kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
- Thread starter
- #41
Haya ndo yanayosemwa na jimbo la Geita Mjini mkuu! Rogers Ruhega ambaye ndiye aliyepeperusha bendera ya Chadema mwaka 2010 na kuwapa CCM ushindani wa kutosha ameambulia nafasi ya 3 kwenye kura za maoni!! Na nimeambiwa yanayosemwa mtaani ni haya haya kwamba walioshinda wamepiga goli la mkono!! Ngoja tusubiri tuone.
CCM wamebadilisha mbinu mwaka huu wanaingiza fedha kwa wajumbe na kumpigia kampeni mjumbe dhaifu ili wao wakisimamisha wa kwao ashinde kiurahisi, kwa hiyo CHADEMA makao makuu kama wana nia ya dhati kuhakikisha CHADEMA(UKAWA) wanaingiza wabunge wengi Bungeni wafuatilie kwa umakini mkubwa sana matokeo ya kura za maoni katika majimbo yote wasipoangalia wanaweza kushitukia idadi ya wabunge inapungua kuliko ilivyo sasa kwani fedha za ESCROW zinafanya kazi yake muda huu.