Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelsoni Mandela toka ameanza kuugua amekuwa akitibiwa nchini mwake mpaka alipofariki dunia. Hii ni kwasababu nchi yake imethamini sekta ya afya hivyo hakukuwa na haja ya yeye kwenda kutibiwa nje. Ingekuwa Tanzania, mtu wa hadhi yake ungekuta amefia Uingereza, Ujerumani, India au Afrika kusini na sasa hivi tungekuwa tunasubiri maiti kutoka huko. Hii ni kwasababu viongozi wamepuuza sekta muhimu kama elimu na afya lakini bila aibu utawakuta wanasimama majukwaani na kutamba kuwa wameimarisha sekta ya afya na elimu wakati wao hawatumii huduma hizo kwakuwa ni mbovu. Katika nchi za wenzetu kama Uingereza, huwezi ukiwa waziri au waziri mkuu ukasimama bungeni au hadharani na kusema mathalani hali ya elimu au afya ni nzuri wakati wewe mwenyewe hutumii huduma hizo na badala yake unatumia huduma za watu binafsi au nje ya nchi. Kwao ni lazima ujiuzulu mara moja. Hapa kwetu utashangaa waziri au rais anasema tumeinua elimu na afya wakati yeye mwenyewe na familia yake hawatumii huduma hizo ambapo wanakimbilia India, Uingereza, Ujerumani na sasa Afrika ya kusini.
Kutokana na hilo ndipo nikapata wazo la kuishauri serikali kujenga hospitali maalumu itakayokuwa na vifaa vya kisasa kama vile wanavyovifuat ng'ambo na kuwa na madaktari mabingwa maalumu kwa jili ya kucheck afya na kutibu viongozi wa juu tu na watu maalumu watakaopewa kibali na ikulu kutibiwa katika hospitali hiyo kama wanaovamiwa na kung'olewa meno, macho, kucha, nk. Hii itasaidia kupunguza gharama za viongozi wetu na baadhi ya wananchi wenye matatizo maalumu ya dharura kama kuvamiwa kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi. Wakati mwingine tunawapoteza watu kwasababu ya kucheleweshwa kufikishwa hospitali mfano mtu anavamiwa leo inaonekana hapa hawawezi sasa mpaka afike Afrika ya kusini au Uingereza anakuwa kasha cheleweshwa matokeo yake anafika na kufa.
Gharama za uendeshaji wa hospitali hii zitakuwa ndogo kwani haihitaji watu wengi. Inahitaji madaktari bingwa kama watatu mfano wa moyo, upasuaji mishipa ya fahamu, magonjwa kama kansa na UKIMWI na manesi wachache sana. Hii ni muhimu kwasababu serikali katika bajeti yake ya 2013/2014 imetenga shilingi bilioni moja kwaajili ya mazishi ya viongozi na pia imetenga shilingi milioni 18 kwa ajili ya wajumbe wa tume ya katiba watakaopata UKIMWI wakiwa kazini. SERIKALI INA AKILI!
Nchini Uingereza waziri wa elimu aliwahi kulazimishwa kujiuzulu baada ya kusema hali ya elimu katika shule za umma(Public Schools) ni nzuri wakati mtoto wake alikuwa anasoma shule ya binafsi. Wabunge wakamwambia hana udhu ya kusema hivyo kwasababu ingekuwa ni kweli hali ni nzuri mtoto wake naye angekuwa anasoma huko. Aliachia madaraka mara moja. Hapa kwetu?