steve_shemej
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,092
- 1,433
Makambako ni sehemu maarufu Sana hapa nchini kwakuwa ipo katika njia panda ya kwenda Mbeya, Songea na Iringa
Makambako kwa Sasa inapatikana katika mkoa wa Njombe
HISTORIA YAKE
Kipindi cha ngoni migration wangoni baada ya kuikalia Songea walitamani wajitanue mpaka panapoitwa Iringa kwa Sasa lakini mpango wao ulipata changamoto kila walipofika sehemu inayo itwa Makambako hivi Sasa kipindi hicho palikuwa na jina jingine
Wangoni walipofika eneo hilo walikuwa wanakabiliwa na Vita kubwa kutoka kwa majeshi ya chifu Mkwawa ambapo walipigana Vita mara mbili bila ya kupatikana mshindi mngoni alirudi nyumbani na Mkwawa alirudi kwake mara ya tatu mngoni alipanga Tena shambulio dhidi ya vikosi vya Mkwawa
Vita hii ya tatu Mkwawa alishindwa Vita alipoteza 70% ya Askari wake wote baada ya Mambo kuwa MAGUMU Mkwawa alituma wazee kwenda Songea kwa chifu Songea kuomba Vita isitishwe na wasipigane Tena
Wangoni walikubali na wakaombana wawe watani tangu hapo mhehe na mngoni ni watani
Sasa pale walipokuwa wanapigania wakaamua wapape jina mngoni akaamua paitwe MAKAMBAKU kwa kingoni KAMBAKU ni mtu shupavu mwenye nguvu MAKAMBAKU ni uwingi
Watu walikuwa hawaezi kuita MAKAMBAKU wakawa wanapaita Makambako Kama inavyoitwa Sasa hivi
Hiyo ndyo historia fupi
Sent using Jamii Forums mobile app