TRANSPONDER
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 399
- 988
Hodi hodi watu wangu wa kijiweni.
Baada ya kuwa msomaji wa Makala za watu kwa muda mrefu, nimeona mimi pia nisiwe mzigo kwenu bali niwaletee moja kati ya historia za vugu vugu la vita kati ya Marekani na Iran.
Kama inavyosemakana na watu wengi kwamba Iran amejiandaa sana kukabiliana na Marekani katika uwanja wa vita.
Je ni kitu gani hasa kipo kati ya nchi hizo mbili kupelekea mvutano huo? Je ni kwanini mvutano huo unaendelea huku viongozi wakuu wa nchi hizo wakienelea kubadilika?
Basi shuka nayo hii na wewe upate madini haya niliyoyachambua kwa kina sana.
Kwanza ningependa watu wote tuwe na uelewa wa nini maana ya neno “Diplomasia”, ukifungua kamusi ya Cambridge utakuta Diplomasia ni usimamizi wa mahusiano kati ya nchi mbili au ni taaluma ya kushughulika na watu bila kuwakosea au kuwakasirisha.
Diplomasia ndio inachochea usambazaji wa taarifa, mawasiliano na kupeana ujuzi wa aina mbalimbali kati ya nchi na nchi.
Kwa hapa kwetu naweza kutoa mfano wa mtu kama Mzee Kikwete ndiye mwanadiplomasia bora kuwahi kotokea baada ya hayati Baba wa taifa.
Sio kwa kumpendelea bali ni kwa namna alivyoshughulikia matatizo ya ndani nan je ya nchi bila kumwaga damu kiholela. Kupitia diplomasia ndio tunaona vitu kama balozi za nchi nyingine katika nchi fulani.
Turudi kwenye historia yetu, wenzatu hawa wa Iran na Marekani hawajawahi kuwa na uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1980. Hii ni kufuatia unyama uliofanywa katika ubalozi wa Marekani miaka hiyo (Nitakuja na hicho kisa mwisho wa historia hii).
Kuvunjwa kwa mahusiano kati ya nchi moja na nyingine huandamana na kufungwa ghafla kwa ofisi za ubalozi katika nchi husika.
Mfano Tanzania tutakapovunja uhusiano na Kenya tutafunga mipaka yote kati yetu na balozi wao tutamtimua, na wao watafanya hivyo hivyo kama si kumteka, basi hilo likitokea kama matokeo ya vita kuna mateka watachukuliwa na baadhi ya mali zitakuwa zimetekwa, lazima kuwe na namna ya nchi hizi mbili kuwa na uwakilishi wa namna nyingine kufuatilia watu na mali zao katika nchi hizo.
Hapo ndipo wataalam wakaja na neno “Protecting power” , Protecting power ni nchi inayowakilisha nchi nyingine katika nchi ambayo haina uhusiano nayo wa kidiplomasia.
Kwa mfano huo wa Tanzania na Kenya basi tungesema Uganda atuwakilishe nchini Kenya basi Uganda angekuwa ni protecting power yetu nchini Kenya.
Vivyo hivyo kwa Marekani na Iran, Pakistan alitumika kama protecting power ya Iran nchini Marekani na Uswisi kama kawaida yake akatumika kama protecting power ya Marekani nchini Iran.
Nimesema Uswisi kama kawaida yake sababu ndiye aliyekuwa protecting power ya Marekani nchini Cuba tangu 1961 hadi 2015 Obama alipofanikiwa kutumia uwezo wake wa kidiplomasia kurudisha uhusiano kamili wan chi hizo mbili uliokufa kipindi Field marshal Fidel Castro anaingia madarakani nchini Cuba.
Kiongozi mkongwe zaidi Mashariki ya kati ambaye ni kiongozi mkuu wa Iran Ali Hossein Khamenei ndiye aliyekataza mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani mwaka 2018 na kuturudisha katika matumizi kamili ya protecting power.
Uhusiano wa nchi hizi mbili ulianza katikati ya karne ya 19 hadi mwishoni mwa karne ya 19, Kipindi ambacho Iran ilikuwa ikiitwa Persia.
Kipindi hicho nchi za uingereza na urusi zilikuwa zikitamani sana kuitawala Iran hivyo Iran ilitawaliwa na hofu iliyoipelekea kuiamini sana Marekani ambayo ilikuwa haina maono ya kutawala nchi nyingine.
Uaminifu huo ulipelekea Shahs (Jina lililotumika kuwataja wafalme na viongozi wakubwa wa Persia enzi hizo) kuwateua wamarekani Arthur Millspaugh na Morgan Shuster kuwa Majenerali wa kuheshimiwa nchini humo.
Wakati wa vita ya pili ya dunia Iran ilivamiwa na Uingereza pamoja na Muungano wa kisovieti ambao walikuwa na ushirikiano mkubwa na Marekani katika vita.
Japo hilo lilitokea uhusiano wan chi hizi mbili uliendelea bila tatizo lolote baada ya vita mpaka pale serikali ya Mohammad Mosaddegh ilipopinduliwa kijeshi katika mapinduzi yaliyoongozwa na CIA wakisaidiwa na MI6.
Baada ya mapinduzi hayo walimweka kiongozi wao waliomtaka Shah Mohammad Reza Pahlavi na uhusiano wao ukaimarika mara dufu hadi wairan walivyoamka kutoka usingizini na kuja na kile kilichoitwa Mapinduzi ya Iran mwaka 1979 kumuweka mtaalam asiyewachekea Wamarekani The grand Ayatollah Ruhollah Khomeini.
Kwa jina lingine mapinduzi ya Iran yanajulikana kama mapinduzi ya dola la kiislamu. Hapo tunaweza kusema waliamka na kukimbia bila nguo kwa filimbi za Wamarekani ambao bado walikuwa wakiwachezea mchezo wa kuwaweka kwenye sitofahamu iliyosababisha mgogoro wa mafuta mwaka 1979 uliosindikizwa na vita kati ya Iraq na Iran.
Utashangaa kwanini Mmarekani anamchezesha Iran ngoma hiyo, jibu ni jepesi sana kwani utamu wa mafuta ndio ulituulia ndugu zetu zaidi ya mia moja pale Morogoro.
Wamarekani walibaki kwenye mshangao kwani hawakutegemea kama vuguvugu lilikuwa likiendelea Iran lingifikia hatua ya kumtoa madarakani kibaraka wao.
Kwa taarifa ilitumwa na CIA ikulu miezi sita kabla ya mpinduzi ya Iran ilisema kwamba Iran haipo katika harakati za mapinduzi wala vuguvugu litakalopelekea mapinduzi nchini humo.
Kiongozi mpya Khomeini, ambaye wamarekani walipendelea kumuita “Great Satan” alitoa magugu yote yaliyoachwa na shah kwa kuanza na Prime minister na nafasi yake kuwekwa mwanasiasa wa kawaida Mehdi Bazargan ambaye pia alikuwa na mahaba kwa Wamarekani.
Hadi wakati huo Wamarekani walitegemea uhusiano wao na Iran utaendelea kuwa wa kawaida. Wanamapinduzi wa Iran walitaka kumuua kiongozi waliomtoa madarakani.
Kama kawaida yao Wamarekani wakishatafuna kama mua hawatokuhitaji tena Basi serikali ya Jimmy Carter ikakataa kumpa msaada wowote kiongozi aliyepinduliwa ikiwamo kumrudisha madarakani.
Hata pale kiongozi huyo alipougua saratani na kutaka kwenda kutibiwa marekani ubalozi wa marekani mjini Tehran ulikataa kumpa visa ili kukuza uhusiano wao na serikali mpya kuwawezesha kufaidi utamu wa Mafuta.
Lawama ziwaendee wanasiasa wakongwe wa Marekani Kissinger na Rockeffeller waliofanikiwa kumshawishi J Carter kumruhusu Shah akatibiwe Marekani.
Hilo ndilo likawa kosa kubwa kwa Wamarekani kwani wana mapinduzi wa Iran walipata uthibitisho kwamba Kiongozi huyo anapanga njama za dhidi ya mapinduzi yao, hivyo wakamtaja kama kibaraka wa marekani hali iliyopelekea wana mapinduzi hao kupeleka dhoruba ubalozi wa Marekani nchini Iran.
Tarehe 4 Mwezi wa kumi na moja 1979 wanamapinduzi hao waliteka ubalozi wa Marekani jijini Tehran na kuwateka wanadiplomasia wa Mmarekani 52 kwa siku 444.
Waziri mkuu Bazargan alipinga swala hilo la kuchukua mateka ubalozi wa Marekani hali iliyompelekea yeye mwenyewe kujiuzulu baada ya tukio hilo.
Kitendo cha waandamanaji wa Iran kuwateka wanadiplomasia wa marekani kilikuwa kinapingana na sharia ya kimataifa inayokataza kukamata wanadiplomasia wa nchi nyingine na inazuia askari wa nchi mwenyeji kuingia katika eneo la ubalozi wa nchi ngeni.
Swali la kujiuliza ni “Je Marekani alikubali tu watu wake washikiliwe nchini Iran kwa siku 444 bila kuwaokoa?” Jibu ni hapana.
Hapa ndipo Marekani alipata aibu ya karne pale alipojaribu kuwakomboa wanadiplomasia wake.
Hii wenyewe waliita Operation Eagle Claw.
Ngoja kidogo niwadorishie operesheni hiyo kwa uchache, tiririka nayo!
SEHEMU YA PILI inaendelea post inayofuata