Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Camillus Wambura amesema jeshi hilo halitovumilia mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuvunja amani ya nchi kwa namna yoyote ile.
IGP Wambura amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Agosti 11, 2025 katika Shule ya Polisi Tanzani- Moshi.
“Jeshi la Polisi liko imara na litaendelea kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa shwari wakati wote na halitomvumilia mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuvuruga amani ya nchi yetu kwa namna yoyote ile.” Amesema Camillus Wambura.
Aidha amesema hivi karibuni vilijitokeza vikundi vya baadhi ya watu kwa mwamvuli wa siasa, demokrasia na uanaharakati na kuanza kuleta taharuki na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kutoa maneno ya uchochezi katika majukwaa mbalimbali yakiwa na uelekeo wa kuvuruga amani ya nchi na tayari jeshi la polisi limechukua hatua stahiki za kisheria kudhibiti vitendo hivyo vya kihalifu na sasa hali ni shwari.