Backdoor
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 316
- 422
Habari za wakati huu wakuu..
Hebu leo tujifunze kidogo Juu ya dhambi.
Toka kuumbwa kwa ulimwengu halikuwa kisudi la MUNGU watu wake aliowaumba kwa sura na mfano wake(ambayo ni roho) wateseka iwe kwa maradhi, magonjwa ama Vita.
Asili ya MUNGU ni wema, hivyo Kila atendalo ni jema.
Sasa dhambi ni Nini?
Dhambi ni mzizi ambao huzalisha lolote lisilo la haki.
Na haki je?
Haki ni uwezo wa kusimama mbele za Mungu pasipo kuhesabiwa hatia.
Dhambi ndio huzalisha makosa. Hivyo basi kuzini, kuiba kuua ni matokeo tu ya dhambi.
Inakuaje Sasa tuna dhambi..
Rejea kitabu Cha mwanzo, mtu wa Kwanza Adam alipoanguka katika uasi na Kula tunda aliloambiwa asilile. Hapo ndipo sote tunaangukia katika dhambi.
Kwanini?
Kwasababu sote tuna mbege ya Adam ndani yetu.
Mbegu ya uasi(dhambi). Hii ndio inatufanya wanaadamu wote tuwe na dhambi.
Swali ambalo watu wengi hujiuliza kwanini Mungu aliamua kumuua mwanae wa pekee badala ya kumuua shetani, ni kwasababu hata shetani akitolewa Leo Bado tunabaki na hatia mbele ya MUNGU kwaajili ya mbegu tuliyo nayo.
Ndio maana Sasa MUNGU aliamua kushughulika na mzizi.
Hapo ndipo alipomtuma mwanae YESU KRISTO asiye wa asili ya dhambi alipokuja dunia. Yeye anatoka mbinguni,tukumbuke alizaliwa kwa uwezo wa roho mtakatifu.kwa maana nyingine alizaliwa bila kuwa mbengu ya Adam ndani yake ambayo asili yake ni dhambi.
Ili kututoa katika asili ya dhambi na kutufanya tuwe wenye asili ya Mungu ambayo ni kutokutenda dhambi.
Sasa ilifanyikaje?
Ndipo alipokuja ulimwenguni na kufa na kufufuka.
Kwa kuamini hilo, ndio ondoleo la dhambi linapotokea. Na ndio kuzaliwa mara ya pili katika(roho).Ambapo mtu ahesabiwi Tena dhambi.