Ijue historia ya kaburi la Sharif Abdushakur Salim Al Attas lililopo Samora, Posta Jijini Dar es Salaam

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Kuna bustani moja katikati ya jiji la Dar es salaam (katikati ya barabara ya Samora, India na Mosque) maeneo ya clock tower. Ukifika katika bustani hiyo, kitu cha kwanza utakachokiona pale ni kaburi lililojengewa na marumaru nyeupe na ambalo kwa mujibu wa watu waliozoea kukaa pale mara kwa mara ni kwamba kuna mtu maalumu ambaye hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha mazingira yaliyozunguka kaburi hilo (siyo bustani yote!) na hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo (sijui hulipwa na nani). Vile vile nimesikia kwamba baadhi ya watu huenda kuabudu pale nyakati za usiku.

Je, kaburi hili ni la nani katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji?​
Je, kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yavyohamishwaga kutakuwa na athari gani?​

Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu ni Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo ingetoa mwanya hata vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa mhasisi wa Taifa letu, vile vile kwa vitendo vya hawa MAFISADI tungeweza kuamua wana JF tukaenda kuwaombea dua baya.



************************
Maoni kutoka kwa wadau​

************
 

Mtaalam, hili kaburi bado lipo, hata leo asubuhi nilipita hapo nimeliona limeoshwa limetakata kweli. Si unajua tena marumaru?

Kwa wanaojua, tafadhali tupe habari zaidi. Ni la mtu gani?
 
Waungwana kwa yeyote anaejua vizuri jiji la Dar maeneo ya Posta kuna kaburi moja tu la kipekee makutano ya Samora Street na India street karibu na clock tower, pembeni kidogo kuna bank ya NMB, Jmoo au maarufu kama Harbor view. Pana kontena la Voda hivi!

Hili kaburi nimejaribu kwa mda mrefu kuwauliza wale wanaoshinda eneo hilo hasa madereva tax wamesema hawajui ni la nani!Sasa ndugu wana JF kwa yeyote anaejua juu ya kaburi hili tena limejengwa kwa marumaru nyeupe anipe ufafanuzi! Je, lina uhusiano wowote na ukombozi wa taifa hili?

Je, lina uhusiano wowote na jiji la Dar? Je, lina uhusiano wowote na CCM?

Natumia simu ningeweza kupost na picha yake ila kama kuna mdau aliye jirani na eneo hilo anaeweza kupost picha naomba afanye hivyo!
 
Mimi nalijua vizuri sana lipo maeneo ninako ishi. Marehemu ni MTANZANIA wa kwanza kuwa IMAMU ktk miaka hiyo ya 1800. Usisahau maunganisho yale ni ya mitaa ya Msikiti na India na yanaendelea hadi Samora. Jina lake silikumbuki. Asante. kaburi hili limekuwa kama limetupwa lakini ni historia nzuri sana. Japo linatunzwa hakuna kibao chochote cha kuonyesha historia ya IMAMU wetu huyu.
 
Uislamu nijuavyo ulianzia kule Kilwa iweje huyu mtz azikwe pale? Je huko kilwa hakuna watz wa mwanzo kabisa walioamini uislamu? Kwanini waislamu hawamuenzi Imam wao wa mwanzo badala yake wanakaa kueneza udini kupitia kwa Alhaj JK mkweree?
 

JMoo ndo jengo gani? Mi nnavyojua JMoo ni jina la msanii wa HipHop Tanzania. Hilo jengo ni J. Mall. Usichanganye Tui na Maziwa siku nyingine.
Asante kwa kunielewa.
 
Idadi ya watu waliokwishakufa toka dunia imeumbwa ni wengi sana kulingana na makaburi yaliyoko sasa, nahisi kuna makaburi mengi sana yalifutika bila sisi kufahamu.
So possible hata hapo mliopo kuna makaburi chini ya nyumba mnayoishi
 
Niliwahi sikia juu ya hilo kaburi, hapo palikuwa na nyumba ya mhindi -Mtanzania. Alifiwa na mkewe na akuwa na mtoto, wala mrithi mwingine. Hivyo alikabidhi eneo hilo kwa Mwl. nyerere, akamwambia watu wapunzike katika eneo lile, pasijengwe chechote, mpaka hati yake ya ardihi itakapokwisha., ndipo mwl akawakabibidhi hlmashauri ya Jiji walitunze
 
Kuna walakini na hoja yako ndugu!
 
Mimi nilisikia kuwa hilo ni jaribio la kutwaa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumba ya ibada ya dini mojawapo hapa tanzania. Nilijuzwa kuwa hakuna kaburi wala nini ni kwamba baada ya watu wa dini hiyo kuona kuwa ni la wazi waliamua wajenge kaburi hilo ili baadaye wawezejenga nyumba yao ya ibada. mwanzoni jiji waliondoa ujenzi huo lakini wenyewe wakarudi kwa kasi na kulijenga na kuwatisha wote watakao jaribu kuzuia mpango huo.

Hivyo hiyo ni mpango mkakati wa muda mrefu ya kutwaa eneo hilo la wazi. Kabla ya mpango huo miaka ya 1999/2000 hakukuwa na kitu hapo. Jamaa mmoja alisema hata ukichimba hapo hakuna kitu kama mabaki ya binadamu wala nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…