Igunga ni onyesho la vita halali dhidi ya mafisadi na watetezi wao

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234



Kwa hali yoyote ile matukio ya Igunga yanayotokana na kampeni za uchaguzi ni mapambano halali dhidi ya ufisadi uliokithiri chini ya mfumo wa serikali ya chama tawala – CCM.

Jimbo la Igunga lilikuwa linashikiliwa na Mbunge Rostam Azizi – fisadi aliyekubuhu kwa hujuma dhidi ya Watanzania kwa ujumla wao, ingawa inadaiwa alikuwa anawaendeleza watu wa jimbo lake kwa kuwafanyia mazuri mengi.

Nasema ‘inadaiwa’ kwani hali inayojionyesha sasa hivi hiyo ni dhana iliyokuwa inasambazwa tu kipropaganda, kutokana na wana-Igunga wengi kuwaunga mkono CDM kutokana na sera zake za kuikwamua nchi kutoka katika ufisadi ili kuikwamua nchi ili ipate mandeleo ya maana.

Kwa hivyo Igunga chini ya Rostam ilikuwa ni alama tosha ya ufisadi na hivyo mapambano yanayoendelea kulikomboa jimbo, kitu ambacho kinaelekea kutimia na hivyo kuwatia kiwewe wachache katika CCM ambao wameamua kubeba silaha na kuzitumia katika kulinda minofu yao iliyo vinywani na ambayo inawawia vigumu kuitema.

Kwa kiwewe chao, sasa hivi katika kampeni zao hata hawatangazi zile ahadi zao lukuki ambazo wana-Igunga wameng’amua kuwa ni laghai tu, na badala yake wanaendesha kampeni kuwa CDM ni chama cha vurugu!

Nimemwona Mbunge wa viti maalum wa CCM, Bulaya, mwanamama akiwa katika kijiji cha Itumba akiwahutubia wanakijiji wapatao 20 waliohudhuria kusikia uharo aliyokuwa akiwaambia – eti wakimchagua mgombea wa Chadema basi nchi itaingia katika vita kama vile Burundi nk, na badala wanavijiji kwenda kuhudumia mashmba yao watakuwa wanajifungia ndani kuogopa vita.


Sijawahi kusikia hotuba ya kipumbavu kama hiyo. Hakutaka kuwaambia kwa nini wanatumia jembe la mkono miaka 50 baada ya uhuru, elimu duni, maji taabu, zahanati bila dawa -- huku nchi yao (pamoja na jimbo lao la uchaguzi) lina utajiri mkubwa wa madini ambayo yanasombwa kwenda nje huku nchi ikipata punje tu ya malipo (3% royalty)?


Hebu fikiria Tundu Lissu atakapokwenda katika kijiji hicho cha Itumba na kuwaambia ukweli huo kwa nini wana shida hizo, na CDM ikiingia madarakani itafanya nini kuwakwamua, ikianzia na kuyaokoa mabilioni ya hela yanayoingia katika mifuko ya mafisadi vigogo ndani ya serikali ya CCM, ambao wawakilishi vikaragosi vyao vimeingia Igunga na silaha wanazotembea nazo wazi wazi viunoni, na wengine kuzifyatua ili wana-Igunga na wananchi wengine waendelee kuzama katika dimbwi la ufukara.


Igunga ni vita halali kati ya ufisadi na watetezi wao, na wapenda haki na maendeleo. Ni vita ngumu kwani mafisadi wana-control dola na vyombo vyake, lakini hawana nguvu ya umma. Ni mapambano ya kijasiri kabisa.

 
Back
Top Bottom