Ijengwe hospitali maalumu ya kutibu viongozi na watu maalumu

Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
10,340
Likes
6,699
Points
280
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
10,340 6,699 280
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelsoni Mandela toka ameanza kuugua amekuwa akitibiwa nchini mwake mpaka alipofariki dunia. Hii ni kwasababu nchi yake imethamini sekta ya afya hivyo hakukuwa na haja ya yeye kwenda kutibiwa nje. Ingekuwa Tanzania, mtu wa hadhi yake ungekuta amefia Uingereza, Ujerumani, India au Afrika kusini na sasa hivi tungekuwa tunasubiri maiti kutoka huko. Hii ni kwasababu viongozi wamepuuza sekta muhimu kama elimu na afya lakini bila aibu utawakuta wanasimama majukwaani na kutamba kuwa wameimarisha sekta ya afya na elimu wakati wao hawatumii huduma hizo kwakuwa ni mbovu. Katika nchi za wenzetu kama Uingereza, huwezi ukiwa waziri au waziri mkuu ukasimama bungeni au hadharani na kusema mathalani hali ya elimu au afya ni nzuri wakati wewe mwenyewe hutumii huduma hizo na badala yake unatumia huduma za watu binafsi au nje ya nchi. Kwao ni lazima ujiuzulu mara moja. Hapa kwetu utashangaa waziri au rais anasema tumeinua elimu na afya wakati yeye mwenyewe na familia yake hawatumii huduma hizo ambapo wanakimbilia India, Uingereza, Ujerumani na sasa Afrika ya kusini.
Kutokana na hilo ndipo nikapata wazo la kuishauri serikali kujenga hospitali maalumu itakayokuwa na vifaa vya kisasa kama vile wanavyovifuat ng'ambo na kuwa na madaktari mabingwa maalumu kwa jili ya kucheck afya na kutibu viongozi wa juu tu na watu maalumu watakaopewa kibali na ikulu kutibiwa katika hospitali hiyo kama wanaovamiwa na kung'olewa meno, macho, kucha, nk. Hii itasaidia kupunguza gharama za viongozi wetu na baadhi ya wananchi wenye matatizo maalumu ya dharura kama kuvamiwa kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi. Wakati mwingine tunawapoteza watu kwasababu ya kucheleweshwa kufikishwa hospitali mfano mtu anavamiwa leo inaonekana hapa hawawezi sasa mpaka afike Afrika ya kusini au Uingereza anakuwa kasha cheleweshwa matokeo yake anafika na kufa.
Gharama za uendeshaji wa hospitali hii zitakuwa ndogo kwani haihitaji watu wengi. Inahitaji madaktari bingwa kama watatu mfano wa moyo, upasuaji mishipa ya fahamu, magonjwa kama kansa na UKIMWI na manesi wachache sana. Hii ni muhimu kwasababu serikali katika bajeti yake ya 2013/2014 imetenga shilingi bilioni moja kwaajili ya mazishi ya viongozi na pia imetenga shilingi milioni 18 kwa ajili ya wajumbe wa tume ya katiba watakaopata UKIMWI wakiwa kazini. SERIKALI INA AKILI!

Nchini Uingereza waziri wa elimu aliwahi kulazimishwa kujiuzulu baada ya kusema hali ya elimu katika shule za umma(Public Schools) ni nzuri wakati mtoto wake alikuwa anasoma shule ya binafsi. Wabunge wakamwambia hana udhu ya kusema hivyo kwasababu ingekuwa ni kweli hali ni nzuri mtoto wake naye angekuwa anasoma huko. Aliachia madaraka mara moja. Hapa kwetu?
 
Attachments:

Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,595
Likes
3,150
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,595 3,150 280
Tumia akili wewe, kwahiyo Viongozi ndio mnamaana sana kuliko sisi wanachi, Badala kusema Idadi ya vitanda ingozwe na kujenga Hospitali za Uwakika Kila Mkoa na Kila wilaya. Unakuja na Ufujaji wa fedha wakati muhimbili tu hapo wagonjwa wanalala chini.
 
LOOOK

LOOOK

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Messages
3,395
Likes
69
Points
145
LOOOK

LOOOK

JF-Expert Member
Joined May 17, 2011
3,395 69 145
Hahahaaaaaaaaaaaaaaa!hiyo hospitali viongozi wote wa upinzani watakuwa wanadungwa polonium coz naamin itakuwa under Ccm
 
F

fazahausi

Senior Member
Joined
May 8, 2013
Messages
139
Likes
0
Points
33
F

fazahausi

Senior Member
Joined May 8, 2013
139 0 33
tena nngekuwa daktari hao viongoz wenu mafisad nngewachoma sindano za sumu wote wakafie mbal,,,pambafffffff
 
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
2,163
Likes
1,005
Points
280
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
2,163 1,005 280
Tatizo la hospitali zetu sio madaktari ni vipimo..

Nimefika Apollo hakuna tofauti yeyote na sisi kwa kuangalia manesi na ma Dr wao ukitoa ma specialist wachache..

Sema vipimo na vifaa ndio si mchezo, unaingia chumba kufanyiwa check up kama upo contol room ya kampuni ya technologia. Mashine za kufa mtu..

nilienda na mgonjwa alikuwa anafanyiwa check up ya tumbo akamezeshwa kidonge wakati kinavyoshuka kinapiga picha tumbo. Zima na zinatokea kwenye ma screen ya ukutani kama maigizo vile..
Jamaa wana ratio ya 1 nurse per patient,

Nina imani ma dr tunao na nia wanayo sema vifaaa tu na mishahara duni ndio inayotukwamisha
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,514
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,514 280
Tumia akili wewe, kwahiyo Viongozi ndio mnamaana sana kuliko sisi wanachi, Badala kusema Idadi ya vitanda ingozwe na kujenga Hospitali za Uwakika Kila Mkoa na Kila wilaya. Unakuja na Ufujaji wa fedha wakati muhimbili tu hapo wagonjwa wanalala chini.
haha..pengine ana maanisha pawe mahali pa kuwachinja vyema wakileta za kuletwa.Sababu kubwa ya viongozi kutibiwa nje ni kuogopa pinduliwa kwa madakatari locala kuwazimisha.Unadhani km ndugu yako aliuwawa Olasiti au Soweto ,halafu kauli za maCCM na viongozi wa juu zikawa zile utawaacha?
 
kukomya

kukomya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Messages
344
Likes
21
Points
35
kukomya

kukomya

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2011
344 21 35
Binafsi nimemwelewa mleta mada. Hiingii akilini baada ya miaka 50 ya kujitawala viongozi wetu wanategemea hospitali za nje ili kutibiwa hata mafua!
Mkanganyiko zaidi unakuja serikali hii hii inapopanga bajeti ya zaidi ya bilioni moja kwa mazishi ya viongozi!
Ingekuwa heri zaidi kama fedha hizo zingetumika kununulia mitambo ya kisasa pale Muhimbili au Lugalo (Kwa usalama zaidi) na kuboresha mishahara na posho za wahudumu wa kitengo kile. Haiwezekani kabisa sisi kama nchi tushindwe kuwa na hospitali moja, mbili au hata tatu za viwango vya wenzetu.
Kwa kuanza tunaweza ajiri maspecialist wa viwango vya kimataifa toka nje watakaofanya kazi na wa kwetu hapa, watakapomaliza mikataba watawakabidhi watanzania na hapo tutakuwa tumefanikiwa kuihamisha tekinolojia.
 
Ndugu yangu

Ndugu yangu

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
608
Likes
48
Points
45
Ndugu yangu

Ndugu yangu

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
608 48 45
Tatizo la hospitali zetu sio madaktari ni vipimo..

Nimefika Apollo hakuna tofauti yeyote na sisi kwa kuangalia manesi na ma Dr wao ukitoa ma specialist wachache..

Sema vipimo na vifaa ndio si mchezo, unaingia chumba kufanyiwa check up kama upo contol room ya kampuni ya technologia. Mashine za kufa mtu..

nilienda na mgonjwa alikuwa anafanyiwa check up ya tumbo akamezeshwa kidonge wakati kinavyoshuka kinapiga picha tumbo. Zima na zinatokea kwenye ma screen ya ukutani kama maigizo vile..
Jamaa wana ratio ya 1 nurse per patient,

Nina imani ma dr tunao na nia wanayo sema vifaaa tu na mishahara duni ndio inayotukwamisha
tatizo viongozi wetu hawaiamin nchi yao kama inawatalaam wazuri sana, ndio maana hawashughulikii na kuboresha hos zetu
 
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
10,340
Likes
6,699
Points
280
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
10,340 6,699 280
Tumia akili wewe, kwahiyo Viongozi ndio mnamaana sana kuliko sisi wanachi, Badala kusema Idadi ya vitanda ingozwe na kujenga Hospitali za Uwakika Kila Mkoa na Kila wilaya. Unakuja na Ufujaji wa fedha wakati muhimbili tu hapo wagonjwa wanalala chini.
Ndio tatizo la kukurupuka. Hujanielewa kabisa. Ungekuwa mtu wa fasihi ungenielewa mapema. Hiyo mimi nimeitoa kama kejeli kwa viongozi wetu kutojali wananchi na kujijali wenyewe. wao wakiumwa hawada shida wanakuimbia mbio nje wakati mwananchi wa kawaida hawezi. wakijenga hospitali nzuri zenye vifaa na wataalam wazuri watakuwa hawana haja ya kwenda nje na hivyo kupunguza matumizi makubwa ya kuwatibu nje. We kwa pupa zako umefikiri mimi nataka tu viongozi ndio wapate matibabu mazuri, sio maana yangu. Nilitaka wajifunze kwa hayati Mandela ambaye ameugulia na kufia nchini mwake kwasababu kile wanachokifuata viongozi wetu nje wao wanacho na sis tunaweza pia kama tukidhamiria. Kama unauchungu kweli mbona hujahoji kwanini viongozi wajitengee bilioni moja kwa ajili ya mazishi yao? Je ina maana wananchi hawahitaji gharama za mazishi? Jihadhari kujibu kitu ambacho hukielewi vizuri kwani utaishia kujidhalilisha. Kuna issues ambazo zinataka uzichukulie Literary sio literally
 
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
10,340
Likes
6,699
Points
280
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
10,340 6,699 280
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelsoni Mandela toka ameanza kuugua amekuwa akitibiwa nchini mwake mpaka alipofariki dunia. Hii ni kwasababu nchi yake imethamini sekta ya afya hivyo hakukuwa na haja ya yeye kwenda kutibiwa nje. Ingekuwa Tanzania, mtu wa hadhi yake ungekuta amefia Uingereza, Ujerumani, India au Afrika kusini na sasa hivi tungekuwa tunasubiri maiti kutoka huko. Hii ni kwasababu viongozi wamepuuza sekta muhimu kama elimu na afya lakini bila aibu utawakuta wanasimama majukwaani na kutamba kuwa wameimarisha sekta ya afya na elimu wakati wao hawatumii huduma hizo kwakuwa ni mbovu. Katika nchi za wenzetu kama Uingereza, huwezi ukiwa waziri au waziri mkuu ukasimama bungeni au hadharani na kusema mathalani hali ya elimu au afya ni nzuri wakati wewe mwenyewe hutumii huduma hizo na badala yake unatumia huduma za watu binafsi au nje ya nchi. Kwao ni lazima ujiuzulu mara moja. Hapa kwetu utashangaa waziri au rais anasema tumeinua elimu na afya wakati yeye mwenyewe na familia yake hawatumii huduma hizo ambapo wanakimbilia India, Uingereza, Ujerumani na sasa Afrika ya kusini.
Kutokana na hilo ndipo nikapata wazo la kuishauri serikali kujenga hospitali maalumu itakayokuwa na vifaa vya kisasa kama vile wanavyovifuat ng'ambo na kuwa na madaktari mabingwa maalumu kwa jili ya kucheck afya na kutibu viongozi wa juu tu na watu maalumu watakaopewa kibali na ikulu kutibiwa katika hospitali hiyo kama wanaovamiwa na kung'olewa meno, macho, kucha, nk. Hii itasaidia kupunguza gharama za viongozi wetu na baadhi ya wananchi wenye matatizo maalumu ya dharura kama kuvamiwa kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi. Wakati mwingine tunawapoteza watu kwasababu ya kucheleweshwa kufikishwa hospitali mfano mtu anavamiwa leo inaonekana hapa hawawezi sasa mpaka afike Afrika ya kusini au Uingereza anakuwa kasha cheleweshwa matokeo yake anafika na kufa.
Gharama za uendeshaji wa hospitali hii zitakuwa ndogo kwani haihitaji watu wengi. Inahitaji madaktari bingwa kama watatu mfano wa moyo, upasuaji mishipa ya fahamu, magonjwa kama kansa na UKIMWI na manesi wachache sana. Hii ni muhimu kwasababu serikali katika bajeti yake ya 2013/2014 imetenga shilingi bilioni moja kwaajili ya mazishi ya viongozi na pia imetenga shilingi milioni 18 kwa ajili ya wajumbe wa tume ya katiba watakaopata UKIMWI wakiwa kazini. SERIKALI INA AKILI!

Nchini Uingereza waziri wa elimu aliwahi kulazimishwa kujiuzulu baada ya kusema hali ya elimu katika shule za umma(Public Schools) ni nzuri wakati mtoto wake alikuwa anasoma shule ya binafsi. Wabunge wakamwambia hana udhu ya kusema hivyo kwasababu ingekuwa ni kweli hali ni nzuri mtoto wake naye angekuwa anasoma huko. Aliachia madaraka mara moja. Hapa kwetu?
[h=1]JK aenda kuchunguzwa afya Marekani[/h]
Rais Jakaya Kikwete, ameondoka nchini kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa Rais Kikwete aliondoka juzi Jumatano na kwamba kulingana na ratiba ya uchunguzi wa afya yake anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, haikueleza bayana tatizo linalomsumbua Kikwete mbali ya kusisitiza kuwa amekwenda huko kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Taaarifa za hali ya afya ya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2009, ikiwa ni siku chache tu baada ya kushindwa kukamilisha hotuba aliyokuwa akiitoa kwenye sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Rais Kikwete alilazimika kukatiza hotuba yake na kwenda kwenye chumba cha mapumziko kwa muda wa dakika 10 kutokana na kile kilichoelezwa na daktari wake kuishiwa nguvu.

Source: Mwananchi 20/12/2013

Hapa ndipo msingi wa hoja yangu ulipo. Miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru viongozi wetu hawawezi kuchunguzwa afya zao na kutibiwa kwenye nchi zao kama Mandela. Halafu huyu huyu kesho anasimama jukwaani na kutangaza kuwa "tumeimarisha sekta ya afya kwa kujenga hospitali na kusomesha madaktari wengi kuliko wakati tukipata uhuru wakati yeye mwenyewe hatibiwi na madaktari hao. Kisha utamsikia akisema "tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele.." Huu ni unafiki. Ni mabilioni mangapi yanateketea kwa safari na matibabu ya viongozi wakubwa nje? Je kwanini wasitumie mabilioni hayo kujenga hospitali ya "nyota tano" ili nao watibiwe na kufia hapa hapa?
 
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
10,340
Likes
6,699
Points
280
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
10,340 6,699 280
Tumia akili wewe, kwahiyo Viongozi ndio mnamaana sana kuliko sisi wanachi, Badala kusema Idadi ya vitanda ingozwe na kujenga Hospitali za Uwakika Kila Mkoa na Kila wilaya. Unakuja na Ufujaji wa fedha wakati muhimbili tu hapo wagonjwa wanalala chini.
JK aenda kuchunguzwa afya Marekani

Rais Jakaya Kikwete, ameondoka nchini kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa Rais Kikwete aliondoka juzi Jumatano na kwamba kulingana na ratiba ya uchunguzi wa afya yake anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, haikueleza bayana tatizo linalomsumbua Kikwete mbali ya kusisitiza kuwa amekwenda huko kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Taaarifa za hali ya afya ya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2009, ikiwa ni siku chache tu baada ya kushindwa kukamilisha hotuba aliyokuwa akiitoa kwenye sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Rais Kikwete alilazimika kukatiza hotuba yake na kwenda kwenye chumba cha mapumziko kwa muda wa dakika 10 kutokana na kile kilichoelezwa na daktari wake kuishiwa nguvu.

Source: Mwananchi 20/12/2013

Hapa ndipo msingi wa hoja yangu ulipo. Miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru viongozi wetu hawawezi kuchunguzwa afya zao na kutibiwa kwenye nchi zao kama Mandela. Halafu huyu huyu kesho anasimama jukwaani na kutangaza kuwa "tumeimarisha sekta ya afya kwa kujenga hospitali na kusomesha madaktari wengi kuliko wakati tukipata uhuru wakati yeye mwenyewe hatibiwi na madaktari hao. Kisha utamsikia akisema "tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele.." Huu ni unafiki. Ni mabilioni mangapi yanateketea kwa safari na matibabu ya viongozi wakubwa nje? Je kwanini wasitumie mabilioni hayo kujenga hospitali ya "nyota tano" ili nao watibiwe na kufia hapa hapa?
 
MSHINO

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Messages
861
Likes
24
Points
35
MSHINO

MSHINO

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2013
861 24 35
Hospitali maalumu kwa viongozi ipo pale Victoria alipokuwa amelazwa marehem mzee wetu Kawawa.
 
MSHINO

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Messages
861
Likes
24
Points
35
MSHINO

MSHINO

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2013
861 24 35
Km Rais mwenyewe na familia yake wanatibiwa ulaya wananci wake wafanyeje? awsubiri kufa tu kwa sababu hawawezi kwenda ulaya. Na hii ingetosha kuwaondoa madarakani. km hawataki kuleta huduma bora za afaya basi watibiwe hapa hapa tujue moja.
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Likes
5
Points
135
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 5 135
[h=1]JK aenda kuchunguzwa afya Marekani[/h]
Rais Jakaya Kikwete, ameondoka nchini kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa Rais Kikwete aliondoka juzi Jumatano na kwamba kulingana na ratiba ya uchunguzi wa afya yake anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, haikueleza bayana tatizo linalomsumbua Kikwete mbali ya kusisitiza kuwa amekwenda huko kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Taaarifa za hali ya afya ya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2009, ikiwa ni siku chache tu baada ya kushindwa kukamilisha hotuba aliyokuwa akiitoa kwenye sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Rais Kikwete alilazimika kukatiza hotuba yake na kwenda kwenye chumba cha mapumziko kwa muda wa dakika 10 kutokana na kile kilichoelezwa na daktari wake kuishiwa nguvu.

Source: Mwananchi 20/12/2013

Hapa ndipo msingi wa hoja yangu ulipo. Miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru viongozi wetu hawawezi kuchunguzwa afya zao na kutibiwa kwenye nchi zao kama Mandela. Halafu huyu huyu kesho anasimama jukwaani na kutangaza kuwa "tumeimarisha sekta ya afya kwa kujenga hospitali na kusomesha madaktari wengi kuliko wakati tukipata uhuru wakati yeye mwenyewe hatibiwi na madaktari hao. Kisha utamsikia akisema "tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele.." Huu ni unafiki. Ni mabilioni mangapi yanateketea kwa safari na matibabu ya viongozi wakubwa nje? Je kwanini wasitumie mabilioni hayo kujenga hospitali ya "nyota tano" ili nao watibiwe na kufia hapa hapa?
Serikali hii inaongozwa na majambazi, na matapeli wa ccm.
 
A

Alex Katto

Senior Member
Joined
Mar 3, 2013
Messages
155
Likes
1
Points
0
Age
26
A

Alex Katto

Senior Member
Joined Mar 3, 2013
155 1 0
Sasa kaka malezo yako na ishaur ni vizur lakina unaposema iwe ni kwaajili ya viongozi unakosea, kwani viongozi sio watu? We sema itengenezwe hosptali ambayo ipo full kila kitu kwa ajili ya nnchi.
 
Forum statistics

Threads 1,251,558
Members 481,767
Posts 29,775,953