Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Ujue yeye ana Jeshi akitoa amri wewe ndiyo utaumia na wala siyo huyo Lissu yeye atakjmbilia Ubelgiji au na wewe tayari una uraia wa Ubelgiji.
Mbona unachekesha, eti Sirro ana jeshi, jeshi gani? Yaani huyu Sirro ambaye kwa taratibu anatakiwa ampigie Mh. Lissu saluti! Acha utani, wenye jeshi ni wananchi na hata hiyo serikali iliyopo madarakani ni ya wananchi japo wapo wapumbavu hata hilo hawalijui. Kumbuka Tanzania itaendelea kuwepo bila CCM, bila Chadema, bila Magufuli, bila Sirro, bila wewe, bila mimi na bila vichaa wote wanaoamini wana hati miliki ya taifa hili.
 
Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
View attachment 1587125
Moshi ule ugeni mliouhitaji kwa mahaba makubwa, IGP amewalahisishia. Lissu itikia wito na kisha nenda kaendelee na kampeni zako KLM. Natambua wanataka kukutoa ktk reli kipindi hiki, yaani huku kikao cha maadili cha tume ya taifa ya uchaguzi, kule wito wa polisi, lkn popote ulipo wananchi wenye kukuunga mkono wapo.

Mpe nafasi sasa Zitto naye aendelee na mapambano kusini mwa nchi yetu. Ni lazima kitaeleweka tu mwaka huu.
 
Talk is cheap utekelezaji wa sheria inabidi uwe consistent ili message ifike na watu waheshimu taratibu. Just as my man Skinner did with his pigeons you got to set the right operant conditionings.

We get it vyombo vya ulinzi na usalama vina sympathy na Lissu na wamejitahidi vya kutosha kumfumbia macho. But Lissu is a mental case siku zinavyoenda na hizi empty threats ndio anazidi amini Tanzania inamuogopa yeye na huyo Amsterdam wake.

Something needs to be done kumrudisha kwenye mstari afanye siasa za kistaarabu na kuacha kujifanya a ‘demagogue’ wanna be or else; hakuna namna.
 
Unafikir Lissu ni Lowassa au Kamuulize afande Muroto mzee wa kipigo cha mbwakoko na ushupavu wake na vitisho ila kwa Lissu alinywea maana Lissu alimfuata live akamwambia mzee nipe gari langu

Achana na huyo muulize huyo kamanda wa Nyamongo alipokuwa anapiga watu mabomu baada ya Lissu kumfuata ikawaje ikabidi asalimu amri

SASA IKO HIVI Lissu ni kama Mafuriko kabla ya kukukumbuka unaweza sema sijui tunayazuia hivi au vile ila yakikukumba lazma uhame nyumba
Kama huamini subiria baada ya kwenda huko kwa Sirro kitatokea nini lazma Siro atakuja na lugha za kistaarabu ambazo wewe Mataga hutotegemea
Lisuu ni 🔥🔥🔥🔥🔥 Mungu yuko ndani yake wazee
 
Mbona unachekesha, eti Sirro ana jeshi, jeshi gani? Yaani huyu Sirro ambaye kwa taratibu anatakiwa ampigie Mh. Lissu saluti! Acha utani, wenye jeshi ni wananchi na hata hiyo serikali iliyopo madarakani ni ya wananchi japo wapo wapumbavu hata hilo hawalijui. Kumbuka Tanzania itaendelea kuwepo bila CCM, bila Chadema, bila Magufuli, bila Sirro, bila wewe, bila mimi na bila vichaa wote wanaoamini wana hati miliki ya taifa hili.
What is your point here!!?
 
Talk is cheap utekelezaji wa sheria inabidi uwe consistent ili message ifike na watu waheshimu taratibu. Just as my man skinner did with his pigeons you got to set the right operant conditionings.

We get it vyombo vya ulinzi na usalama vina sympathy na Lissu na wamejitahidi vya kutosha kumfumbia macho. But Lissu is a mental case siku zinavyoenda na hizi empty threats ndio anazidi amini Tanzania inamuogopa yeye na huyo Amsterdam wake.

Something needs to be done kumrudisha kwenye mstari afanye siasa za kistaarabu na kuacha kujifanya a ‘demagogue’ wanna be or else; hakuna namna.
Kwan mkuu kamchokoza nani
Lissu anaongea kitu live and direct kwan si bima ya afya iko kwenye ilan yao
Kwan vipalata si wizi mtupu kuna picha ya muhusika pale hizo pesa zinapitiwa na mkaguzi wa serikali acha mawazo finyu kama ni uongo kwa nn deni la Taifa lifike 64% tok 40% this is fucking shit we cant entangain wizi afu akisema manasema akaripoti polisi Kwan hao askari si nduguzetu wanaishi Mbinguni ama wanavuta hewa ya carbon monoxide si oxgen wacha mtu aseme hali halisi ndo utaratibu wake 💯🤸🏿‍♀️🤸🏿‍♀️🤸🏿‍♀️🤸🏿‍♀️🤸🏿‍♀️🤔🤔🤔
 
Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
View attachment 1587125

Na safari hii yasifanyike makosa.
 
Nyinyi endeleeni kumvimbisha kichwa tu huyo Lissu. Atakapoanza kunyea ndoo mtakaa kimyaa kama wakati ule Faru John ananyea ndoo mlikuwa mbaliii.
Kiongozi wa upinzani siku zote lazima ujiandae kisaikolojia na kunyea ndoo si rahisi kupambana na mwenye dola usipokuwa jasiri
 
Hata Siro anatakiwa kutumia hekima sasa kila sehemu Lissu anapokwenda watu wanatamani kumfata sasa aende Moshi kituoni ni Kama anamfanyia kampeni mpaka polisi maana polisi watakuwa wamefanikiwa kufatwa na mgombea wa kiti cha uraisi na tume hivyo hivyo sasa hapo wajiongeze.
 
Lissu hawezi kwenda huko.

Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zinaelekeza Serikali au mdau yeyote asiyeridhika na mwenendo wa mgombea kupeleka malalamiko kwenye Kamati ya Maadili ya Uchaguzi. Polisi ni sehemu ya Serikali; wadau wengine ni vyama vya Siasa na NEC.

Kwa tangazo hili sasa tunaweza kuunganisha dots kubaini maudhui ya tamko la leo la Ubalozi wa Marekani!

Ninaamini busara itawarudia wahusika kujizuia kuwasha moto kabla ya wakati wake.
 
Siro anatia aibu kutii maagizo, awaambie mapolisi wake waache dabo standard, wafanye kazi kwa sheria na sio maagizo ili kuepuka wasikaripiwe.
 
Lisu siasa hawezi ugombea uraisi ni kutafuta kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.Yeye badala ya kuwarahizishia kazi zao apendwe anafanya ziwe ngumu na anawafokea

Hawamhitaji MTU wa aina hiyo anayefanya kazi yao kuwa ngumu awe amiri jedhi wao
Uchaguzi mkuu vyombo vya ulinzi na usalama hawatampa kura yeye na chadema kwa kufanya kazi zao kuwa ngumu unnecessary
 
Hata sijaelewa...nani kalalamika kwa IGP?!Aripoti kituoni,kwa amri.ya IGP? ama??
 
Siku zote polisi ndio uwachokoza wapinzani, mabomu ya nini kwa watu wasiofanya fujo.
Hata aibu hawana kipi wanachojifunia Hali maisha yao magumu mbwa choka mbaya 5 yrs Hakuna nyongeza mishahara.
 
Hata sijaelewa...nani kalalamika kwa IGP?!Aripoti kituoni,kwa amri.ya IGP? ama??
Yule bwana baada ya kumuagiza mahera wa tume asiyejua Sheria za tume kugonga mwamba kaamua kumtumia ziro kumpiga biti,huu wito wa mitandaonii utaishia kwenye mitandao hivyo hivyo.
Hakuna kosa kumfokea polisi asiyefata sheria.
 
Back
Top Bottom