Ijue historia fupi ya fundi wa mpira mwamba PEP GUARDIOLA

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,491
Wahenga walivoleta hule msemo wa mchumia juani hula kivuli ulikuwa una maana kubwa na ulikuwa unatumika kwenye nyakati mbali mbali basi ndo Marcelo Bielsa dhidi ya Pep Guardiola, tunaishi kwenye nyakati za kufanikiwa na kujituma na kumtanguliza Mungu mbele yake.
.
.
Mnamo mwaka 2006, Oktoba Pep Guardiola, alikuwa na miaka 35, alikuwa anacheza mpira Mexico, Daraados de Sinaloa( nchi ya madoni), alisafari Maili 5000, kutoka Mexico mpaka Argentina kwenda kukutana na Marcelo Bielsa mwalimu alikuwa anamvutia ( Roll Model wake) na kuomba ushauri je huu ni wakati sahihi wa mimi kuingia kwenye ukocha.
.
.
Bielsa alikuwa katikati ya jiji la Buenos Aires, akipumzika baada ya miaka miwili kuachana na timu ya Taifa ya Argentina, ambayo alikuwa anaifundisha, Bielsa alimpokea Guardiola, kwa furaha sana,na rafiki yake ambaye alikuwa mwandishi wa filamu na director David Trueba, walifika nyumbani kwa Bielsa.
.
.
Guardiola alisema atoisahau hii siku sababu Bielsa alikuwa mkaribu na tulianza maongezi kuhusu mpira tu yalichukua masaa 11, mpaka usiku kabla ya Bielsa kumpeleka kwenye library yake , alimwambia Pep Guardiola, lazima utambue falsafa zako zinataka nini kisha utambue na staili ya mpira wako , Bielsa alimchukua Pep Guardiola mbaka kwenye library yake kumejaa vitabu vya mpira, vya kila aina, Pep Guardiola alishangaa sana.
.
.
Bielsa ukumbuke hapo awali alipewa jina la ' El Loco' la utani sababu ya mpira wake kwa kushambulia, na falsafa zake za mpira, Bielsa akamwambia Pep, kuna mda unatakiwa uwe kiburi na uamini unachokiaminiutafanikiwa, kama unaona vile umeshindwa kazi achia alafu nenda kampumzika akili itulie kisha urudi tena, ndipo mwaka 2012, kuondoka Barcelona, Pep alienda Marekani mwaka mzima kupumzika, huku akikataa ofa mbali mbali hapo awali.
.


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Nimepata point kwamba lazima utambue na usimamie falsafa zako kwenye ndoto unayotaka kukamikisha . Asante mkuu.
 
Kocha ambae hana akili yeye kila mechi anafunguka UEFA champions league ataisikia tu atabeba league mpaka achoke ila kwa dharau zake kwa UEFA champions league ataiota tu.
 
Mi nachojua GUARDIOLA Barcelona yakina rivaldo, Patrick kluivert,marc overmars alikuwa mchezaji wa KAWAIDA TU ila mara nyingi kocha mzuri KWENYE maisha yake yakimpira IKIFANYA uchunguzi yakinifu hawajawhi kuwa coaches wazuri zaidi ya zidane tu ila wengi makocha wakubwa utasikia ahh alikuwa Fulani Hadi waku re call historian yake kwanza
 
Huu ujinga wa source # 1 na # 2 ni ulimbukeni?
Hutaweka source yoyote
 
Kocha ambae hana akili yeye kila mechi anafunguka UEFA champions league ataisikia tu atabeba league mpaka achoke ila kwa dharau zake kwa UEFA champions league ataiota tu.
We umeanza kufatilia mpira juzi au? kwaiyo pep hana taji la UEFA?

au hayo alibeba kwa kupaki basi?
 
Kocha ambae hana akili yeye kila mechi anafunguka UEFA champions league ataisikia tu atabeba league mpaka achoke ila kwa dharau zake kwa UEFA champions league ataiota tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom