Guardiola awaonya wachezaji wa City kuingia mitandao ya jamiii baada ya Grealish kuvamiwa na vibaka

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,716
29,071
Mzuka wanajamvi,

Kocha mahiri wa timu ya mpira katika ligi kuu ya uingereza Manchester City Pep Guardiola. Amewatahadharisha wachezaji wake kuwa makini wanapoingia kwenye mitandao ya jamii na kuanika mali zao na lifestyle zao.

Hii imetokea baada ya kiungo mkabaji wa timu hiyo Grealish familia yake kuvamiwa na vibaka usiku wa boxing day wakati City ikicheza na Everton.

Vibaka hao walifanikiwa kuiba vito vya thamani jewellery vyenye thamani ya zaid ya euros million moja.

Pep ambaye waafrika wengi wanadhani ni mbaguzi aliendelea kusisitiza kwa kuwatahadharisha na kuwaonya wachezaji wake wakae mbali katika mitandao ya jamii na kuwa wasiri katika maisha yao.

Akaendelea kusema nyie mmebahatika kuwa wachache wenye maisha mazuri na hela nyingi. Kuna mabilion ya watu huko nje wanastruggle sana katika maisha kwa iyo wakiwaona mnavyoanika mali na maisha yenu mtandaoni mnawatamanisha na kuwa karibisha.

Akawatolea mfano mchezaji wake wa zamani Joao Cancelo ambaye alivamiwa kwake ureno na vibaka na kukatwa kwa kukwaruzwa na kisu alipojaribu kupambana nao.

Pia amewashauri wachezaji wake watilie maanani swala la ulinzi kwa kutumia mitambo maalum na makampuni ya ulinzi. Licha ya huo ushauri ni huhuyu Grealish alitumia zaidi ya pauni laki tano za babu kuzungushia fens ya umeme na mitambo ya hatarii kuzuia vibaka lakini vibaka waliweza kuingia.

Wachezaji wengine ambao wameshavamiwa na vibaka na kuibiwa fedha na vitu vya thamani ni Paul Pogba, Jesse Lingard, Pierre Aubamayang, Kurt Zouma.

Pia aliyekuwa mke wa Kanye West Kim Kardashian alivamiwa na kuibiwa kiasi kikubwa cha jewellery na fedha Paris ufaransa baada ya kuposti kwe Instagram.

Kwa nini na vibaka wa huku kwetu wasiwalize matijiri uchwara kina Chief Godlove?

King Kong III



View: https://www.youtube.com/watch?v=nQNIU82Da7Y&pp=ygUkQ2hpZWYgZ29sb3ZlIGFraWxpc2hhIGt1a3UgbWJ3YSB3YWtl
 
Pep ambaye waafrika wengi wanadhani ni mbaguzi aliendelea kusisitiza............
Kwani kulikuwa na umuhimu wa kuandika hv au kuna kitu unakiandaa.?
Anyway, kama Waafrika mnarukaruka uwanjani na anaona hamna umuhimu kwenye timu yake bc naona yupo sahihi
 
Guardiola sioni kama ni mbaguzi, yupo very smart

Wale wenye element ya kujiona wanabaguliwa waache hiyo tabia watakufa kwa stress
 
Back
Top Bottom