe na bara bara zingine
   
 19. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Mbezi (Morogoro road)-Malambamawili-Kinyerezi-Banana (Km
  14.0); Ubungo Bus Termanial-Mabibo-Kigogo Round about (Km 6.4)

  barabara hizi tayari iko kwenye ujenzi au hatua zaq mwisho kukamilika sasa sijui hii ilikuwa ilani ya 2005-2010 au 2010-2015 nilitegemea kuwe na bara bara zingine

  Kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART).

  huu mradi si ulishaanza zamani nachelea kusema kuwa watu hawafanyi kazi zaidi ya kukopy na paste
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia 1.0 ya pato ghafi la Taifa
  (GDP) kwa ajili ya Utafiti, Maendeleo na Maonyesho ya Matokeo ya Utafiti
  (R,D&D).

  nchi hii itaendeleaje kama hawajatoa kipaumbele kwenye Utafiti, Maendeleo na Maonyesho ya Matokeo ya Utafiti (R,D&D). sipati jibu baaado tutabaki nyuma <=1% kweliiiiiiiiiiii????????!!!!!!!!!???
   
Loading...